Isingekuwa mfuko wa bima ya afya (NHIF) ningefanya nini?

POLE sana mkuu kwa kufiwa na Maza,,Mungu awafanyie wepesi..

Lakini hili kuna namna limekaa kama T A N G A Z O hivi... hebu liweke vizuri halijapendeza
 
Bima inasaidia sana. Dada yangu NHIF walimlipia matibabu zaidi ya Milioni 170.
 
Kwako mtumishi wa umma ni furaha vipi kwa mwananchi wa kawaida sasa hizo gharama unafikiri anapambana nazo vipi maana yeye kujiunga ni mtihani package ni ghali sana
 
Pia sahivi kuna maboresho mengi kwenye hizi bima kuna walaka umetolewa juzi juzi kuna dawa nyingi zimeingia ni kazi nzuri ya Ummy Ally mwalimu waziri wetu wa afya
Achana juma na rozi, viatu vilikuwa vikubwa kwake
 
Bima ililetwa kwa lengo hilo hapo.
Kwa hio usishangae

Watu wanaangalie mbele ili kusaidia watu kama wewe
 
Ndio boss. Mwaka wa 6 huu tangu atibiwe. Anaendelea na mishe zake kama kawaida.
Ni habari njema. Maana case za kansa ninaowasikia hufariki wakiendelea na matibabu ikaanza kunifanya ni matibabu ya kansa ni kutimiza tu wajibu
 
Ni habari njema. Maana case za kansa ninaowasikia hufariki wakiendelea na matibabu ikaanza kunifanya ni matibabu ya kansa ni kutimiza tu wajibu
Ni kweli mkuu. Wapo wengi wanapona ila story yao haisikiki sana kama mtu akifariki. Nimekutana na watu wana maiaka zaidi ya 15 tangu wapone
 
Ni kweli mkuu. Wapo wengi wanapona ila story yao haisikiki sana kama mtu akifariki. Nimekutana na watu wana maiaka zaidi ya 15 tangu wapone
Serikali ningependa ufanye kampeni kama wanavyofanya kansa ya matiti. Watu wapimwe mass testing kujua kama Wana dalili za kansa au la. Watu wengi wenye kansa za aina tofauti na hiyo ya matiti hujulikana wakiwa katika hali mbaya ambapo gharama na kubwa na hata wakiziingia kupindua meza unakuwa ngumu.
 
Kwa uhakika NHIF ni moja ya Mashirika adimu sana hapa nchini ambayo yanatimiza wajibu wao kwa Umma kama sheria ya kuundwa kwake ilivyoainisha. Wengi wetu sasa tungekuwa upande wa pili kama huduma hii isingekuwepo. Wastaafu wengi kimbilio letu ni huko. Nawahimiza waajiri na pia waajiriwa kwamba wahakikishe wamejiunga na utaratibu huu ambao huwahakikishia matibabu wakati wanapokuwa wagonjwa. Si tu wao bali pia na familia zao na wategemezi wengine kama ilivyoanishwa katika mkataba. Hongereni sana NHIF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…