Israel imepokea ndege za kijeshi kutoka USA

Israel imepokea ndege za kijeshi kutoka USA

Israel imekalia ardhi ya watu.kimabavu na kwakushirikiana na Marekani wanaeneza propoganda zao kua wana mkono wa Mungu na cjui huyo Mungu ni wa aina gani.
 
Israel imekalia ardhi ya watu.kimabavu na kwakushirikiana na Marekani wanaeneza propoganda zao kua wana mkono wa Mungu na cjui huyo Mungu ni wa aina gani.
Hakuna cha mabavu hapo mkuu bali hiyo nchi walipewa na Mungu kwa lile agano kati ya Mungu na Ibrahim; hata kuichukua tu kwenyewe Joshua alipambana na hao hao wafilisti pamoja na wakanaani. Hii vita siyo ya leo bali ni maelfu ya miaka na siku zote Isarael ndo watakaoshinda tu, si iran, saudia, uturuki, iraq, jordan na nyingine a ulimwengu wa kiislam zitaweza kuishinda Israel, hata wakiiazima urusi na cjina hamna kitu, angalia hapa Isaya sura yote ya 54 na sura yote ya 60.

Tatizo watu wakiambiwa kuwa yote yaliyosemwa kwenye Biblia ni lazima yatimie bila kuangalia nani anapata na nani anakosa lakini walio upande wa Mungu wa Israel ndo watakaoshinda.
 
Who cares Mimi ni Mlokole lakini utakatifu wa mwanadamu uko moyoni sio kwenye majengo au Ardhi. Hii tabia ya kumwaga damu kupigania Ardhi na Majengo ni upuuzi na ushetani. Hakuna sababu yoyote ya Irael kufanya Uchokozi wa kuvunja Msikiti kwa sababu ya historia ya Sulemani aliyeishi miaka karibu 4000 iliyopita.
Kama ni hivyo basi South Africa ichukue kuanzia Capetown mpaka ziwa Nyassa maana ilikuwa himaya Takatifu ya Mfalme Shaka.
Wewe utakuwa mlokole ubwabwa bila shaka.
Heri ungekaa kimya kuficha ujinga wako.
 
Tofauti yako na Mimi wewe Ni Religious Fanatic, Mimi ni Mfuasi wa Kweli wa Kristo ambaye alikuja Kuiokoa Dunia yote. Lakini siasa ya Dunia hii inakudanganya kuwa Wapo wanadamu wanaostahili zaidi Kwa kupendwa zaidi na Mungu. Lakini sijui kama ulishasoma Biblia na Kuona Yesu alisema nini Kwa Lile Tawi la mzabibu lililomkataa! Tunachojazwa Leo ni Siasa za Waliojawa na Kiu za Damu za wengine. Yesu hana Kabila pendeleo, Wote watakaompokea Atawapa Uwezo Kuwa wana, Ennendeni Ulimwenguni Kote mkawafanye watu Kuwa Wanafunzi wangu, watakaomkubali mwana wanao uzima na watakaomkataa mwana hukumu ya Milele. Je ni Kinanani walimkataa na Kumuuwa Yesu na Wanamkataa hata leo? Je ni Kina nani Wanamkataa Yesu kuwa Mwana wa Mungu? Wote Lao Moja!
Kwa hiyo wewe na Mungu nani mkweli?? Mungu aliwaambia Israeli watu hawa(hao unaowatetea wewe) watakuwa MWIBA kwa Israeli kwa kuwa tu walishindwa kuwaangamiza pale Mungu alipokuwa amewaamuru kufanya hivyo. Hii INA maana kwamba hayo yanayoendelea Mashariki ya Kati yataendelea mpaka atakaporudi Kristo kuweka utawala wake wa ile miaka 1000, sasa sijakuelewa wewe msisimko wako ume-base wapi. Yamkini, ungesema unaombea Mungu yanapotokea mapigano au mashambulizi yasiwe na athari sana kwa jamii ya wanadamu ila kujifanya mlokole extreme wa kupingana hata na Yale waliyotabiriwa watu hawa naona unapoteza muda tu, na sijui hakika kama umefuatilia sana habari za nyakati za mwisho has a mambo ya dhiki kuu ambapo vita in miongoni mwa mambo ya nyakati za mwisho.
Na sidhani kama kuna MTU anafurahia umwagikaji damu anayemcha Bwana.
 
