Mbona bodaboda wengine wanaingiza kipato kizuri kwa siku. Kuna boda nafahamiana nae ana stress za mke na biashara kufeli, akawa anakuja kibaruani kwangu kupumzika kupoteza muda. Hana motivation ya kufanya kazi hivyo hakai kijiweni anategemea Bolt kivivu ile sitaki nataka.
Siku moja nikawahi asubuhi jamaa mwingine kumbe aliomba bodaboda na simu ya jamaa usiku akafanyie kazi Bolt. Aliichukua saa tatu usiku akairudisha saa nne asubuhi akaniachia 38,000 nimpe jamaa. Nadhani mafuta hakununua na jamaa alilalamika kuwa nimeachiwa hela kidogo. Ila mabodaboda wengi ninaotumia hata wawe wanafanya kazi kiasi gani hawaweki mafuta ya zaidi ya 20,000 kwa siku.
Bodaboda mwenye akili timamu Dar ni zaidi ya kima cha chini cha mshahara wa serikali.