Ni wale wasiojua historia na mwenendo wa siasa za kimaslahi za kimataifa vinginevyo tupo wakristu wengi tu ambao hatuiungi mkono Israel
Sawa mkuu ila ninawasiwasi kweli unausoma unabii wa Isaya 54
Evidence yako nini? biblia? na kama Mungu ni upendo kwanin awagawe watoto wake? maana palestine nao ni watu,wameumbwa kwa mfano wa Mungu. Wanastahili pia upendo na wao je waende wapi?
Swali zuri sana hili; ukisoma Biblia kitabu cha Mwanzo 12:1 utaona Mungu anazungumza na Abramu ambaye baadae alimbadirisha jina kuwa Ibrahimu maana yake ni baba wa mataifa (Abramu maaa yake ni baba wa wengi) Ibrahimu maana yake ni baba wa mataifa.
Mungu anamwambia Ibrahimu atoke kwenye nchi aliyozaliwa na kwenda kwenye ambayo haijui. Ibrahimu alifaya hivyo, na nchi yenyewe alimuonyesa ni nchi ya Canaani, kwaba vizazi vyake vya nne ndiyo vingeimiriki hiyo nchi.
Vizazi vya nne vya Ibrahimu ni watoto kumi na mbili wa Yakobo hawa ndo kabila kumibna mbili za Israel, yaani Mungu alimbadirisha Yakobo na kumwita Israeli maana yake ni mshindi.
Vizazi hivi vilikaa Misri kwa mda wa miaka 430, na wakawa wameongezeka sana na kufikia ngazi ya kuwa taifa. Musa aliwaongoza kwenda
kwenye hiyo nchi ya Ahadi maana Mungu alimtuma afanye hivyo.
Kwa miaka 40 walitembea na Musa akafa na kumwachia Joshua hiyo kazi, haikuwa rahisi kuirithi hiyo nchi kwahiyo walipigana na Wakanaan, wafilisti, wayebus, wahiti, waamaleki, waamori, wa (Moabu leo Saudi Arabia).
Ndivyo walivyo ichukua hiyo nchi, lakini watu waliowasumbua sana ni wafilisti leo wapalestina hasa upamde wa gaza. Daudi ndo mfalme pekee aliyeweza kuliunda pamoja taifa la Israel kama empire.
2Nyakati 3:1 inasema juu ya Sulemain kuanza kuijenga nyumba ya BWANA huko Yesrusalemuya mashariki katika mlima moria, hapo ndo hekalu lilijengwa 957 B.C.
ugomvi hapa ni ardhi hata hivyo hiyo iliisha, ila ugomvi mkubwa uliopo sasa dini na eneo la kuabudia. Kumbuka Wayahudi walijenga Hekalu zamani sana ambapo Mfalme Daudi ndo aliyepata wazo la kujenga nyumba ya BWANA na kuabudu humo na Mungu akaona ni vyema ila akamwambia kuwa mjenzi wa hiyo nyumba ni mwanae Sulemani.
Wakati Sauli akiwa mfalme wa Isarae makao makuu yake yalikuwa Gibeah na siyo Yerushalayimu, Daudi ndiyo aliyeuteka mji huu kutoka kwa wayebusi na kuuchagua kuwa makao makuu ya Israel maana ulikuwa katikati ya milima kwamaaba hiyo haingukuwa rahisi maadui kuufikia, wenyeji waliuita Yebusi Daudi akaubadilisha kuwa Yerushalayimu kama wao huuita kwa lugha yao sisi huku huuita Yerusalemu, huko ndo kuna mlima Moria.
Waislam walijenga msikiti wa al aqsa juu ya msingi wa Hekalu lile la pili lilojengwa na Nehemia baada ya lile la kwanzavkubomolewa na Nebukadreza mwaka 586 Yeremia 39:1
70 AD. Rumi walibomoa hekalu hili la
pili. miaka ya 567 Wakristo walijenga
kanisa juu ya misingi ya hekalu la pili. mwaka 705 waislma walilibomoa hili kanisa na kujenga ule msikiti wa ali aqsa, kisha pale lilipokuw hekalu la kwanza waislamu tena wakajenga lile jengo linaloonekana la duara juu katikati ya mji wa Yerusalemu.
Sasa Wahudi walisharudi kweye ile nchi yao ya ahadi 1945 AD, na waataka kulijenga Hekalu mahali palepale alipokuwa amelijenga Suleman tena kwa ramani na vipimo vilevile alivyotumia Sulema. Huo ndo ugomvi kati ya Isarel na ulimwengu wa kiislamu maana msikiti wa ali aqsa na lile jengo la duara (dome) yote yapo kwenye kiwanja komoja kile kile kinachohitajiwa na Wayahudi kwa ujenzi wa Hekalu la tatu, tayari wameshaanza na mipango na maandalizi ya ujenzi na ndo maana kila kukicha vita kati ya ulimwengi wa kiislamu na Israeli unaongezeka.
Ila Israeli ndiyo mshindi wa hii vita maana ni unabii unatimia siyo mapenzi au matawa ya mtu fulani, na lengo lake ni kuelekea mwisho wa hii
dunia maana baada ya hapo Yesu Kristo ataonekana mawinguni na mwaliko mkubwa wa malaika pamoja na wateule na ataimaliza vita kuu ya tatu ya dunia yaani armagedonia.