SI KWELI Israel Ina Sheria ya Kupinga Ukristo

SI KWELI Israel Ina Sheria ya Kupinga Ukristo

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Salam Great Thinkers!
Nimekuwa nikisikia kuwa Taifa la Israel limetunga Sheria ianyozuia shughuli zozote za kueneza Ukristo ktk Taifa Hilo.
Je kuna ukweli katika hili?
israel flag.jpeg
 
Tunachokijua
Israel ni nchi inayopatikana mashariki ya kati, nchi hii imeelezewa kwenye Biblia kama nchi ambayo Yesu Kristo alizaliwa, kuishi na kufanya injili huko, takribani asilimia 73.8 ya wakazi wa Israel kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2021 ni Wayahudi, asilimia 18 ni waislamu na 1.9 ni wakristo na asilimia 1.6 ni Wadruzi.

Ukristo ni imani (dini) ya watu wanaoamini katika Yesu kristo kuwa ni mwokozi wa wao na dhambi zao, mwana wa Mungu aliyezaliwa na kisha akafufuka kutoka wafu aliyetabiriwa kuja ulimwenguni katika agano la kale na habari za uwepo wake kuandikwa katika agano jipya.


uhalisia kuhusu Israel kuwa na sheria ya kupinga Ukristo

JamiiCheck imefuatilia uhalisia wa madai kuwa Israel wana sheria ya kupinga Ukristo na kubaini kuwa madai hayo si ya kweli ila kulikuwa na mapendekezo ya kuwekwa kwa sheria hiyo yaliyotolewa na baadhi ya wabunge.

Wabunge wawili wa Kiyahudi wa ultra-Orthodox wa Knesset (bunge) la Israel, Moshe Gafni na Yaakov Asher walitoa pendekezo mwaka Januari, 2023 la kuwekwa kwa sheria ambayo itatoa kifungo cha mwaka mmoja kwa watu ambao watawashawishi watu wengine kuhama kutoka kwenye dini zao za awali kwenda kwenye dini nyingine. Ambapo muswada huu ulipendekeza pia kifungo cha miaka miwili kwa mtu atakayemshawishi mtu mwenye umri chini ya miaka kumi nane kuhama dini yake.

Tovuti ya allisraelnews ilieleza kuwa msisitizo mkubwa wa viongozi hao ulikuwa ni kuwazua waumini wa dini ya kikristo na wafuasi wa Yesu kuhubiri kuwa Yesu ndiye Masihi na Mungu jambo ambalo wanahisi lingewashawishi Waisraeli kumfuata.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alieleza kuwa muswada huo hautapitishwa kuwa sheria nchini humo ambapo kupitia ukurasa wake wa X (Twitter) pia aliandika kuwa;

“Hatutaendeleza sheria yoyote kuilenga jamii ya kikristo”

Licha ya kuwa waziri mkuu wa taifa hilo aliwahakikishia na kuwatoa hofu wakristo kuwa muswada huo hautakuwa sheria bado pendekezo hilo lilikuwa likiwapa hofu wakristo nchini humo.​
Maelezo kama hayaeleweki!
Unasema sheria iliyopendekezwa inahusu marufuku ya mtu yeyote kushawishi mtu wa dini moja kuhamia dini nyingine lakini unaweka nukuu ya Benjamin Netanyahu "Hatutaendeleza sheria yoyote kuilenga jamii ya kikristo” .
Je kwani sheria iliyopendekezwa inahusu Wakristo tu?
 
Back
Top Bottom