Mdondoaji,
..Karume aliwahi kunukuliwa akisema "azimio la arusha mwisho chumbe". Zanzibar haikuwahi kuwa nchi ya kijamaa kama tunavyoujua huku Tanganyika.
..wakati mnasubiri kurudishiwa pwani ya Afrika mashariki, na kuanza kuchimba mafuta, kuna mambo ambayo mnapaswa kuyarekebisha ndani ya Zanzibar ya sasa ili msonge mbele.
..kuwa na eneo kubwa na rasilimali nyingi haimaanishi kwamba moja kwa moja mtapata maendeleo. we have all those things in Tanganyika lakini hatuna maendeleo kwasababu ya uongozi na mipango mibovu.
..narejea hoja yangu kwamba Zanzibar ilianza kudhoofika kidogo kidogo toka enzi za Sultani. kile kitendo cha kunyanganywa maeneo iliyokuwa "ikimiliki" ni ushahidi tosha kwamba Zanzibar ilikuwa dola dhaifu/inayodhoofika kulinganisha na dola zilizokuwepo wakati huo.
..we can discuss jinsi gani zao la karafuu limedorora hapo Zanzibar. inawezekana kabisa price controls ikawa moja ya sababu. hilo huwezi kusingizia muungano. karume alitaifisha ardhi kabla hata hatujaungana. inawezekana pia utaifishaji ardhi uliliweka zao hilo ktk mikono ya watu wasio na ujuzi na mitaji ya kilimo chake. we saw what happened in Tanganyika when sisal production was nationalised. hii inaweza kuwa thread inayojitegemea na si vizuri kutumbukiza siasa humo.
Mohamed Shossi,
..ni kweli Karume alikuwa na nia ya kuibadilisha Zanzibar ifanane na nchi zilizoendelea.
..tatizo lake ni kwamba alianza kuwekeza ktk miradi ambayo haikuwa sustainable.
..Karume alipaswa kuwekeza ktk sekta kama za viwanda, utalii, kuimarisha kilimo etc etc. badala yake akajikita kwenye sekta zinazotumia fedha kama kujenga nyumba za wazee, kuanzisha TV kama huduma na siyo biashara, etc etc.
..sasa utaona kwamba Karume alikuwa mtumiaji mzuri wa fedha badala ya kuwa mzalishaji mzuri.
..Zanzibar ni nchi ya kwanza kuwa na TV ya rangi, hilo halina ubishi. but what happened after that, ni muhimu zaidi. ungetegemea Zanzibar ndiyo wawe wanaongoza basi kwa utaalamu wa sekta ya habari ya TV ktk eneo hili la Afrika lakini sivyo.
..mwingine anajisifia Zanzibar ndiyo nchi ya kwanza Afrika kuwa na matawi ya mabenki ya Ulaya. this is another wrong notion. hizo benki zilikuwepo hapo kuinyonya Zanzibar na siyo kitu kingine. vijana wa leo tunapaswa kujiuliza what happened to Benki ya Watu wa Zanzibar. nini kimefanyika kuhakikisha benki hiyo inajitanua maeneo mbalimbali ya Zanzibar,Tanganyika,and beyond?
Joka kuu,
Vile vile Karume alipofatwa na Nyerere mara ya kwanza alimwambia hakuna muungano baina ya zanzibar na Tanganyika ila baada ya kuona anaweza kuja kupinduliwa na Babu ndio akasema zanzibar na Tanganyika ziungane, wewe jiulize kwanini terms and condition za muungano wa Tanganyika na Zanzibar wanazifahamu Nyerere tu na Karume???
