Super Brain
Member
- Apr 17, 2016
- 45
- 38
Watu wengi wamekuwa wakiwa na hamu kubwa ya kupata kazi, mara wapatapo kazi wamekuwa wakibweteka na kuishia kuwa na mawazo madogo ama plan ndogo yaani ya kuwa tu na nyumba na gari.
Yaani wengi hatuna project za muda mrefu. Unamkuta mtu anaishi maeneo kama Iringa sehemu ambayo unaweza ukatumia pesa ndogo kuwekeza katika kilimo cha miti baada ya muda mfupi wa miaka minne au mitano ukapata mamilioni ya shilingi yeye hudharau na kusema miaka yote hiyo ya kazi gani? Mi kwanza nina kazi yangu.
Baada ya miaka minne hadi nane yule aliyepanda miti unamkuta yuko mbali na ameanzisha miradi mikubwa na nymba na kila kitu yeye anaishi maisha yaleyale.
Mtu anakopa milioni kumi na tano na kwenda kujenga kanyumba fulani na kujisifu nina akili wakati wenzake ile pesa wanagawa nusu yake na kuanzisha mradi na kuusimamia vilivyo na kujikuta akipata faida kila siku mwisho wa siku hupelekea kujenga bonge ya mjengo na mradi unaendelea na kuendelea kuwekeza wakati yule aliyekopa na kujenga nyumba yupo palepale.
Woga ndiyo kitu kinachowakandamiza, wanaogopa kupata hasara mwisho wa siku wanaishia kuishi maisha yaleyale.Huwaza nikianzisha biashara nitaanguka,huogopa risk.
Kwa mawazo kama haya hata ulipwe milioni ngapi utaishia kuwa mtumwa huku ukilalamika mshahara hautoshi lakini kama unapata vijisend vyako akili yako ukawaza positive na ukafanyia wazo lako utakuja kuwa na pesa ndefu mwisho wa siku na kuachana na utumwa wa kuburuzwa na kuishi bila hofu.