Nini mtazamo wako katika hili?
MJ1,
Naona umetumia maneno matatu (ku-spy, ku-monitor, na Kuchunguza (investigate?)) ambayo kimsingi yanaweza kuwa na majibu tofauti.
Ku-spy ni kuiba au kupata taarifa fulani
kwa siri (mara nyingi taarifa kutoka kwa adui yako). Kwa msingi huu, sioni sababu ya kum-spy mwenza wako. It is really unethical especially kama hakuna enemity kwenye hiyo relationship. Ni matumizi mabaya ya preveleges zinazopatikana kwenye ndoa.
Ku-investigate (kuchunguza), hapa lengo ni
kupata taarifa zaidi (details)juu ya jambo fulani mahususi ili
kujua ukweli. Hii halihitaji kufanywa kwa siri. Inaweza pia kujumuisha mahojiano na muhusika. Ni muhimu sana kufanya uchunguzi juu ya jambo fulani kabla ya kulifanyia maamuzi iwe ni katika ndoa ama katika mahusiano ya kawaida.
Ku-monitor, hapa unaangalia kama reality ina conform na expectations zako au makubaliano katika muda fulani kwa lengo la
kurekebisha kama kuna unacceptable/intolerable deviations. Mara nyingi katika mahusiano 'monitoring' inatokea unconsciously (ingawa hata consciously kama kuna kitu maalumu mmekubaliana - kwa mfano kuacha pombe, sigara etc) na binafsi sioni kama ni mbaya.
Investigation inaweza kuanza kutokana na matokeo (feedback) ya monitoring. Kama kwa mfano expectations zako ni kuwa mume awe nyumbani by saa mbili usiku. Unconsciously, utakuwa unamonitor muda anaourudi,na endapo ataanza kuchelewa kurudi, tayari utapata feedback kuwa sasa anarudi baada ya saa mbili. Kama hili ni tatizo kwako unaweza anzisha uchunguzi wa kwa nini anachelewa kurudi. Uchunguzi unaweza kuwa kumuuliza tu kwa nini anarudi muda tofauti na zamani na unakwenda mbele kujaribu kuverify sababu atakazozitoa. Hili hulifanyi kwa siri ni lazima umwambie kutoridhika kwako na muda anaorudi pamoja na sababu anazozitoa.
Labda nimalizie kwa kusema kuwa hakuna uhuru usiokuwa na mipaka iwe ni katika ndoa ama kwengineko.