Vile sawa naweza kubaliana na wewe kuwa wazanzibari nao walichangia kwa namna fulani usocialism but the mastermind behind zanzibar revolution alikuwa Nyerere maana yeye ndio aliyekuwa akiratibu na kusimamia maandalizi yalipokuwa yakifanyika Dar. Vilevile walikuwa wakitrain vijana pindi watakaposhika madaraka waende kuongoza nchi au hilo unalibisha. Ndio maana walipoingia madarakani walikuwa na ideology kama ya Nyerere ya usocialism. Kama mwandishi huyu anavyosema:-
It has taken a full thirty years for Zanzibar to throw off the Marxist legacy of 1964 and some things will never recover: thanks to a disastrous experiment with state-owned collective farms, for example, the clove industry is virtually dead and cannot now be privatised again. But the V.I Lenin Hospital has survived (now rejuvenated and known by the politically neutral name of the Coconut Palm Infirmary), and a major restoration project is underway in Stone Town to preserve the finest of the old palaces before they crumble into the dust. Visitors to Zanzibar are now welcomed rather than restrained (as happened in the aftermath of the Revolution), and it is no longer assumed that anyone inspecting the buildings of Stone Town is necessarily doing so at the behest of the CIA. Hotels for backpackers have proliferated- parts of Stone Town are beginning to look like an African Goa- and one or two really good restaurants and hotels have also come up, notably Emerson's, the labour of love of a New York psychiatrist who came to Zanzibar four years ago, had a mid-life crisis, and decided to stay on.
(William Darlympe)
Vilevile unanyang'anyi wa eneo la pwani waliufanya wakati ambapo dola kuu duniani ilikuwa uingereza karne ya 19 na 18. Sasa nikuulize Sultani wa Zanzibar alikuwa na ubavu gani wa kupambana na Uingereza wakati ule. Ndio maana yule mwanasheria alinambia kama wakijenga kesi hawa jamaa zetu santuri itakuwa tamu Joka Kuu kwani waingereza na wajerumani walitumia ubabe kumnyang'anya Sultani wa zanzibar eneo alilokuwa akimiliki kihalali na kisheria. So hapa sio kwamba eti dola ilikuwa weak hapana ila walitumia ubabe na ubeberu kwasababu walijua bandari ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi zao. Ni kama sasa hivi ilivyo Hong Kong na China unataka kuniambia Hong Kong ni dola weak? Chechnya na Russia , Hawaii na US, na kwengineko kwingi tu. So hoja yako sio sahihi na ni weak.
Kuhusu uongozi mbovu sikatai na in fact nakuunga mkono kuwa lack of accountability na ufisadi unachangia kurudisha nyuma maendeleo but tukitazama impact yake na impact ya kumezwa na muungano nadhani hasara ni kubwa zaidi. Mfano Per capital income ya mzanzibar before muungano na miaka michache baada ya muungano ilikuwa £7,000 au $20,580 sasa hivi per capital income ya mtanzania including mzanzibari ni $720 tu! sasa nikuulize ni akina nani wameumia? Unakuta muungano una hasara zaidi kuliko hayo unayoyasema ambayo very trivial.
Vile nimekupa mfano wa banking sectors kuwapo africa mashariki zanzibar kwa maana kuwa it is a signal ya jinsi Zanzibar uchumi wake ulikuwa imara. Wewe, nikuulize swali kwanini hawakufungua branch za benki zao Tanganyika??? Vilevile, nikuulize benki za nje zinafata nini katika nchi zaidi ya kutengeneza faida?
Baadhi ya maneno mengine naweza kukubaliana na wewe mfano Karume alikuwa mtumiaji zaidi ya uzalishaji but hilo linachangiwa na kuwa jamaa alikuwa hajasoma hata darasa mmoja. alichukuliwa toka Malawi na Nyerere ili aje kuongoza nchi for the interest ya Nyerere. Hata hivyo Karume alikuwa na uzalendo na ndio maana aliweza kujenga barabara na nyumba ila alikuwa hataki ushauri wa wasomi maana alikuwa akiwahofia watampindua. Sasa hata wewe ukimweka mtu asiyejua nini unafanya unadhani who will take the blame? Nyerere na Tanganyika mkuu we have our big share of blame usikatae hilo.