hukumpenda kwa dhati wewe naona!!!!!! haaah!
kuna mfanyakazi mwenzangu alioa muislamu na kabila tofauti na lake, akatengwa na ukoo kwamba kaoa chasaka na yule demu pia katengwa kwamba kaolewa na kafri, lkn kwa sababu wao walipenda kwa dhati waliendelea kuishi tu vizuri na wakafunga ndoa ya kiserikali maisha yakaendelea wakazaa na watoto wao, hakuna aliemlazimisha mwenzie kubali dini, wote ni wafanyakazi na ni msaada mkubwa kwa wazazi wao kiuchumi kila mmoja kwa nafasi yake na kwasababu wana hekima hawakusitisha huduma makwao. Baada ya miaka 10 ya ndoa yao, mke bila kulazimishwa alibadili dini kumfuta dini ya mumewe na wakabariki ndoa yao kidini, maisha yanaendelea raha mustarehe, wazazi wao walishasahau zile hasira za mwazo wanafurahia tu kulea wajukuu.