Irudie asili yako, wewe ni mkuu wa hii Dunia

Irudie asili yako, wewe ni mkuu wa hii Dunia

Jitu la kienyeji

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,445
Reaction score
7,987
Tukiwa wadogo tulishika tofari mkononi tayari kwa kujitwisha kichwani safari kuanzisha.

Tulipita kwenye hii Hatua, ilikuwa ni kipindi tunatafuta Hela ya daftari na kalamu, uku mama akiwa mstari wa mbele kunipa Moyo.

Mwanangu utafanikiwa tu na wewe usijali, "soma mwanangu soma"

Na leo tupo chuo tuko kwenye hatua nyingine ya mapambano bado tunayasaka Mafanikio yaliyo kwenye elimu na huku chuo nako naona changamoto nyingi zinanikabili, mawazo mbalimbali yananijia mazuri na mabaya.

Kiufupi tu mambo hayaendi.
-Kwenye hili Mungu tu ndo Mtatuzi wangu

Nivile tu kijana nipo katika ujana wenyewe ambao bila akili ya ziada kutoboa nyavu ni changamoto, hivyo inahitaji kutumia ujasiri na Hekima nyingi kufanya maamuzi bila kujali Hadhira itapokeaje na itakuchukuliaje juu ya Maisha unayo amua kuyaishi

(ZINGATIA: Ilimladi tu Mtazamo wako na maisha yako hayana ubaya na Jamii/ikiwa ni uhalisia wa jamii, uko huru kuyaishi mawazo yako)

Vijana wengi wakiufikia ujana huwa wanazidiwa na ujana, maana ujana una mambo mengi yanayo hitaji Busara katika utatuzi wake,
Ujana unahitaji akili ya ziada ili kuuelewa, bila akili hiyo kijana utajikuta wewe ndo wewe tu, lugha zote zako, tabia zote zako, yaani kijana na ujana Vimeumana.

Kuna uhuru wa kusema lakini hauwezi kuwa uhuru baada ya kusema, kijana kuwa makini, Wahenga hawakuwa wajinga walivosema
"UJΔNΔ NI MΔJI YΔ MOTO"

ZINGΔTIΔ: kijana kipindi chako icho kitumie vizuri kuandaa vizuri taarifa yako ya habari ya Uzeeni mwako, usije ukaishia tu kuchanganyikiwa na mambo ya ujanani, hayo ni ya moto inabidi uwe na kipozeo.

Nilipo kuwa mdogo miaka ya 2002 nilipelekwa shuleni 𝑣𝑖𝑑𝑢𝑑𝑢 mpaka 2003 na mwaka ulio fuatia nkapelekwa Msingi (nikifuatiwa na kauli mbiu kutoka ughaibuni ati! "Haki elimu",

hakika macho yangu yalianza kuona mbali, yalianza kuangazia hivi
Je! Ivi mimi nikisoma ntafanya kazi gani?

Yaliangaza kazi zote hakika haikuwepo maana mm nilikuwa nikiuwazia 𝙪𝙝𝙪𝙧𝙪 wa mtu akiwa kazini hicho tu ndo kilicho nifanya nikaanza kuona kazi zote hazinifai uko selikalini maana kazi zote hua wanamasharti yao kazini kwao, me tatizo ni hayo masharti sikuyataka.

Kule kunyenyekeana me ndo skutaka.

Niliona mbele yangu kuwa me sitakiwi kusimamiwa na mtu kwenye maisha yangu nitajiingoza mwenyewe, maana nyuma yangu yupo
🇲‌🇺‌🇲‌🇧‌🇦‌ 🇼‌🇦‌🇳‌🇬‌🇺‌ alie umba waafrika wote Yaani Watu weusi

Huyo ndo kiongozi wangu pekee, Ambae aliumba watu wake wakiwa wamejitosheleza kwa kila idara.

Nilichukia elimu miaka yangu yote mpaka sasa sjawai kuikubari japo kwa akili za Dunia hii ya leo ilio chini ya Backup ya Wazungu bila elimu utaonekana mjinga huna lolote.