Watanganyika sijuh mna matatizo gani yani kila inapozungumziwa israel tayali mnakwenda kwenye udini hata yakiwa mambo ambayo uhitaji uwepo wa roho mtakatifu unaitaji akili ndogo tu tena yenye uwezo wa 2G bado mtu anaingiza udini na bahati mbaya ndani ya israel ni
76.1% jewish
16.2%muslim
2.1%christian
1.6% druze hawa ni kma waislam tu
4%wapagani
so wapagani ni wengi kuliko chrstian
hapa tujadili hoja si kuleta vifungu vya maandiko ambayo wakat wingine sioni kama vinafaa mada ni mambo ya kijeshi si kidini sasa vifungu vya maandiko vya nini????
israel ndio nchi inayopokea misaada mingi kutoka US na kwa mwaka US inatoa 4.4 billion usd kwa jeshi la israel na hii kampuni ya Lockheed Martin watengenezaji wa hyo ndege ya F -35 na nyingne ya Lockheed Martin F-35 Lightning II ambayo ni 5th Generation fighter inauwezo wa kutumika kwenye vitego viwili vya jeshi yani Navy and Air Force fighter ndege hii ilikuwa ni Joint Strike kati ya lookheed martin na Boeing kumbuka Boeing wana kitengo cha Boeing Defense, Space & Security na wamesha tengeneza ndege na vifaa vyiing vya kijeshi kama
Boeing B-54 na B -52
Boeing XB-55
Boeing XB-56
Boeing XB-59 na Boeing X-32 ambayo ndo zilitengezwa pamoja na Lockheed Martin F - 35 Lightning II ambayo ilishinda ktk hyo joint strike
Bora umenitoa tongo tongo sasa hawa wakristo wanatoka povu la nn kumbe hata uislam ndan ya izlael upo kuliko ukristo
 
hivi mkuu unafikiri kuna DNA ya kiyahudi?
Nijuavyo DNA Ya muisrael asilia ukiilinganisha na ya mpalestina asilia ni kitu kinaendana ,
wayahudi waliathiriwa sana na uvamizi wa waasyria walioporomosha utawala wao,na walipokua uhamishoni walijenga umoja wakijitenga bila kuingiliana na jamii za huko,wakiwa na mawazo ya kurudi palestina na kuliinua taifa lao upya.
Imani hiyo ikageuka kuwa dini,wakiamini mkuna masiha atawakuja kuwatoa katika mateso na kuirudisha israel itawale dunia,
wao dunia hawakumaanisha mpaka huku africa etc,
walijua maana yale ya caanan na kandokandoni ndio dunia.
Iman ilikuwa naikazaliwa dini ya kiyahudi ikiwa imebase katika utaifa.
Sasa hao european jews ndo walikuja kuanza kupata wazo la kuitawala dunia yote kwa maana hasa ya dunia nzima,
na hapo ndo matatizo yalipoanzia.
Kamsome albert pike utaona nachomaanisha
mkuu, ipo DNA ya myahudi. na kuna kiwango chake ambacho kinatofautiana sana na ile ya mwarabu. na ukitaja uarabu, jua wameingiliana sana, watu wa iran, watu wa iraq, pakistan, syria, lebanon, turkey, sio waarabu. waarabu ni wale wa north africa, saudia, UAE, yemen. hao ndio waarabu. lakini kwasasa hao waarabu wameingiliana sana na hao waajemi na wamedi, waashuru/syria, wamesopotamia/wababilon etc. wamezaliana na DNA ikapotea. lakini ya kiyahudi kwasababu ya strick rules ya kuoana ilibaki palepale. hii wanaifanya, na waliifanya hata kwa wayahudi wa kiafrica, wale toka ethiopia. kwasasa pale Ethiopia wamebaki kama laki mbili tu, wengine wote walishanyanyuliwa kwa ndege wanaishi israel, na hawa walikuja kule baada ya malkia wa sheba kuzaa na suleiman alipomtembelea na ndipo dini ya kiyahudi ikahamia kwenye kabila hili dogo la ethiopia waliokuwa wajukuu wa suleiman. kuna historia ndefu. walipopima DNA waligundua wale wa ethiopia wanayo sawa tu na wale wa israel ambao ni wazungu. unatakiwa kuelewa kwamba wenzetu wazungu wanapima sana DNA na wanafuatilia historia ya asili yao sana. hata hao african americans leo hii ukikutana na mmoja atakuambia mimi wazazi wangu walitokea either nigeria, east africa, ghana, cameroon etc. wayahudi ndio kabisaa huwa wanapima kujiridhisha kwasababu kwao ni ufahari mkubwa sana kuwa myahudi, tena wa ukweli ambaye haigizi.
 
