Maisha ya huko Turkana ni zaidi ya maisha ya kuzimu.
Katika karne hii ya sayansi na technolojia watu wanasafirisha watoto kwa kutumia punda.
Turkana ni nchi ndani ya nchi, wapo na jeshi lao. Kila mtu anamilki bunduki. Tangu Kenyatta aingie madarakani sijamsikia akitembelea maeneo yale.
Yesu alitolea mfano kuzimu kwa kutumia shimo la takataka lililokuwa nje ya mji wa jerusalem. Shimo hilo moto ulikuwa hauzimiki lilikuwa linaitwa jehanamu.
Yesu angetokea leo hii angetolea mfano wa kuzimu na Turkana.
Najaribu kutafakari kama kweli shetani(ibilisi) alifukuzwa toka mbinguni na kuangukia duniani, basi huyo ibilisi aliangukia kenya sehemu inayoitwa Turkana.
Napenda kuwauliza wakenya je, mnampango gani na Turkana!? Au mmeitelekeza!?
Njaa, magonjwa, utapiamlo, vita, vurugu, shida ya maji, hakuna umeme, hakuna barabara, mitandao ya simu haisomi, ubakaji.
Kila aina ya shida zinapatikana Turkana.
View attachment 1632351View attachment 1632352View attachment 1632353View attachment 1632354View attachment 1632355