Is this one Kenyan?

Is this one Kenyan?

Umekwenda kipindi cha Xmas wakati mji umefulia, nenda Jan kati wakati watu wamerejea mishe.
Tena naweza nikakuelekeza wapi uanzie maana Dar napajua sana kuzidi wengi wenu humu.
Nikirudi nitapiga mapicha na kuyaleta humu muone watu wanavyoteseka kisa ukosefu wa mabasi ya kutosha.
Wanajazana stendi, likija inakua vuta nikuvute, halafu milango lazima ifunge, hivyo inabidi msukumane humo ndani muachie nafasi mlangoni, midereva yenyewe imenuna kwa uchovu na ukosefu wa hela, hauwezi kumuuliza kitu.
Madubwasha ya kusoma tiketi ili ikuachie uingie au kutoka stendi haifanyi kazi siku hizi, kuna jamaa wamewekwa hapo kazi yao kukagua hizo tiketi, jamaa wenyewe wachovu huwa hata hawashughulki, unapita tu.
Yaani awali wakati hayo mabasi yanaanza, yalikua nafuu hata kuzidi taxi, nilikua natoka hotelini na kufika mjini ndani ya muda mfupi, lakini kama ilivyo kwa Mswahili, huwa mtihani sana kutunza na kudumisha chema.
Naona ulikuja kutoa ushamba,uje tena upande electric train 2020,Sikh hizi haina haja ya kwenda Europe ni hapahapa bongo wakenya wanakuja kutoa tongo tongo,juzi nipo pale kibo nikakuta watoto wa kagame wanazungumza kilugha Chao wakisubiri bus.lmfao
 
Yaani wakenya wana wivu na chuki mbaya sana,mtu anafikia kusema eti kuku wa nairobi ni watamu kuliko Dat!
 
Hiv unajua km mkenya mwenzenu kaongea mambo ya msingi kuliko huyo bwege ulomleta???!!!!
Mkenya mwenzako kasema ukweli Kenya hamuna muungano mmeendekeza ulafi,ubinafsi na ukabila.
Kitu km hiko hakipo Tz tuna muungano hatujali ubinafsi wala ukabila.
Pima point za huyu jamaa na mkenya mwenzenu.
Halafu akazidi kueleza kuwa mi highway km yote ila bado haikidhi mahitaji.
BRT inahitajika kuwepesisha usafiri wa ummah.
Kaenda mbali zaidi na kusema Dar hakuna slums km Nairobi.
 
mkenya gani asiyejua spelling za kibera eti kibras...mswahili tu huyo anaunga unga tu mitandaoni!
Kumbuka alikua ana type sio kuongea.
Kuna typing error hata ww huzifanya mara nyingi.Kwahiyo usimkatae mwenzako.
 
Na mbona nikiingia google map nikisearch slum ni dar naandikiwa not available [emoji23][emoji23][emoji23]
Lakini nikiandika slum in Nairobi zinakuja nyingi sana.
"Ukweli " kwako ni zile maoni tu zinazo kwenda laini na maoni zako , si ndio?

Kwa hivyo ni ukweli pia wale wanahabari wa kimataifa wamechapisha habari kwamba Dar es Salaam 70% ina slums.
 
Back
Top Bottom