Ishara ya dole la kati la Zuchu ndiyo chanzo cha kupigwa mawe?

TheMaster

Member
Joined
Aug 10, 2023
Posts
36
Reaction score
68
Kwa kilichotokea mbeya, Msanii wa WCB kwajina maarufu ZUCHU kuwanyooshea mashabiki kidole cha kati kisha kuanza kurushiwa mawe na chupa za maji na baadhi ya Mashabiki walioonesha kukerwa na kitendo kile Huwenda ukawa ni mtego kwa serikali na chama cha CCM.

Hii si mara ya kwanza kwa bint huyu wa kizanzibari kufanya matusi stejini, aliwahi kufanya matusi ya uchi akiwa jukwaani zanzibar kisha kufungiwa kwa muda wa miezi 6 na faini, ila juzi tena amerudia vilevile kutukana jukwaani hadharani kabisa.

Je anafanya hivi kwa kujiamini yeye ni Mzanzibari na raisi ni Mzanzibari hivyo hakuna wa kumgusa??

Je anafanya hivi kwa kujiamini kuwa Huwenda kwasababu ni mwana CCM bhasi CCM Iitamlinda??

Akili kumkichwa BASATA, bint huyu adhabu inamstahiki kali kabisa bila kujali uzanzibari wake wala hadhi yake
 
Duh kwahy hiyo ni kabla ya kurushiwa makopo, basi wanambeya wapo sahihi. Hawa wasanii wana upuuzi mno.

Anyway, hapo Samia na chama chake wameingia vp? Au ilikuwa ni tamasha la kichama?
 
Hiyo picha emeeditiwa na machawa wa ccm ili kuficha ukweli, ni kwamba alimtaja mama Samia ndo watu wakamaind na kumtoa baruti
 
Dotto magari najua upo humu mwambie mama ,dogo anaharibu
 
alilushiwa kopo na mtu mmoja baada ya kuleta issues za 5 tena, akachukulia personal na kutaka kuanza kubishana na cloud nzima

Wakaamua kumuonesha kua hawajafamya bahati mbaya, wakarusha tena na tena, akamind akasepa.

Ukiacha hizo, WCB walifeli kuplan security ya ile stage, maana mashabiki walikua na access ya kusogelea mpaka kingo za stage, mabainsa wote wako jukwaaani badala ya kua chini kutuliza na kupanga watu.

pili, ile show ilikua bure 😃, thus means hata vichaaa, Wanywa visungura walikuepo pale, ndo walianzisha huo upuuzi, so next time lazima wafanye analysis ya matukio vzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…