nikikujibu kuhusu dini yao ya kiyahudi, umeongea vitu usivyovijua. dini hii na taratibu zooote wanazofanya leo hii kwenye masinagogi ndizo walifanya hata wakati Yesu yupo duniani. ni torah ile ile wanatumia, na desturi zilezile wanatumia. kuhusu masihi, hata wakati Yesu yupo walikuwa wanaamini masihi anakuja ili kuja kuwakomboa toka kwa Warumi. na kusambaratika kwa wayahudi kulikuja baada ya Yesu kupaa mbinguni baadaye kabisa. ndio walitawanyika kabisa pamoja na kwamba kipindi hicho walikuwa na nchi yao lakini wakiwa chini ya ukoloni wa warumi, na pamoja na kuwa chini ya ukoloni bado walipewa haki ya kuchagua viongozi wao kina Herode na kufuata dini yao. utaifa wa israel haujazaliwa juzi, wala miaka 2000 iliyopita, ulikuwepo tangu enzi za Musa ndugu yangu, hao jamaa wan aumoja hivyohivyo hata walipokuwa uhamishoni wana umoja hivyohivyo huko huko uhamishoni. hata ukienda nchi zingine ukawakuta, wana umoja hivyohivyo na utaifa hivyohivyo. ukisema tumsome ALBERT PIKE unaleta utani, huyo ni mpuuzi tu, unatakiwa kusoma Biblia haya yote yapo kwenye Bible iliyokuwepo hata kabla ya huyo albert.
 
Wewe utakuwa mlokole ubwabwa bila shaka.
Heri ungekaa kimya kuficha ujinga wako.
Mimi nilichopinga ni kuwa hakuna sababu ya kuvunja Msikiti ili Israel iwe Israel. Kwani kama Mungu alikuwa hawataki hao waliujenga huo msikiti, wakati wakiujenga kwani alikuwa wapi? Wokovu wetu upo Rohoni na Katika sadaka ya Yesu Kristo. Hayo mengine ya Kuvunja misikiti, kuuwa wengine kama mbwa unayajua wewe. Naijua bibilia kuliko unavyodhani. Nimeenda Shule ya Bibilia, Nimefundisha na Kuhubiri miaka zaidinya 20. Na nimeandika Vitabu 2 vya Kikristo. Najua na Kuamini Israel kama taifa lolote linahitaji kujilinda. Nisichokubali ni kuwa ati Israel imepewa mamlaka na Mungu ya kuuwa na kumwaga damu bila hatia.
Kama unajifanya mjuaji wa Biblia Imeandikwa Wazinzi wapigwe mawe, Je tufanye hivyo leo? Kama hilo halifai, kwanini kupigania ardhi na kuuana ni sawa! Na kwanini Yesu "alivunja" amri kwa kukataa kupiga mawe? Kama kuna upumbavu ulionikuta nao mimi ni hilo la kukataa kupiga mawe, kumwaga damu za wengine kwa Kisingizio cha dini. Upumbavu huo basi Nautaka.

