Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu post ndo nimeisoma leo, sina idea ya chochote ulichokielezea, unaweza kunipa msaada gani juu ya mada yako kupata pesa?
Samahani kama nitakuwa nimekukwaza.
Nakutumia mkuuHaujanikwaza mkuu.
Kuuliza si ujinga.
Unaweza nitumia email nitakupatia mafunzo + mentorship.
Upwork mbona hawajaverify account yangu wananitaka nini? Ukipata kazi nyingi na wewe unaziuza kwa watu wanafanya kwa niaba yako
Mkuu tumia Payoneer, mimi ni mdau huko since 2014, huwa natumia payoneer master card, ni cheap sana, hio ya wire transfer iliniumiza sana miaka ile, ukitaka link ya payoneer chukua kule kule upwork au tumia hii hapa Payoneer | Get Paid by Marketplaces & Direct Clients WorldwideInternational/wire bank transfer.
Rahisi tu.
Mkuu tumia Payoneer, mimi ni mdau huko since 2014, huwa natumia payoneer master card, ni cheap sana, hio ya wire transfer iliniumiza sana miaka ile, ukitaka link ya payoneer chukua kule kule upwork au tumia hii hapa Payoneer | Get Paid by Marketplaces & Direct Clients Worldwide
Mkuu post ndo nimeisoma leo, sina idea ya chochote ulichokielezea, unaweza kunipa msaada gani juu ya mada yako kupata pesa?Greetings brothers and sisters.
Leo kama kawaida nipo hapa nataka nikupatie darasa jinsi unavyoweza tengeneza $300+ kwa mwezi katika online platform ya UpWork ukiwa hapa Tanzania.
Haijalishi upo na college degree or darasa la saba. Inachotakiwa ni uwe na weledi katika fani yako lakini pia unafahamu jinsi yakupata kazi unazo apply.
Nasema hivi kwa sababu binafsi nafanya kazi kama Freelancer UpWork na nimepata gigs (kazi) mara kadhaa kwa hiyo nafahamu kitu ninachoenda kukufahamisha.
Kwa mfano sasa hivi ninaendelea na gig (kazi) ya $1,000. Nakamilisha hii ndani ya siku 20. 55% ya kazi tayari.
Angalia hapa.
View attachment 1239945
Ok tuachane na $1,000 leo nataka nikuonyeshe jinsi utakavyoweza kutengeneza $300 kila mwezi ukifanya kazi kwa kutumia skills zako.
Ready?
Let’s go.
1 • Jitahidi upate kazi ya pesa kidogo ukiwa unaanza ili upate reviews lakini pia UpWork wataverify identity yako.
Ok.
Kuna baadhi ya watu wanadhani wakisha register account zao UpWork basi wanaweza ku-apply kazi kubwa zinazohitaji uzoefu mkubwa na kulipa pesa nzuri $5,000 +
You are wrong man.
Hata kama wewe ni experienced katika fani yako kumbuka ukiingia UpWork hakuna anayekufahamu akuamini akupe kazi kubwa angali ndogo tu unaweza kufanya.
Clients wanaotafuta Freelancers wana akili na uzoefu. Hata andika yako tu wakati unaapply kazi wanafahamu wewe ni beginner kwenye hii jukwaa.
Ukiwa unaanza weka focus yako kwenye small gigs upate experience jinsi utakavyoweza kufanya kazi bila kusuasua.
Pia hapa utapata advantage kwa sababu UpWork wata verify Identity yako kwa hiyo clients wataona wewe ni wa kuaminika zaidi na kazi nyingi zitakuja kwako.
Nitakuwa hapa nikikuonyesha proof kadiri siku zitakavyokuwa zinaenda.
2 • Skills zako pekee hazitoshi kama hujui kuuza hizo skills.
Ngoja nikwambie kitu mtu wangu.
Kuwa programmer, translator, graphic design, voice over artist etc haitoshi kukufanya upate kazi UpWork.
Hii huwa naisema sana na leo nitarudia tena.
Ili upate kazi inabidi ujue mbinu za kuuza ujuzi wako.
Kumbuka ili kupata kazi inabidi uwasiliane na client yako sasa hapa usipofahamu mbinu za kukamata attention yake ni ngumu sana hata kama wewe ni mkali katika skills zako.
Nafahamu watu wengi wengi wenye ujuzi wa programming, graphic design and web development lakini hawapati kazi.
Unahitaji kujifunza hili kama kweli upo serious kupata kazi UpWork.
3 • Everything takes time. Kuwa na subira acha papara.
Unajua nini?
Baadhi ya watu hawana subira kwa jambo lolote.
Wanaanza side hustle online wiki hii wiki inayofuata wamechoka wanaacha na kuhamia kwenye mambo mengine.
Mtu wangu ukiona upo na hii habit utapata tabu sana kupata success kwa sababu kwa kama utaamua kufanya kazi gani mafanikio hayatokuja kwa urahisi.
Utahitaji kufanya kazi unayofanya every single day. Tena si kwa wiki chache bali kwa miezi mingi.
Hapo vipi?
Do you have what it takes?
Kwa sababu mara nyingi utakapoapply kazi UpWork chances are utakosa hasa hasa kipindi cha mwanzo. Sasa ili uweze ku-break hii mambo inabidi uwe mvumilivu. Experience ndiyo inakuja kwa namna hii.
4 • Be mindful. Si kila kazi ni ku-apply tu.
Yes.
Beginners hawajui hili.
Si kila kazi inayoendana na ujuzi wako basi inafaa u-apply.
Ukiwa beginner UpWork lenga kufanya kazi zinazoonyesha “entry level au intermediate level”.
Hapo utakuwa na chance kubwa ya kupata kazi.
Does that make sense to you?
I hope it does.
Kazi zinazoonyesha expert level mara nyingi zinahitaji watu walio earn atleast $100 katika kazi zao UpWork. Sasa hapa ukija kichwa kichwa proposal yako itakuwa declined.
5 • Ukishapata kazi za pesa ndogo na kupata review sasa ni wakati waku aim higher $300+ kwa mwezi.
Ok.
Umeshapata kazi chache na review zako ni nzuri. Nini kinafuata.
Kinachofuata ni kuendelea kuwa active huku focus yako ikilenga kupata gigs kubwa zinazolipwa vizuri kwa sababu mosi tayari upo na reviews, identity yako kama Freelancer ipo verified kwahiyo clients wanakuamini zaidi.
Hapa inabidi u-take advantage ya hii opportunity. Binafsi baada ya kufanya kazi chache za pesa kidogo na kupata reviews nzuri lakini pia identity yangu kuwa verified imesaidia sana client wengine kuniamini na kunipatia kazi zao.
Hivi ndiyo pesa ndefu inavyotengenezwa UpWork.
Niishie hapa kwa leo.
Tukutane wakati mwingine.