Ishi ndoto yako

Ishi ndoto yako

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2013
Posts
735
Reaction score
1,467
Kuna wakati kwenye maisha unaweza kuona kama vile kuna watu ambao wana uwezo MDOGO kuliko wewe ila wamepewa NAFASI kubwa unayostahili wewe. Ukijipima kimoyomoyo unasema “yaani hata sielewi kwa nini watu hawanioni”.

Unaanza kujifikiria-Mbona mimi nina KIPAJI kikubwa kuliko chake ila yeye anapewa nafasi kila siku mimi hawanioni? Mbona kila siku anapewa yeye nafasi na kusemwa vizuri ila kazi yangu hakuna anayeiona? Mbona akifanya kitu kilekile ambacho mimi huwa nakifanya yeye anaonekana genius wakati mimi nikifanya kinaonekana cha kawaida. Mbona nafanya kwa BIDII kuliko wao ila HESHIMA kila siku inaenda kwao?

Nimejifunza kwenye maisha kuna kitu kinaitwa “The Law of Timing”. Hii inahusisha wakati wako SAHIHI wa KUDHIHIRISHWA. Ukifanya na watu hawasemi, hawasifii au hawakutambui haimaanishi HAWAONI na wala haimaanishi UNAPOTEZA MUDA. Usiache, endelea. Ukilazimisha kuonekana kabla ya muda wako utapotea kabla ya muda wako, ”Trust the Process”.

Kila mtu ana wakati wa KUDHIHIRISHWA kwake. Huo wakati ukifika hata wewe utashangaa jinsi kila unachofanya kinavyoleta matokeo makubwa. Usipime siku kwa MAVUNO ya kila SIKU bali ipime kwa MBEGU unazokuza kila siku. USIACHE kumwagilia kwa HASIRA za kuona mbegu HAIOTI. Muda wako UNAKUJA!


#Nanauka
 
Hapo pa kumwagilia mbegu kwa hasira ata kama haioti usipaamin sana utapoteza maji mengi kumbe mbegu ndio inazidi kuoza..dawa ni kupata mbegu itakayochipua bila gharama na kuukuza mche kwa gharama maana tiari tumaini lipo!
 
Its true,inatakiwa tumsikilize Mungu,yeye ndio anaejuwa ni wakati gani unafaa kuachilia baraka zako,God's timing is the best ever...
 
Hii inaitwa unapaswa kutumia ujasusi wa kiuchumi pia katika harakati za kutimiza ndoto zetu
Hapo pa kumwagilia mbegu kwa hasira ata kama haioti usipaamin sana utapoteza maji mengi kumbe mbegu ndio inazidi kuoza..dawa ni kupata mbegu itakayochipua bila gharama na kuukuza mche kwa gharama maana tiari tumaini lipo!
 
Back
Top Bottom