Any one who think that his humanity has more value than that of others, based on his religion, ethnicity, wealth, education or any social grouping, such a person is dangerous and a curse among humanity.
 
Waethiopia na Wamasai ndio wana wa Ibrahim, mpaka kufikia kwa Selemani, Je nao Tuwape Tu 21 au F35 wazitumie kupambana na Wakulima wanaochukua arthi yao Takatifu?

On a Serious Note Wamasai na Waethiopia ni Wana wa Israel halisia. Hata leo wamasai bado wanapenda kuvaa mavazi ya Rangi nyingi kama lile la Yusufu alilopewa na Baba yake Yakobo. Ila dunia imedanganyika sana na historia za uwongo, Ndio maana leo Mafarao waliokuwa Weusi ti. Tunaonyeshwa walikuwa wazungu!
 
Kwa hiyo wewe na Mungu nani mkweli?? Mungu aliwaambia Israeli watu hawa(hao unaowatetea wewe) watakuwa MWIBA kwa Israeli kwa kuwa tu walishindwa kuwaangamiza pale Mungu alipokuwa amewaamuru kufanya hivyo. Hii INA maana kwamba hayo yanayoendelea Mashariki ya Kati yataendelea mpaka atakaporudi Kristo kuweka utawala wake wa ile miaka 1000, sasa sijakuelewa wewe msisimko wako ume-base wapi. Yamkini, ungesema unaombea Mungu yanapotokea mapigano au mashambulizi yasiwe na athari sana kwa jamii ya wanadamu ila kujifanya mlokole extreme wa kupingana hata na Yale waliyotabiriwa watu hawa naona unapoteza muda tu, na sijui hakika kama umefuatilia sana habari za nyakati za mwisho has a mambo ya dhiki kuu ambapo vita in miongoni mwa mambo ya nyakati za mwisho.
Na sidhani kama kuna MTU anafurahia umwagikaji damu anayemcha Bwana.
Kama Mkristo unachotakiwa kujua ni Jambo moja, Yohana akasema Mtazame mwanakondoo wa Mungu aiondoaye dhambi ya Uliwengu! Mengine yatakuchanganya. Wenye kiu za damu za watu na Ajenda zao nao Wanatumia Maandiko. Kama mandiko ya agano la kale yana maana kwako Pia leo toa sadaka za Wanyama! Usichague fuata yote!
 
Leo bwana Donald Trump kamteua mtu mtata anaye support israel jerusalem occupation. Dah!! Kweli usiyempenda kaja na vighola.
 
