Ishara 10 za manabii na mitume feki waliotapakaa Tanzania

Kubali kujirekebisha mtu wa Mungu, kwani unapungukiwa na nini. Achana na ubishi usio wa lazima. Hayo mambo aliyoainisha ni kweli tupu,ndivyo mnavyofanya,je? Kwa utashi wako unadhani mambo hayo yanampendeza Mungu?.
Nataka unifunulie huo ukweli. Mimi sio mbishi... Funua ukweli ili huo ukweli utuweke huru... Who is authentic then !!!
 
Kajaribu kuwahubiria . Kuna wachawi wangapi uliwahubiria wakaokoka na kuna manabii wangapi uliwahubiria wakagoma ?
wachawi wengi wameokoka kuliko hao wanao jiita manabii,
https://www.facebook.com/Yesu alikuja kutuponya na si kukanyagisha watu mafuta, hiyo ni ibada ya sanamu na kafara.
huyu hapa nabii wako :
Alikuwa Shoga, sijui kama ameacha
 
Ndani ya mkoa mmoja unawakuta manabii/mitume zaidi ya 5+, wakati maandiko yanasema nabii akizaliwa ujue nabii aliyekuwa akihudumu eneo hilo hana kitambo kirefu. Na nabii siyo kama machungwa kila mkoa unayo[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Dah nimecheka sana mkuu
 
Wanaongoza kwa ushirikina we nimeona kuna gazeti limeandika eti kuna nabii anauza chupi za kike kwa wanawake hivi hapo kuna usalama?
Bora mchawi ana huruma, mkeo akikwambia anakwenda kwa hawa manabii na mitume, kama ni issue ya ndoa lazma aliwe mzigo ndio ahudumiwe;
Hawa jamaa ni matapeli wamejificha kwenye kivuli cha udini.
 
Ni sawa... Tumepewa akili tupime hizo nabii... Lakini kuhukumu sio kazi yetu. Ukiona mafundisho yake hayakufai kaa pembeni. Kuna mwingine kwa mafundisho hayo dhaifu atapata hapo neno litakalomgeuza na kumnusuru na jehenamu !!!
Sawa
 
Unabidii utume utoke wapi nyie jamani dah wakristo mna kazi kweli
 
Hivyo vyeo vya unabii wanapewa na nani alafu wamewateka sana wanawake yaani nabii ana walinzi
 
Waacheni,kila mtu afate anachoamini.
Ata ambao awajiiti manabii na mitume pia wapo waongo na wazushi.
 
Unabii juu ya dunia ulishafungwa, kinachosubiriwa ni mwisho wa dunia sasa hawa jamaa ni unabii gani hasa wanaotoa. Halafu qualification ya kuwa mtume ni kupeleka injili kule ambako haijafika kama alivyofanya mtume Paulo kule Rumi na Asia na namna lilivyofanya kanisa katoliki kupeleka injili karibu dunia nzima. Sasa mtu anajiita mtume wakati yuko hapa hapa bunju ambapo watu wote walishasikia mafundisho ya injili....
 
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, Nyakati za leo hakuna nabii, tangu ujio wa Yesu, mabii walikuwa wanatumika katika jambo fulani kama misingi ama tamaduni vimeharibiwa na watawala, hapo ndipo manabii walikuwa wanakuja, kazi yao kuu ni kutabiri yajayo, kuonya, nakutoa adhabu moja kwa moja ambayo Mungu amezungumza nao, siku hizi kunawanafunzi wa Yesu tunawaita " second disciples" Neno nabii ni neno zito sana, nabii akikutizama lazima utetemeke manake nikama umekutana na malaika, hao ambao wapo leo ni matapeli wanafanya biashara
 
Mpaka leo hii hakuna nabii wala mtume aliyetuambia corona inaisha lini,,ila wanasubiri wanasayansi wagundue dawa na wao ndo waanze kuponya corona kwa miujiza
 
Leo hawa manabii na mitume wetu wamepewa stahiki yao, kwakweli wanachokifanya sio kitu kizuri, wanatumia changamoto za maisha ya watu, na hasa wanawake, kuwa ndio mitaji yao ya kupigia hela. Wamwogope Mungu Mungu kwakweli
 
Atakua Jamaa fulani anajiita Mtalemwa, Son of Major one, anapatikana makongo juu pia huyu jamaa
 
Aiseee mleta uzi umegonga mulemule kwa matapeli wajasilia dini , their are taking advantage of ignorance of the mass .Mimi mwenyewe nikiwa kama dereva wa wazito nimekutana na manabii na mitume uchwara wengi kwa waganga wa kienyeji , wakifuats dawa za kujaza watu na nguvu za kufukuzia mapepo . Ushahidi ninao nitaandika Uzi hapa nikipata muda ili watu waweze kujifunza .
 
Hao tumeishawashitukia,hiyo ni njia ya kupiga hela tu,hakuna kitu hapo,
Kuna bango moja huwa naliona pale Mwenge,Dar,eti "clinic ya yesu'harafu Kuna picha ya kuuzia sura.huwa nacheka sana,
Mwanzoni Hawa manabii walikuwa wakishindana kuweka picha zao kwenye mabango ya matangazo,sasa hv Kuna fasheni imekuja wanaweka picha zao wakiwa wamekumbatia wake zao,
 
Ndani ya mkoa mmoja unawakuta manabii/mitume zaidi ya 5+, wakati maandiko yanasema nabii akizaliwa ujue nabii aliyekuwa akihudumu eneo hilo hana kitambo kirefu. Na nabii siyo kama machungwa kila mkoa unayo🤣🤣🤣
imeandikwa kwny kitabu gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…