Good Guy I will assume wewe ni mtanzania, kwa mtanzania kufungua account ya benki Kenya, swali la kwanza utaulizwa kama una doc zozote au unafanya nini Kenya. Kama ni mwanafunzi au the like hutasumbuliwa ila kama utasema umeenda ki biashara au kikazi, wataomba work permit na KRA pin ( category resident non Kenyan).
Kiukweli kuna usumbufu, sijui kwa nini kufungua tu account kwa kuwa ni foreigner unapewa masharti magumu kama unaomba kazi, njia rahisi ni fungulia Ksh account Tz kwa bank kama KCB au Equity, watakunyima ATM card ila service nyingine zote utapata kama kawaida.