mkuu, ipo DNA ya myahudi. na kuna kiwango chake ambacho kinatofautiana sana na ile ya mwarabu. na ukitaja uarabu, jua wameingiliana sana, watu wa iran, watu wa iraq, pakistan, syria, lebanon, turkey, sio waarabu. waarabu ni wale wa north africa, saudia, UAE, yemen. hao ndio waarabu. lakini kwasasa hao waarabu wameingiliana sana na hao waajemi na wamedi, waashuru/syria, wamesopotamia/wababilon etc. wamezaliana na DNA ikapotea. lakini ya kiyahudi kwasababu ya strick rules ya kuoana ilibaki palepale. hii wanaifanya, na waliifanya hata kwa wayahudi wa kiafrica, wale toka ethiopia. kwasasa pale Ethiopia wamebaki kama laki mbili tu, wengine wote walishanyanyuliwa kwa ndege wanaishi israel, na hawa walikuja kule baada ya malkia wa sheba kuzaa na suleiman alipomtembelea na ndipo dini ya kiyahudi ikahamia kwenye kabila hili dogo la ethiopia waliokuwa wajukuu wa suleiman. kuna historia ndefu. walipopima DNA waligundua wale wa ethiopia wanayo sawa tu na wale wa israel ambao ni wazungu. unatakiwa kuelewa kwamba wenzetu wazungu wanapima sana DNA na wanafuatilia historia ya asili yao sana. hata hao african americans leo hii ukikutana na mmoja atakuambia mimi wazazi wangu walitokea either nigeria, east africa, ghana, cameroon etc. wayahudi ndio kabisaa huwa wanapima kujiridhisha kwasababu kwao ni ufahari mkubwa sana kuwa myahudi, tena wa ukweli ambaye haigizi.
mimi navyofahamu DNA Haiwezi kubadirika by simply kufuata jina fulani,mfano hapa walioitwa wayahudi ni wale waliotokana na mtoto wa yakobo alieitwa yuda.
Kuna DNa ya mtu kutokana na amezaliwa na nani.
Hata wayahudi wale wa european jew,wamechanganya damu na wazungu,kwahiyo DNA haiwezi kuwa ileile ya mwanzo.
Myahudi wa ethiopia au moroco hawezi lingana DNA na myahudi wa marekani,russia ama ujerumani.
Israel iko middle east na sio europe,lakini hawa wanaojiita wayahudi,wengine ukiwaangalia ni wazungu pure.
Pia tuchukue mfano yesu alikuwa myahudi na aliongea kiaramaic.

Aramain empire ilikuwa damusca syria,na mtawala wake maarufu aliitwa Hazael(mungu kaona).
Hawa ndo waliongea kiaramac.
Ukiifuatilia pia jacob alirudi Panda aram kutafuta mke,
hawa pia asilimia kubwa waliongea kiaramic kabla empire ya assyria haijawatawala.
So utaona kuwa kwakua chimbuko la akina yakobo ni kule asyria lazima Dna zitaendana na wakazi wa kule.
Mfano mjaluo wa tarime na yule wa uganda ama kenya lazima vinasaba vitaendana
 
nikikujibu kuhusu dini yao ya kiyahudi, umeongea vitu usivyovijua. dini hii na taratibu zooote wanazofanya leo hii kwenye masinagogi ndizo walifanya hata wakati Yesu yupo duniani. ni torah ile ile wanatumia, na desturi zilezile wanatumia. kuhusu masihi, hata wakati Yesu yupo walikuwa wanaamini masihi anakuja ili kuja kuwakomboa toka kwa Warumi. na kusambaratika kwa wayahudi kulikuja baada ya Yesu kupaa mbinguni baadaye kabisa. ndio walitawanyika kabisa pamoja na kwamba kipindi hicho walikuwa na nchi yao lakini wakiwa chini ya ukoloni wa warumi, na pamoja na kuwa chini ya ukoloni bado walipewa haki ya kuchagua viongozi wao kina Herode na kufuata dini yao. utaifa wa israel haujazaliwa juzi, wala miaka 2000 iliyopita, ulikuwepo tangu enzi za Musa ndugu yangu, hao jamaa wan aumoja hivyohivyo hata walipokuwa uhamishoni wana umoja hivyohivyo huko huko uhamishoni. hata ukienda nchi zingine ukawakuta, wana umoja hivyohivyo na utaifa hivyohivyo. ukisema tumsome ALBERT PIKE unaleta utani, huyo ni mpuuzi tu, unatakiwa kusoma Biblia haya yote yapo kwenye Bible iliyokuwepo hata kabla ya huyo albert.
mimi mkuu nilikuwa naongelea story ya BC(Before Christ),kabla yesu hajazaliwa,sasa wewe unafikiri nilikuwa naongelea wakati wa yesu wakati wa utawala ya Roman.
Urudi usome upya history ya mwaka 1000BC-500BC.
Vuguvugu ya dini ya kiyahudi ilianza baada ya ufalme wa israel kuvunjika na ukabaki ufalme wa yudah,
kabla ya hapo utawala wa israel ulikuwa ukiabudu tofauti na utawala wa yudah na hapakuwa na dini inayoitwa leo Judaism
 
