Waamuzi 16:1-22
Samsoni akaenda Gaza, akaona huko
mwanamke kahaba, akaingia kwake. Watu wa
Gaza wakaambiwa, ya kwamba, huyo Samsoni
amekuja huku. Wakamzingira, wakamvizia usiku
kucha, penye lango la mji, wakanyamaza kimya
usiku kucha, wakisema, Na tungoje mpaka
mapambazuko, ndipo tutamwua. Basi Samsoni
akalala hata usiku wa manane, akaondoka
katikati ya usiku, akaishika milango ya lango la
mji, na miimo yake miwili, akaing’oa pamoja
na komeo lake, akajitwika mabegani,
akavichukua hata kilele cha mlima ule
unaokabili Hebroni.
Imagine mtu anaenda kupiga shoo katikati ya maadui zake.