Hakuna kitu kinaitwa uislamu moderate! Uislamu umesimama kutokana na qurani, hadith, na miratul rasul! Na kigezo chao chema ni muhammad kwisha. ukipenda katafakari personal profile ya muham mad ili uuelewe uislamu!
Mbona hao unaowaita moderate hawatangazi hadharani kwamba aya inayosema "fight(slay and kill) those who do not believe in allah......" haitoki kwa allah! Q9:29! mbona hawasemi; "wafanyeni wayahudi na wakristo rafiki zenu!" q5:51-52, au waseme "wayahudi si adui zenu!" Q5:82!
you may think you know what islam is all about.....!
but the black flag of islam flies over US embassy in Tunisia!
Mpendwa, mbona unaonekana vile ukijadili mambo ya Usilamu hadi kushindwa kusoma, kutoa taarifa hata kuleta uwongo mtupu.
1. Hakuna bendera nyeusi juu ya ubalozi wa Marekani mjini Tunis; wala haikuwepo. (Waandamanaji walipanda ukuta wiki iliyopita na kuonyesha bendera nyeusi huku ukutani - ambayo si "juu ya ubalozi"- kwa dakika kadhaa hadi kuondolewa na polisi ya Tunisia. Hii unaweza kujua na sasa sijui kama unaleta uwongo kwa kusudi au unaridhika na kopi-paste kwenye kurasa za takataka?
2. Unaleta ayat kutoka Quran, tuangalie matumizi yako ya Q9:29. U
naleta nusu ayat na hapa unafanya sawa kabisa kama kaka yako wa kiislamu Gavana anayependa kuleta vichekesho kwa kutaja nusu ayat za Biblia na kujenga hojo juu ya vipande hivi.
Basi jaribu kuleta ayat yote ya Q9:29 halafu utuambie hii inayoandikwa inatokea wapi? Tuone kama utalaamu wako ni zaidi kuliko kopi-paste kutoka intaneti.
3. Kwa jumla unanipa picha ya kwamba unaangalia hao wakorofi waislamu wa mwelekeo wa salafiya ya jihadi na kuamini hao ni uislamu mwenyewe.
Si vile lakini, namshukuru Mungu. Hao ni wachache; katika mazingira ya vta na udikteta wanasogea mbele; lakini ilionekana kwa dunia yote jinsi walivyo wachache katika maandamano dhidi ya baolzi za Marekani wiki iliyopita.
Mfano Benghazi, Libia: waandamanaji mia kadhaa walisimama mbele ya ofisi ndogo ya ubalozi wa Marekani, makumi wa kundi la Ansar-Sharia walikuwa na silaha na mwishowe kumwua mbalozi na walinzi wake; Tendo hili lilifatwa na maandamano wa waislamu 30,000 wa Benghazi waliofukuza Ansar-Sharia kutoka mji wa Benghazi.