David and the Kingdom of Damascus
The city of Damascus is at least 4000 years old. It is recorded as being conquered by Pharaoh Tutmosis in the 15th century BC and it became the capital of anAramean kingdom from the 11th century BC.The Kingdom of Aram-Damascus resisted the Assyrians until late in the 9th century BC, and even came up against Pharaoh Shoshenk in the Jezreel Valley, conquering Israelite Dan along the way. Israelite refugees, displaced by the Arameans, resettled in the hill-country.
In contrast to its heroics and intrigues of "King David", the Bible avoids mentioning Aram's 9th century conquest of much of Israel. Dan, Hazor, Jezreel and Megiddo were among the cities destroyed.
"Around 835 and 800 BC the kingdom of Aram-Damascus controlled the upper Jordan valley and significant areas in northeastern Israel – and devastated major Israelite administrative centres in the fertile Jezreel valley as well."
–Finkelstein, Silberman,The Bible Unearthed,p202.
Curiously,King Hazael of Aram-Damascus (844-803) enjoyed a 40-year reign – just like that ascribed to the biblical 'David' (and, for that matter, also to his son 'Solomon'!). The existence of Hazael is not in doubt, whereas outside of the biblical texts, there is as yet NO historical proof of a Hebrew king named David ruling an 'empire'.Much has been made of the so-calledTel Dan Inscription recovered in 1993 (see below) but the"Davidic empire" remains a pious invention, inspired by an Arab kingdom of the same place and time.
Where Did They Get Their Ideas From?
David –Based on the King of Damascus.

whose_kingdom.jpg
.

Arab kingdom of Hazael
"Damascus reached its zenith during the reign of Hazael ... Transjordanian regions were overrun ... Hazael was able to cross Israelite territory to progress down the coastal plain to take Gath in Philistia ...
In fact,Hazael appears to have established an empire or sphere of influence not unlike that ascribed to David."
– B.S.J. Isserlin,The Israelites,p86.
Not David, But Hazael
The city ofMethegammah(Tell es-Safi/ Gath) –hometown of Goliath!–was destroyed in the9th century BC, not the 10th, and apparently after a siege.
According to archaeologists of Bar-Ilan University, the conqueror was none other than Hazael, King of Aram-Damascus !
 
Una akili sana

Who cares Mimi ni Mlokole lakini utakatifu wa mwanadamu uko moyoni sio kwenye majengo au Ardhi. Hii tabia ya kumwaga damu kupigania Ardhi na Majengo ni upuuzi na ushetani. Hakuna sababu yoyote ya Irael kufanya Uchokozi wa kuvunja Msikiti kwa sababu ya historia ya Sulemani aliyeishi miaka karibu 4000 iliyopita.
Kama ni hivyo basi South Africa ichukue kuanzia Capetown mpaka ziwa Nyassa maana ilikuwa himaya Takatifu ya Mfalme Shaka.
 
Tofauti yako na Mimi wewe Ni Religious Fanatic, Mimi ni Mfuasi wa Kweli wa Kristo ambaye alikuja Kuiokoa Dunia yote. Lakini siasa ya Dunia hii inakudanganya kuwa Wapo wanadamu wanaostahili zaidi Kwa kupendwa zaidi na Mungu. Lakini sijui kama ulishasoma Biblia na Kuona Yesu alisema nini Kwa Lile Tawi la mzabibu lililomkataa! Tunachojazwa Leo ni Siasa za Waliojawa na Kiu za Damu za wengine. Yesu hana Kabila pendeleo, Wote watakaompokea Atawapa Uwezo Kuwa wana, Ennendeni Ulimwenguni Kote mkawafanye watu Kuwa Wanafunzi wangu, watakaomkubali mwana wanao uzima na watakaomkataa mwana hukumu ya Milele. Je ni Kinanani walimkataa na Kumuuwa Yesu na Wanamkataa hata leo? Je ni Kina nani Wanamkataa Yesu kuwa Mwana wa Mungu? Wote Lao Moja!
u seem to be muslim,mbona hujaquote kifungu chochote kwny bible mkuu kusupport ukisemacho??
 
