worry not mdogo wangu
ndoa has everything to do with this coz ndio chanzo cha swali la MJ1
Aksante frank,ni kweli na hii haihusiani na ugonjwa. Ni mtafaruku ambao ulitokea na zikatolewa second chances nyingi tu lakini bado hali iliendelea kuwa mbaya na more abusive mpaka upande mmoja uliposema sasa basi. So hakuna makubaliano ya pande zote mbili na upande mmoja bado una hope ya kurudiwa kwa staili ile ya "huweziishi bila mimi wewe, unanipenda sana mimi".Hii iko 50 kwa 50,inategemea ni kipi hasa kilichowafanya watengane,je ni ugonjwa ama ni mtafaruku tu katika mapenzi,kama ni ugonjwa na wote wakaridhia kuachana inawezekana kabisa wakawa friends na kushiriki masuala mengine ya kifamilia kama ulivyoainisha hapo juu,lakini kama c ugonjwa na waliachana kwa sababu za mitafaruku katika mapenzi kibongo bongo duh HAIWEZEKANI
My self ni vigumu sana kuja kumpenda mwanamke yoyote yule with my all heart, nitakachojitahidi ni kumuonesha kwamba namjali na nampenda lakini whatever the case i have nothing to lose from any woman.
...aha, ok....
hii ina tafsiri tofauti na ninayoizungumzia mimi... kwa kesi hii, cheti cha kuachana kinahitajika hapa
kila mmoja ajue haki zake, otherwise 'mtabakia' mnategeana na kila mmoja kumbebesha mwenziwe mzigo wa lawama.
kuachana kwa amani kupo dear,....zipo sababu zinazokubalisha hali hiyo,
ikiwamo mitizamo tofauti ya maisha, kiimani, au tamaduni...(fikiria nje ya boksi)
kuendelea kubanduana hapo sawa lakini mambo ya aut sijui nini,mie sikubali. Nalog off
Ni ngumu sana,kama haijawahi kukutokea ni rahisi kusema. Thru my ezperience no no noooo.
Pole sana i have been thru that now am very happy with my life.
washawasha nawe bwana, asa unabanduanaje wakati kule ulishalog off??
Some people can and some people can't! I fall in the latter group.
If we share a child and we are no longer together then I believe in maintaining a civil and cordial relationship. I don't see the need for hostilities and/or animosity if we've both resigned to the fact that we can't be together.
But a civil and cordial relationship doesn't mean hanging out together and doing things together. This just means we don't have to be fussing at each other over pointless stuff.
Just be good role models to your kid(s) and enjoy life.
hivi unaanzaje kwanza? Mbona ni kitu kigumu sana! Anyway wengine wana mioyo tofauti.
little angel jamani naomba desa mwenzio maana kweli naona kama inanikera sana kiasi cha kuwa ni mtu wa hacra kila sekunde!
Mdogo wangu MJ1,
Hii issue ni nzito kidogo ila inaelezeka...ingawa si rahisi ki hivyo!
Ninavyojua mimi kuna kutengana (wenzetu hapa wanatoa talaka moja au talaka rejea) na kuachana. Kama ni hali ya kutengana tu, watu wanategemea kuwa wahusika watajipa nafasi ya kutosha kutafakari kama wanaweza kulianzisha tena au ndo things fall apart...Katika hicho kipindi, nafasi yoyote ile inayoweza kupatikana, iwe kupitia kwa mtoto au accidents ambazo zinawapa nafasi ya kukutana na kuangaliana usoni at 180 degrees inaweza kuwa chanzo cha mambo mengine mazito......Hapa nashauri mwanamke awe mwangalifu sana kwa sababu kumwingiza mkenge ex-GF au ex-wife ni rahisi sana kama vile kusukuma mlevi wa gongo!!
Kama watu wameachana, tena katika mazingira ya kiafrika basi sioni kama ni possible kuwa na ukaribu wowote...Nadhani hata mambo ya kulea watoto inabidi yawe kwenye makaratasi na siyo kupitia dialogue za kila mara....Mtakuwa mnatafuta au kuonge ongea nini wakati kila mtu keshaanza maisha yake binafsi with or without a new partner??
Sorry kama sijaeleweka...
Babu DC!!
najua ni kweli lazima upate hasira,for me it took like a year hasira kupungua maana ilikua zaidi ya hasira,kuna wakati nilikua nalia tu maana ckua na plan ya kua single parent. I thought i lost the half of my life. But pia ckua radhi kuendelea na mtu ambaye daily ananihurt moyo wangu. Amekuwa king'ang'anizi for three years mpaka ameamua ku give up. Just be strong and firm kwenye decision my dear.
MJ1,ahsante kwa uzi huu.
Nikupe my personal experince.Nimeoa na kuzaa na wanawake kadhaa,wengine wali go on kuolewa,wengine hadi leo ma living single.Wote ni marafiki zangu,sherehe,misiba kwangu wanakuja,kwao nakwenda na sioni tatizo hata kidogo.
Angalizo:Mwanamke ukizaa naye mka break,leeni mtoto mliozaa lakini usilale naye,utaharibu.
hahahahaha...unastushwa na hilo tu,
kwa taarifa yako, mwanamume (tena wa kiafrika) akimwacha mwanamke anatamani kumwona akiwa kichaa anaokota makopo au amefulia hadi chawa wanagawana vipande vipande vya mwili wake... That way anaamini kweli mungu alikuwa amekutoa kwake ila kwa ujeuri wako sasa unaonja joto la jiwe!! Habari ya watoto haipo kabisa kichwani mwake linapokuja suala la kumfikiria mtalaka wake!!
Mwanamume aliyekuacha akikuona unatanua tena na dume jingine, anatamani akaazime bastola ili asione tena hicho kitu ambacho kinampa pressure kama vile amebakiza dakika 10 kuaga dunia!!
Mwanamume kiumbe tofauti na mnachoona kinatembea njiani....kuwa makini na chukua hatua!!
MJ1 nilichojifunza mimi katika maisha ni kuwa kuachana na mtu does not necessarily mean mmekuwa maadui ,unless mwenzio akufanyie kitu kibaya sana kama kukupeleka jela.Katika kuachana initially huwa kuna temper,with time huwa mna cool off na kuanza hata kuchekana.Kuna mwanamke mmoja nilikuwa naishi naye tukagombana akakomba kila kitu mpaka mapazia,siku hizi huwa namtania na kumuuliza hivi chu....i zangu uliziuza soko lipi la mitumba? Anacheeeeeeka na kusema alizitia kiberiti.Mkizaa ndo kabisa mtake msitake mtaongea tu na mtoto kwenu atakuwa bond ya kudumu.Aksante Bishanga kwa hii experience yako. ninajifunza