Ishi vizuri na familia yako hasa watoto wako. Punguza au acha kabisa utemi, ubabe na udikteta

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
MHADHARA (88)✍️
Ishi vizuri na familia yako hasa watoto wako. Punguza au acha kabisa utemi, ubabe, udikteta, ukatili, na ukali usio na maana kwa watoto wako.

Kama umefikia hatua ambayo ukiwa mbali na familia yako watoto wanashangilia huku wanatamani usirudi milele, ndugu yangu badili mtindo (mfumo) wako wa kuishi na watoto.

Tafuta maisha lakini hakikisha unapata muda wa kukaa na familia yako. Ukiwa nyumbani na watoto jipe muda wa kuwasikiliza. Mtoto anapokuita "baba-baba-baba" wewe itika na uonyeshe kwamba uko tayari kumsikiliza, huenda ana taarifa au jambo jema la kukueleza.

Baba mwema ni yule ambaye akisafiri au akiwa mbali na nyumbani kwake watoto wanamkumbuka baba yao. Kama utawajengea watoto mazingira mazuri ya ukaribu na urafiki, ukisafiri watoto kila mara watamuuliza mama yao "baba atarudi lini".

RIGHT MARKER
Dar es salaam.
 
Aisee Umenena vyema sana!Eti mkisikia harufu ya fegi mnazama vyumbani,kikoozi vyumbani,kishindo vyumbani duuh huo sio ubaba Bora!
 
Fact brow 👍😅😅
 
Baba ukiwa hucheki na wowote na watoto wako wakikua huwa hawacheki na wowote
 

Maua yako mkuu.
💐💐💐💐
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…