Ishu siyo mshahara, ishu ni plan

Super Brain

Member
Joined
Apr 17, 2016
Posts
45
Reaction score
38
Watu wengi wamekuwa wakiwa na hamu kubwa ya kupata kazi, mara wapatapo kazi wamekuwa wakibweteka na kuishia kuwa na mawazo madogo ama plan ndogo yaani ya kuwa tu na nyumba na gari.

Yaani wengi hatuna project za muda mrefu. Unamkuta mtu anaishi maeneo kama Iringa sehemu ambayo unaweza ukatumia pesa ndogo kuwekeza katika kilimo cha miti baada ya muda mfupi wa miaka minne au mitano ukapata mamilioni ya shilingi yeye hudharau na kusema miaka yote hiyo ya kazi gani? Mi kwanza nina kazi yangu.

Baada ya miaka minne hadi nane yule aliyepanda miti unamkuta yuko mbali na ameanzisha miradi mikubwa na nymba na kila kitu yeye anaishi maisha yaleyale.

Mtu anakopa milioni kumi na tano na kwenda kujenga kanyumba fulani na kujisifu nina akili wakati wenzake ile pesa wanagawa nusu yake na kuanzisha mradi na kuusimamia vilivyo na kujikuta akipata faida kila siku mwisho wa siku hupelekea kujenga bonge ya mjengo na mradi unaendelea na kuendelea kuwekeza wakati yule aliyekopa na kujenga nyumba yupo palepale.

Woga ndiyo kitu kinachowakandamiza, wanaogopa kupata hasara mwisho wa siku wanaishia kuishi maisha yaleyale.Huwaza nikianzisha biashara nitaanguka,huogopa risk.

Kwa mawazo kama haya hata ulipwe milioni ngapi utaishia kuwa mtumwa huku ukilalamika mshahara hautoshi lakini kama unapata vijisend vyako akili yako ukawaza positive na ukafanyia wazo lako utakuja kuwa na pesa ndefu mwisho wa siku na kuachana na utumwa wa kuburuzwa na kuishi bila hofu.
 

Mkuu umeongea vitu vya msingi sana. Naomba na mimi nitoe maoni yangu, naomba ieleweke kwamba sio kila mmoja wetu ni mzuri kwenye biashara, kuna mtu ukimpa milioni 5 leo ukija baada ya miaka miwili utamkuta amepiga hatua sana. Na biashara licha ya faida zake lakini zinachangamoto zake pia, sio kila biashara itakulipa kama ulivyotarajia, kuna wakati utapiga hasara iliyoenda shule na kuna wakati utafanya vizuri sana, hivyo basi wengine huona afadhali wawekeze kwenye kujipatia kibanda cha kujibanza ili pesa yao isipotee bure.

Mwisho kabisa, kwangu huwa naamini kabisa kwamba nidhamu ya pesa ndio inatofautisha wanaofanikiwa na wasiofanikiwa, namaanisha sio unapata kiasi gani ila unatumiaje kile unachokipata? Elimu ya uwekezaji na ujasiriamali bado inahitajika sana . Ahsante kwa hili darasa kwa kuwa nalo linachangia kuamsha akili za wengi wetu tulioajiriwa kuondokana na ile kasumba kwamba ukiajiriwa utaishi kwa mshahara tu. Ajira tuzitumie tu kama dhamana kwa ajili ya kuaminika kupata vyanzo vya pesa na kufanya miradi mingine.

Shukrani
 
A shilling today worth more than a shilling tommorrow
 
Asante sana
Ujumbe mzur sana kwa maendeleo yetu
 


"Woga ndiyo kitu kinachowakandamiza, wanaogopa kupata hasara mwisho wa siku wanaishia kuishi maisha yaleyale"
Hapa umenena, woga wako ndio umasikini wako na huwezi jua bahati yako bila kubahatisha.
 
Da,nimewekezawekeza mzee ila sipendi kuorodhesha ase!Sijaponda nimetoa elimu,si lazima uchukue nisikulazimishe kama umependa chukua idea,..
 
duuu kweli nimeshuhudia jinsi wastaafu wanavyopata tabu
 
Umetoa wazo nzuri sana halafu kingine ni kutokata tamaa maana unaweza kuanzisha project ukapata hasara hapo ndio tatizo. ..ikumbukwa pia waliofanikiwa walifeli mara nyingi mpaka kuna point mambo yakawa poa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…