Kama hayo ndo mawazo yako, basi ni yako tu wala Mungu hahusiki nimekwambia kasome Ezekiel sura 38 na 39 kisha uje hapa na hoja kamili au kamuulize Mchungaji wako kuhusu Israel na siku za mwisho, nenda kasome Daniel yale majuma sita ya Israel na lile juma la saba linalojumlisha mataifa nje na Israel. Tafuta kujua ndoto ile ya sanamu ya mfalme
Nebukadreza ambayo Danile alitoa fasri yake, linganisha wanyama wanne aliwaona Daniel, tafuta kuijua pembe yenye macho na mdomo iliyoota juu ya mnyama wa nne.
Nenda mnyama juu ya nchi na yule mwingine aliyetoka ndani ya bahari, tafuta kujua sana habari ya Babeli nawanamke aliyepanda juu ya mnyama, haya utayapa kwenye Ufunuo wa Yohana.
Nenda tena soma Injili ya Mathayo sura yote ya 25, Mariko sura yote ya 13, Luka sura yote ya 21, malizia na Wathesalonike wa pili sura yota 2. Sasa jiulize Kristo atakapikuja ayakuta mataifa yanafanya nini huko Yisrael?
Kama unachuki na Wayahudi eti kwakuwa walimuua Yesu Kristo bado tena hujajua kunanini kati ya Mungu na Wayahudi hebu rudia tena kusoma Warumi 11:12-36 uone nini Mtume Paulo anasema juu ya Israel, halafu jiulize baada ya Kristo kuimaluza vita ya Amargedonia Israel itakuwa wapi na Kanisa litakuwa wapi.
Ndugu yangu haya mambo kwa lugha yetu yanaitwa eschatology, kwa mtu yeyote ambaye hii lugha bado kwake ni shida ni vigumu mno kuweza kuyachambua maana yamesemwa na kuandikwa kipoetic na ecalyptici hasa kwenye vitabu vya Ufunuo, Daniel, Ezekiel, 2Thessalonians, Mathayo 25,
Mataifa yote yataufikia mwisho wao bali Israel itabaki pamoja na wale wamtumainio BWANA katika dunia hii ya sasa ndo watadumu milele.