Israel ilipovunja makubaliano na Hamas wakazuia mateka

Israel ilipovunja makubaliano na Hamas wakazuia mateka

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Kwa kweli Israel wamebanwa sana katika hii vita.JWanapigana na mtu ambaye anawafahamu sana hasa katika suala la kuvunja makubaliano na kutotekeleza maazimio.Kwa kujua hilo Hamas wamekuwa wakiendesha vita vyao kwa vipimo madhubuti sana.

Katika siku ya pili ya utekelezwaji wa makubaliano ya kusitisha vita kwa siku nne tayari Israel imeshavunja makubaliano hayo na kuwafanya Hamas wazuie kwa muda kuwatoa mateka 13 Israel mpaka walipopata uhakikisho kutoka kwa wasimamizi wa makubaliano hayo ambao ni Qattar na Misri.

Mambo ambayo Israel wameyavunja kwa mujibu wa msema wa Hamas ni

- Kutoachia idadi ya malori 70 kuingia kaskazini ya Gaza kati ya 200 ya siku ya mwanzo na kupeleka malori 3 tu.

- Israel kuwafanyia fujo na hata kuuwa wapalestina 3 waliotaka kurudi majumbani kwao kaskazini ya Gaza

- Kuendelea kurusha droni hewani za kuwapepeleza wapalestina na harakati zao katika siku hizo nne za usitishwaji vita.
 
Majumbani
Wengi tu wamesharudi na ilikuwa ni moja ya masharti ya makubaliano ambalo Israel amejaribu kulivunja.Pamoja na hivyo watu wamefika na hawataki kurudi tena kusini kusikokuwa na huduma.Wamesema ni afadhali wafe kaskazini kuliko kufa kusini ya Gaza
 
Hujaelewa, anamaanisha majumba yepi unayoyaongelea?
 
Back
Top Bottom