Jackwillpower
JF-Expert Member
- Oct 4, 2017
- 2,467
- 3,687
Israeli imefanya la kustajaabisha huko Syria
Imeshambulia ngome (bezi) za Syria kwa 80% kwa mashambulizi 250 ambayo yameharibu meli, ndege, vifaru na maghala yote ya makombora na silaha zilizokuwa zinatumiwa na Assad, Hezbollah na Iran kwa kile ilichokiita kuzuia silaha hizo zisiangukie mikononi mwa magaidi dhidi yake
Hadi muda huu jeshi la Israeli limeikalia ngome kuu ya jeshi ya Syria huko Damascus baada ya kuitwaa mnano juzi
Kuanzia tarehe 8/12/24 baada ya utawala wa Assad kuangushwa na waasi wa HTS na FSA, Israeli kwa haraka ilinyakua Golan buffer zone. Na zaidi ya hapo wakasonga mbele na kutwaa eneo kubwa la mpakani kati ya Syria na Lebanoni ambalo lina mlima Hermon ambao umetajwa sana kwenye Biblia kama mlima wa baraka.
Buffer zone ni nini
"Ni eneo lisiloegemea upande wowote linalotumika kutenganisha majeshi au mataifa hasimu". Eneo hili lakutwaa buffer zone lina ukubwa wa Sqk 1,150, sasa limeingizwa ndani ya Israeli.
Sababu ya kutwaa maeneo haya
Moja, ni kukata uhusiano wa kijiographia kati ya Syria na Lebanon ili kuzuia upenyeshaji wa makombora toka Iran kupitia Syria kwenda Lebanon kwajili ya Hezbollah.
Pili, Wayahudi wanadai eneo hilo wana uhalali nalo kihistoria. Ingawa hawajaweka wazi dai hilo kisiasa lakini ndio moja ya sababu kuu ya kulitwaa. Katika Biblia, Musa na Joshua waliwapa eneo hilo nusa ya kabila Manase baada ya kulitwaa kwa vita kutoka kwa wenyeji. Kumb 3:8-14, Yoshua 12, 13. Israeli muda mrefu walihitaji kulitwaa eneo hilo ili wapanue mipaka yao kwajili ya kuunda Israeli kuu. Juzi katika net yao nilikuwa nasoma comments za Wayahudi nikaona wote wanaunga mkono kwamba huu ndio wakati sahihi wa kuyachukua maeneo hayo toka Syria na kunywa mafuta ya mizeituni inayotoka huko. Zingatia Wayahudi wanataka kuunda dola la Kiyahudi likiwa na mipaka ile ya kibiblia ambalo mipaka yake inaanzia mto wa Misri (kusini) hadi mto Flat (Iraq) likiichukua Lebanon yote na sehemu ya Syria.
Na kwa upande wa magharibi linatwaa sehemu ya ng'ambo ya mto Yordan, sasa ni nchi ya Yordan. Ramani hii mpya haina taifa la Palestina, na sasa wameshanyang'anywa nusu ya Gaza. Pia Netanyahu aliapa kupanua mipaka ya Israeli na bila kificho alienda UN na ramani mpya ya mashariki ya kati. Zaidi ukitaka kujua siri iliyo nyuma ya jambo hili, tafuta kitabu changu cha SIRI YA UASI KUTOKA MTO HIDEKELI (part 1 hadi 3), utapata mengi ya kushangaza juu ya harakati hii ya Netanyahu na walio nyuma yake.
Mashambulizi ya bezi za Iran
Kuanzia tarahe 8 ndege za Israeli za F35 na F16 zilikuwa zinaruka katika anga la Syria na kushusha makombora yaliyolenga bezi za 21 za Syria ambazo zilikuwa zimesheheni makombora kutoka Iran na Urusi. Bezi hizi zilitumika kuwafunza wanamgambo wa Hezbollah na Hamas dhidi ya Israeli. Bezi hizo zimeharibiwa vibaya sana. Na hadi leo hivi mashambulizi yakiendelea. Israeli imesema itaendelea kuharibu kila kipengele chochote dhidi ya usalama wake.
Waasi wa HTS na SFA wamepokeaje mashambulizi haya?
Waasi wameunga mkono mashambulizi ya Israeli kwenye ngome za Syria. Na wameweka bayana kwamba adui yao sio Marekani wala Israeli tena bali ni Iran na Hezbollah. Hivyo wapo tayari kuanza vita na Hezbollah na Iran pia. Hapa ndio utajua kuwa mpango wa mapinduzi umetengenezwa na CIA na Mossad na MI6 na Waarabu. Na hili ni onesho la baadae la anguko la Hezbollah iliyodhoofika na kisha Iran.
Marekani anasemaje?
Marekani imeunga mkono mapinduzi ingawa bado inaliweka kundi la HTS katika orodha ya magaidi lakini ikiunga mkono SFA. Lakini wamesema wapo tayari kuubadilisha msimamo wao juu ya HTS na kuunga mkono serikali mpya endapo itajitakasa na kuahidi kufanya kazi kwa misingi ya kidomokrasia. Israeli wao wameunga mkono. Pia Marekani imesema haitaliondoa jeshi lake Syria hadi pale itakapolotokomeza kabisa kundi la kigaidi la ISIL.
Nchi za Kiarabu zinasemaje?
Wao wameunga mkono mapinduzi lakini wamekemea mashambulizi ya Israeli na unyakuaji wa ardhi ya Syria. Wao wamesema wapo tayari kufanya kazi na serikali mpya ya Syria.
Urusi inasemaje?
Urusi nayo imekubali kuipokea serikali mpya na wapo kwenye mazungumzo kama bezi zake ziendelee kubakia Syria au la. Ila toka juzi Urusi imeondoa mitambo yake yote ya S400 katika bezi zake mbili zilizo pwani ya Syria. Hadi sasa haijulikani hatima yake, lakini ndio hivyo Putin hana usemi tena ndani ya Syria.
Chini ni ramani inayoonesha mashambulizi ya kushangaza ya Israeli ndani ya Syria.
Na Jeff