carmel
JF-Expert Member
- Aug 24, 2009
- 2,836
- 265
Sijui kwa nini lakini nahisi kuna cold war kati ya wanawake wenye "videgree" na wale ambao hawakufanikiwa kuvipata hivyo videgree. Nilifatilia thread ya da sophy kuhusu ofa au discount kwa shemeji yake, na pamoja na vijembe vingine vyote nilihisi kama suala la videgree vya mgombea mwenza wake nalo linamkera. Hii si kwa da sophy tu bali hii huwa inatokea mara nyingi hata makazini, mitaani tunakoishi na hata masaloon. Kinachonishangaza ni kwa nini wanawake tusifurahie kuona wenzetu wamekula kitabu, na badala yake hiyo inatumiwa kama kosa kwa muhusika, huku ukisakamwa kuwa unajisikia, unaringa eti kwa kuwa tu una videgree. Mbaya zaidi hii inaingia hadi kwa nyumba ndogo, mawifi au hata jamii kujudge kila unachokifanya kwa mfano ukichelewa kuzaa au ukiamua kuzaa mtoto mmoja au wawili utaambiwa unajidai msomi, ukiamua kumwita mwanao jina ulipendalo unaambiwa unajidai msomi, why? mbona mambo haya kwa wanaume hayapo?anyway am just thinking kwa nini mtu asiamue na yeye kwenda shule na kusoma maana siku hizi hata elimu ya o -level kwa miaka 2 inapatikana:lol: na a-level kwa mwaka mmoja pia ipo. na sio lazima kwenda UDSM leave alone nje ya nchi, bali kuna vyuo kibao kuanzia tumaini, st augustine,sijui ruaha, etc na vingine kibao hata vya utalii colleges, why hating the learned sisters, why?