DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Bara, Isihaka Mchinjita, ameikosoa vikali Serikali kwa kushindwa kushughulikia tatizo la ajira kwa walimu pamoja na uhaba mkubwa wa walimu mashuleni.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Julai 11, 2025, katika Jimbo la Pangani, Mkoa wa Tanga, Mchinjita amesema kuwa licha ya Serikali kukiri kuwa kuna upungufu wa walimu 268,000 katika shule za msingi na sekondari, ni walimu 14,000 pekee waliopata ajira tangu mwanzo wa mwaka huu.
Aidha, Mchinjita aligusia hali ngumu inayowakumba wahitimu wa taaluma ya afya, akibainisha kuwa idadi kubwa ya vijana wanaomaliza masomo yao bado hawajapata ajira, huku vituo vya afya na zahanati—hasa vijijini—vikikabiliwa na uhaba mkubwa wa watoa huduma.
Katika hitimisho la hotuba yake, Mchinjita alitoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kuiondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani katika uchaguzi ujao, akisema chama hicho kimeshindwa kusimamia maslahi ya wananchi na kuleta maendeleo ya kweli kwa vizazi vya sasa na vijavyo.