Iringa: Ziara ya Chongolo yampa nyumba Balozi wa Nyumba Kumi

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
ZIARA YA CHONGOLO YAMPA NYUMBA BALOZI WA NYUMBA 10

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ameongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa nyumba ya makazi ya Mwenyekiti wa shina (Balozi) namba saba katika Kijiji cha Ilambilole Kata ya Kising'a iliyopo Jimbo la Isimani katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

Chongolo ameongoza harambee hiyo wakati wa ziara katika ubalozi huo ambapo viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi walioambatana naye kwenye ziara hiyo walichangia vifaa vya ujenzi na fedha taslimu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo.

Ameagiza ujenzi wa nyumba hiyo uanze haraka ili kiongozi huyo ahamie na kwamba ikishakamilika atahudhuria sherehe ya uzinduzi.

Balozi huyo Rose Nzelemera anaishi katika nyumba ya kupanga jambo ambalo liliwafanya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kumchangia ili apate nyumba yake binafsi kwa sababu kiongozi wa shinda ndio mtu anaye anakipigania chama.

Chongolo yupo Iringa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM, kuhamasisha uhai wa chama ngazi za mashina, pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wananchi akiambatana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Sofia Mjema na Katibu wa NEC, Oganaizesheni Issa Ussi Haji Gavu.

FB_IMG_1685452342822.jpg
FB_IMG_1685452345935.jpg
FB_IMG_1685452352846.jpg
FB_IMG_1685452356111.jpg
 
Mwambie Chongolo wako wengi sana kama tafiti zinavyoonyesha

IMG-20180405-WA0006.jpg

Ushahidi mwingine huu hapa

FB_IMG_1575390792397.jpg
 
CCM imeleta umasikini wa kipumbavu sn, hii ni nyumba ya kuishi binadamu kweli tena kiongozi? shame on them
 
Sasa hapo CCM ifanyeje? Watu wanavuna mazao na kula bata hawakumbuki kujenga....
Unatunza hekari moja kwa laki 8 lakini unavuna gunia 6 za mahindi kila gunia ni 40,000 = 240,000, kumbe serikali ya CCM inatakiwa itafutie watu masoko, kuwe na viwanda vya kutosha ajira ziwepo, mi nimelima kwa gharama kubwa sn lakini mpk sasa sijui nitauza kwa shs ngapi nikivuna. Ni aibu na ujinga leo hii Tanzania kuagiza mafuta ya kula, sukari nje
 
Mimi nina mtu namfahamu ana miaka 75. Siku amefariki eti kwake hamna choo wanajisaidia porini. Home ana mifugo ana mashamba...hili nalo la CCM?
 
Back
Top Bottom