Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
BI. TITI MOHAMED ALIVYONIKUTANISHA NA ISMAILI BAYUMI
Tuwekeni kumbukumbu kwani kumbukumbu ikihifadhiwa hukumbusha.
Leo ni siku yangu ya furaha kubwa sana.
Nimekuwa nikiitafuta picha ya marehemu Ismail Bayumi kwa miaka mingi bila mafanikio.
Nataka nieleze vipi nilipata historia ya Ismaili Bayumi.
Siku moja nilikwenda kwa Bi. Titi Mohamed kwa nia ya kufanya mahojiano na yeye wakati ule nafanya utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes.
Nilimuomba Ally Sykes anifanyie miadi na Bi. Titi na akanipangia miadi nikaenda nyumbani kwa Bi. Titi Upanga.
Lile nililolifuata sikufanikiwa kwa kuwa Bi. Titi aliniambia kuwa mimi sina la kuandika kuhusu yeye ambalo bado halijaandikwa na waandishi kabla yangu.
Lakini Bi. Titi juu ya hilo alinifurahisha kwa kuniambia kuwa anawajua vyema wazee wangu.
Bi. Titi ukikaanae utakuwa unacheka na kufurahi muda wote.
Alinyanyuka pale tulipokuwa tukikaa akaenda chumbani kwake akarudi na picha akaniambia, ''Bwana Mohamed unamuona baba yako huyu?'''
Hapo alikuwa ananionyesha picha ya Ally Sykes na yeye kashika khanga anamvisha.
''Hii ilikuwa harusi ya Abraham Arusha namvisha baba yako khanga hapa atushezee ngoma namwambia, ''Sikiliza Ally leo harusi ya mtoto lazima hapa hii leo utuchezee ngoma.''
Ally Sykes akimpenda sana dada yake huyu.
Huyu Abraham ni mtoto wa Ally Sykes.
Mara kadhaa niko na Ally Sykes ghafla anaingia secretary wake Bi. Zainab kumweleza kuwa muuza samaki kaja na vikapu vya samaki kutoka ferry tena maji ya asubuhi.
Namsikia Ally Sykes anamwambia dada Zainab, ''Kikapu kimoja mwambie ampelekee Bi. Titi na kingine apeleke kwa Shariff Juneid.
Wala haulizi bei.
Turudi kwa Ismaili Bayumi.
Nadhani hii Arusha harusini ndiyo ilimrejesha Bi. Titi kwa Ismaili Bayumi.
''Bwana Mohamed funga safari uende Arusha kazungumze na Ismaili Bayumi yeye alifungua TANU Club Mombasa na mimi nilikwenda Kenya katika juhudi za kuwasaidia KANU, Mzee Kenyatta atolewe jela.''
Katika siku hizi za karibuni baada ya kusikia kuwa Bi. Titi ataadhimishwa na Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) nimekuwa katika furaha iliyochanganyika na majonzi ingawa majonzi yamekuwa zaidi kuliko furaha.
Ghafla nimejikuta namuomboleza Bi. Titi miongo miwili baada ya kifo chake.
Kinachoniliza ni kuwa yuko mwanae kila akifurahi atanifungulia ukurasa katika shajara yake aliyokuwa akiandika mazungumzo yake na shoga yake huyu.
Huyu shoga yake hakika ni mtaalamu katika uandishi ananiletea mazungumzo yake na Bi. Titi kaandika ''verbatim,'' yaani neno kwa neno kama mazungumzo yalivyokwenda.
Mimi nikisoma namsikia Bi. TIti anazungumza kwa ile namna yake ya fasaha na maskhara yake.
Shoga yake kamuuliza swali Bi. Titi.
Bi. Titi anajifanya kama vile hakulipenda swali lile anamtaja shoga yake huyu mwanae kwa jina lake ambalo yeye analipenda kumwita mwanae huyu, hapa shoga anajua hizo ni ''gymnastics'' mikwara ya bibi yake kama alivyopenda kumwita ''...ehe umekuja hapa kwa kadha au kadha wa kadha?''
Bi. Titi huyo anarejesha makombora.
Vicheko.
Miaka mingi imepita lakini hadi leo namsikia Bi. Titi akinambia, ''Bwana Mohamed kazungumze na Ismaili yeye atakueleza mipango yao na Tom Mboya hadi TANU tukabisha hodi Kenya kumtoa Kenyatta kifungoni.''
Leo mimi kupata picha ya Ismaili Bayumi sababu yake ni yeye Bi. Titi.
Niliandika makala ya Bi. Titi na kueleza mchango wake katika kumtoa Jomo Kenyatta kifungoni nilieleza katika makala ile kuwa Bi. Titi ndiye aliyenitajia jina la Ismaili Bayumi na TANU Club Mombasa kwa mara ya kwanza.
Binti yake Ismaili Bayumi baada ya kusoma makala ile inayomhusu baba yake katika kupigania uhuru wa Tanganyika ingawa alikuwa nje ya mipaka ya Tanganyika alitokwa na machozi.
Huyu binti ndiyo huyo aliyebebwa na baba yake katika hiyo picha na ndiye aliyeniletea picha hiyo.
Picha hii ilipigwa Nairobi.
Namshukuru mwisho wa shukurani.
Kaifanyia historia ya uhuru wa Tanganyika hisani kubwa sana.
Hawa wazalendo wote watatu, Ismaili Bayumi, Titi Mohamed na Ally Sykes katika picha hii wote wametangulia mbele ya haki.
Wazalendo hawa wameacha nyuma kumbukumbu nzuri na kumbukumbu hukumbusha.
Picha ya kwanza ni Ismail Bayumi na bint yake.
Picha ya pili Bi. Titi Mohamed na picha ya tatu ni Mwandishi na Ally Sykes wakiwa Muthaiga Country Club Nairobi mwaka wa 1989.