Usiunge mkono umwagaji damu, kwasababu yoyote ile. Ni dhambi.

Unaonekana hata hujui historia ya Israel na ya mashariki kati kwa ujumla; si dhani kama unauelewa unabii wa Biblia juu ya Israe na siku za.mwisho; kama wewe ni mlokole basi kwahili pole sana, nenda kumuulize mchungaji wako juu ya mambo haya, muulize hekalu alilolijenga Sulemani liko wapi? na kama halipo ni nani alilibomoa tena ni lini? Je hekalu alilolikuta Yesu Kristo liko wapi? maana Biblia inasema wazi kuwa Yesu aliingia hekaluni na mafarisayo wakaanza kumuuliza maswali, je hili hekalu nani aliliboa na ni lini,
halafu tafuta kujua utofauti kati ya hekalu alilolijenga Sulemanibna lile alilolikuta Yesu. hii itakusaidia kujua nini kinaenda kutokea madhariki ya kati hasa Israel. Tafuta uhusiano wa hekalu linalotaka kujengwa na Wayahudi na ujio wa mara ya pili wa Kristo. Soma Ezekieli sura mbili hizi zote 38 na ile ya 39 kisha ujue Mungu alimwambia nini Ezekieli kuhusu Israel na siku za mwisho; tafuta kujua chanzo cha vita ya magogu na ile Arimagedoni. Basi ikiwa wewe unajaribu kuwa na huruma zidi ya wafilisti basi hiyo ni huruma yakwako wala Mungu hayumo kwenye hiyo huruma ni lazima yote yatimie yaliyoandikwa. kumbuka vita ya Israel na wafilisti ni ya tangu enzi za Joshua, Waamuzi, Samweli, Mfalme Sauli, Mfalme Daudi hadi leo hii, na mwisho wa yote hayo Israel ndiyo mshindi wa hii vita ikiongozwa na Kristo mwenyewe akiwa MFALME.

Mh! yaani uilinganishe Israel na S. Africa? nyingine ni nchi ya Agano na Ahadi tena Takatifu halafu hiyo S. Africa yako in nchi ya kawaida tu kama zilivyo nchi nyingine tu mfano
S. Sudan. Kwa miaka zaidi ys 1896 Wayahudi walisambaratishwa na Rumi mwaka 70 AD, mwaka wa 1945 baada ya WWII wakarejea sawaswa na neno la Nabii Isaya sura yote ya 54. Pole sana kwa wanaowaunga mkono wafilisti ila hawatafanikiwa hata kidogo maana mpaka mipaka yote na ardhi yote ya Israel ichukuliwe na Wayahudi kama ilivyotajwa na Mungu akimwambia Musa yaani kuanzia mto Jordan hadi milima ya goran ya Syria, hadi upande wa gaza na Yerushalayim yote bila kuigawanya ndiyo mji mkuu wa Yisrael. Hapa akina arafat, abas na wote akina yahe hawana chao.
 
Sawa Mungu ndiye ananijua. Mimi Machozi ya Mtoto wa Kiyahudi, au Kiarabu au Kiafrika, Ukiyasababisha kububujika kwa Ukatili wa aina yoyote Mungu atakuhukumu tu. Ndivyo ninavyoamini. Watoto wanaokufa Syria Leo kwa kuwa tu kuna watu hawakupenda Syria iwe na nguvu unaonaje Yesu aliyesema watoto kama hawa Ufalme wa Mungu ni wao anajisikiaje na aliyeleta mkorogano? Usihukumu usije Kuhukumiwa. Mimi ni Mtu wa haki sana!
kule israel hakuna waliokufa kwa maroketi ya hamas mkuu??
usiwe na mihemko saaana kiasi tu!
[emoji15]
 
Back
Top Bottom