Richard Robert
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 632
- 340
Maditkteta hupanda madarakani kupitia vurugu au mapinduzi au wizi wa kura. Hata hivyo wapo madikteta walioingia kwa njia halali na baadaye kugeuka na kuwa madikteta. Kwa mfano Adolf Hitler, aliteuliwa kuwa Chansela wa Ujerumani au mkuu wa serikali, na Rais Paul von Hindenburg mwaka 1933. Baada ya kifo cha Rais Hindenburg, Hitler akajitangaza kuwa “Führer” (mkuu wa serikali na state - a combination of president and chancellor).
Zifuatizo ni dalili za udikteta, ni wajibu wetu kufahamu haya kwa faida yetu na watoto wa watoto wetu:
1. Madikteta hupenda kutukuzwa na kuabudiwa kama miungu watu. Hutukuzwa kwa propaganda na wapambe wao kama mashujaa wasio na makosa, wasafi na watenda haki.
2. Chini ya madikteta waandamanaji na wapinga utawala mbovu huadhibiwa vikali, wakati mwingine huvunjwa na kuuliwa.
3. Madaraka ya kisiasa hulundukiwa kwenye kundi dogo au kwa mtu mmoja.
4. Vyombo vya habari vinadhibitiwa na kupangiwa cha kusema. Magazeti, redio na T. V. hugeuzwa kuwa vyombo vya propaganda , na muda mwingi hutumika kueneza pambio za kusifu na kumwabudu kiongozi.
5. Vitisho vinavyoratibiwa na dola, tassisi za umma zinazohusika na uhamiaji na ukusanyaji kodi na vitisho vinavyotolewa na dikteta mwenyewe kwa kinywa chake; utekati na kupotea kwa watu (forced dissappearance); mauaji (murder/ purging / political assassination), kufunga jela wakosoaji na wapinzani (mprisonment) kwa makosa ya kubumba kama uhaini, uhujumu uchumi na ugaidi; vurugu zinazofadhiliwa na dola (state-sponsored violence) na uvunjifu mwingine wa haki za binadamu zote hizi hutumika kudhibiti watu chini ya udikteta.
6. Madikteta hudhoofisha taasisi zote za utoaji haki na utawala bora na kuzigeuza kuwa taasisi za kuonea na kukandamiza watu na kulinda tabaka la watawala.
7. Madikteta huwa na wimbi kubwa la walinzi (a larger number of security personnel) ambayo haiendani na hadhi ya nchi husika (which is disproportionate to the country’s status.). Uimarishaji wa ulinzi hutokana na hofu ya kupinduliwa au kuuawa inayoanza kuongezeka baada ya kuendesha serikali kikatili na kuudhi watu wengi.
8. Raia hawaruhusiwi kudhibiti viongozi wanapotomia mamlaka vibaya; Malalamiko yoyote ya raia wema dhidi ya dikteta au wapambe wake hulaaniwa vikali na kuhusishwa na usaliti wenye ufadhili wa watu wenye nia mbaya na nchi.
9. Madikteta hutumia wingi wa wapelelezi wa siri kupeleleza raia (secret intelligence services to spy on the citizens) na kudhibiti mwasiliano binafsi (monitor private communication). Pesa nyingi hutumika kupeleleza raia na kutengeneza wahalifu wa ndani.
10. Madikteta huwekeza sana jeshini. Jeshi huwa namba moja (military is usually a top focus for dictators) na mara nyingi huweka bajeti kubwa kwenye ulinzi kuliko huduma za jamii (they often prioritise defence spending over social services.). Madikteta hutumia fedha nyingi jeshini ili kuzuia uasi dhidi yake.
11. Madikteta hawateui wasaidizi mahiri kuwa kwenye nafasi ya pili kwenye mamlaka; hupendelea kuwa na wasaidizi wenye ushawishi na uwezo mdogo (they prefer figurehead deputies) ili wawe watu wa kufuata maagizo.
12. Madikteta hukusanya fedha kwa wingi na kuwekeza kwenye kulinda madaraka. Hivyo hata ofisi zinazokagua fedha za serikali hudhibitiwa.
13. Hakuna uchaguzi huru na wa haki chini ya madikteta. Wakiruhusu uchaguzi , hudhibiti matokeo kwa kuruhusu watu kupiga kura apendavyo dikteta.
Mwisho wa maditeta waliowengi ni mbaya. wengine huishia kwenye vurugu kama walivyoingia au kuendesha nchi kama ilivyotokea kwa Adolf Hitler wa Ujerumani, Benito Mussolini wa Italia, Saddam Hussein wa Iraq na wengine wengi waliokufa vibaya.