Kinachochekesha hayo maagizo ya mavazi hayajaandikwa kwenye kuran, ni wivu tu na shida za wanaume wa arabia wakawalazimisha wanawake wavae hivi. Kuna story iliandikwa kuwa huko arabia bora mwanamke afiche uso na kuachia uchi
Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao na wahifadhi tupu zao, na wala wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa yale yanayodhihirika. Na waangushe khimaar (shungi) zao mpaka vifuani mwao, na wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao, au baba zao, au baba za waume wao, au wana wao wa kiume, au wana wa kiume wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kiume wa kaka zao, au wana wa kiume wa dada zao, au wanawake wao (wa Kiislamu), au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, au wafuasi wanaume wasio na matamanio ya jimai miongoni mwa wanaume au watoto ambao hawatambui kitu kuhusu sehemu za siri za wanawake. Na wala wasipige miguu yao yakajulikana yale wanayoyaficha katika mapambo yao. Na tubuni kwa Allaah nyote, enyi Waumini mpate kufaulu. [An-Nuwr: 31.]
Na Amesema:
ŁŁŲ§ Ų£ŁŁŁŁŁŁŲ§ Ų§ŁŁŁŁŲØŁŁŁŁ ŁŁŁ ŁŁŁŲ£ŁŲ²ŁŁŁŲ§Ų¬ŁŁŁ ŁŁŲØŁŁŁŲ§ŲŖŁŁŁ ŁŁŁŁŲ³ŁŲ§Ų”Ł Ų§ŁŁŁ
ŁŲ¤ŁŁ
ŁŁŁŁŁŁ ŁŁŲÆŁŁŁŁŁŁ Ų¹ŁŁŁŁŁŁŁŁŁŁ Ł
ŁŁ Ų¬ŁŁŁŲ§ŲØŁŁŲØŁŁŁŁŁŁ Ū Ų°ŁŁ°ŁŁŁŁ Ų£ŁŲÆŁŁŁŁŁ° Ų£ŁŁ ŁŁŲ¹ŁŲ±ŁŁŁŁŁ ŁŁŁŁŲ§ ŁŁŲ¤ŁŲ°ŁŁŁŁŁ Ū ŁŁŁŁŲ§ŁŁ Ų§ŁŁŁŁŁŁŁ ŲŗŁŁŁŁŲ±ŁŲ§ Ų±ŁŁŲŁŁŁ
ŁŲ§ ل٩
Ee Nabiy! Waambie wake zako, na mabinti zako, na wanawake wa Waumini wajiteremshie jilbaab zao. Hivyo kunapeleka karibu zaidi watambulikane (kwa heshima) wasiudhiwe. Na Allaah daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Al-Ahzaab: 59].