Is Feisal Salum ''Feitoto'' overrated?

Is Feisal Salum ''Feitoto'' overrated?

Ukiwa na jicho la kiufundi utaelewa nini ally amemanisha ila kiushabiki utaona kama ameandka story
 
Naunga Mkono Hoja [emoji137]‍♂️[emoji137]‍♂️

TOO OVERRATED
 
Mlimpeleka mlevi afcon akacheze namba ya mkude

Wengi mlijua ni piere lakini piere hakulipiwa na Tff wala hakucheza namba ya mkude
Hivyo mlevi aliecheza namba ya mkude ni fei alieanguka Mara 8 katika dakika 32 za kwanza
 
Habari wanajukwaa?

Leo kwenye pita pita zangu mitandaoni nimekutana na hiyo mada instagram iliyoandikwa na mchambuzi wa michezo pale Azam tv anaitwa Alikamwe, ameandika mengi kuthibitisha statement yake kwamba Feitoto ni overated kwa mpira wetu hapa Tanzania.

Binafsi sikupendezwa na matumizi ya neno '' Overrated '' kwa nafasi yake kama mchambuzi kwani ni wazi anamkatisha tamaa kijana yule ambae kwa muono wangu kiwango chake kimekua kikipanda siku baada ya siku. Unawezaje kutumia takwimu za mechi moja kuthibitisha mchezaji ni overated? Hii si sawa kwa maendeleo ya vijana hawa.

Karibuni kwa michango yenu juu ya kauli hizi za wachambuzi wetu ambao mara kwa mara wamekua wakitumia akaunti zao vibaya kuandika mambo yasiyofaa kwenye mpira wetu.

Alikamwe amezungumza vyema, Feisal anapaswa kuongeza juhudi kwa kasi ana vitu ambavyo ukitazama unaona anashindwa kuvitumia, Sasa ukimpaisha zaidi Ndio wamdumaza
 
Gift mauya ni bora kuliko huyo mpemba.Kuna yule mwingne anaitwa ndemla yuko pale mikiani,wanamsifia kwa kupga mashuti lakni yote yanaenda nje.
Mimi ni simba lakini ndmla ana papara sana ndio sababu inawezekana ana short off target nyingi kuliko mchezaji yoyote katika vpl
 
All in all, Fei Toto ni fundi. Akiufanyia kazi huo ushauri, atafika mbali. Ni kweli kadogo bado kana umayai mayai! Kakiongeza stamina ya mwili wake, pumzi ya kutosha, akili ya kushambulia zaidi kuliko kutoa pasi za kusifiwa na mashabiki, akirudisha yale mashuti yake ya kushtukiza, hakika tutakafukuza ili kakajaribu bahati yake nje ya nchi.
Ajifunze kwa muzamir
 
Hili nilidhani naliona peke yangu namna feisal anavyozungumzwa na mashabiki wa yanga na uhalisia wa kiwango chake ni vitu viwili tofauti dogo ana uwezo wa kawaida sana ila huenda ana kipaji kikubwa hivyo anapaswa aongeze juhudi kuwa bora zaidi, Ali kamwe kaandika kwa nia ya kumjenga japo si wote watatafsiri hivyo
 
Ali Kamwe kijamaa kina ndonga kama mzinga wa nyuki...kila timu na style yake ya kucheza..kiungo wa Barca atapiga pass nyingi kuliko kiungo wa Madrid...hivyo hivyo kiungo wa Simba atapiga vishort passes vingi kuliko wa Yanga
 
Back
Top Bottom