Kwenye hii Dunia, ubatiri mtupu. Kitu ambacho sio kweli maana Elimu yao inamfanya Mwafrika kuipoteza histolia yake, mfumo wake wa kuishi, kula, kulala. Tumeikataa elimu yetu ya Kiafrika leo hii imepotea kabisa, nilikuja kutambua ujanani kuwa kumbe Africa Ina mfumo wake wa Elimu ulio potea ndo maana mimi huu mfumo wa kigeni ulinisumbua sanaa japo kwa kukokotana na familia yangu nkafika chuo lakin kichwani mwangu haijawahi kueleweka, maana ninaasili yangu inayo ning'ang'ania nisiiache.

NYUMBANI KWETU AFRIKA lakini leo watu wanaikimbilia asili ya Wageni ndo maana tunaishia tu kuwasifia kuwa wao ndo watu Vichwa sana Duniani hamna mfano, wakati ni mifumo yao na sio yetu ndo maana ili tuijue lazima wao watufundishe namna ya kuitumia, wanachanganya uongo na ukweli umoumo alafu wao wanafundishana ya ukweli tupu sasa.

Mtu mweusi utaponea wapi?
H͞a͞k͞u͞n͞a͞ j͞i͞p͞y͞a͞ c͞h͞i͞n͞i͞ y͞a͞ J͞u͞a͞ vyote unavyo viona vilikuwa pale mwanzo tofauti ni majina tu
Wasomi wengi wa Elimu ya kizungu na Ujumbe huu wataona kama me nimewehuka, wataona ujumbe huu ni kama Tamthilia za kuwapotezea muda pindi wakiwa wamesongwa na mawazo, afu mimi ntawambia tu kuwa mimi nipo kwa ajili ya Watu wenye akili ya ziada kuchanganua mambo na sio nyie mlio lishwa Matango poli na Wazungu toka Ughaibuni, tena nipo kwa ajili ya Watu weusi walio tayari kuilejea asili yao na kubeba Tofari tayari kwakujitwisha kuianza safari ya kuijenga Afrika huru.

Me ni Ben
Mtu huru
Usijidanganye kama ati mimi ninakuogopa wewe, mimi ?
Sjawai na siwezi ijapo kua naheshimu Mtu,
Hatakama unatisha, sio kwangu mimi![emoji33]

- Hii Dunia inawatu wasio stahili kuwemo kwenye hii Dunia, na hao ndio wanao fanya Mtu mweusi ambaye ni haki yake kuishi na kuitawala Dunia hii aanze kuiona hii Dunia sio mbaya ila walimwengu ndio wabaya,

Muda mwingine mimi nawaza ni ukuu wa na namna gani Mtu mweusi alionao?, uzuri ukioje? Nguvu za namna gani Alizo nazo? Yaani kiufupi tu Mtu mweusi ni nani hasa? Mpaka agombaniwe na kila taifa linalo jitapa leo hii kuwa ndio wenye Demokrasia, wenye nguvu kijeshi, nwalio vizuri kiuchumi nk, nyanja zote za maisha, Mataifa yote ya Weupe yanahangaika kuitafuta elimu ya kumsoma mtu mweusi ni Ameumbwaje, ili wampoteze na kumfutilia mbali kwenye hii ramani ya Dunia, lakin hawawezi.

Ilimladi tu jua [emoji3508] , Nyota [emoji93] na Mwezi hawajavipoteza Mweusi hawezi kupotea Duniani hapa.

-Na safari hii Mweusi mmoja baada ya Mwingine tumeanza kujazana kwenye Uafrika wetu, sisi ni Weusi tutaijenga Afrika yetu lazima, .Tena tumejipanga vikali kukabiliana na hao wageni wetu walio tuletea 🅓🅘🅝🅘 kisha zikatuponza tukawa watumwa.

🅔🅛🅘🅜🅤 🅩🅐🅞 Kisha zikatupotezea mila na desturi zetu, histolia yetu ikapotea kwa kusoma zakwao[emoji3578][emoji21] tu zetu tukafunzwa kuwa ni mbaya adi leo hii

🅝🅐 🅜🅘🅕🅤🅜🅞 🅜🅑🅐🅛🅘🅜🅑🅐🅛🅘 🅨🅐 🅚🅦🅐🅞 ndiyo inayo tutesea vijana wetu Weusi, vimekua kama kioo cha jamii et!
Iko njia ilio sahihi kwa mtu yeyote Mweusi, iludie asili yako wewe ni Mkuu wa hii Dunia.

Nifuate NYUMBANI AFRICA.
 
Back
Top Bottom