Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 373
- 829
Masharti ya makubaliano kati ya Israel na Hamas kwa ajili ya kusitisha mapigano huko Gaza na kuachiliwa kwa mateka yanataraji kukamilika.
Hatua hiyo inakuja wakati Rais wa Marekani Joe Biden akisema makubaliano yako ukingoni kutimia, na kwamba utawala wake unashughulikia suala hilo kwa haraka.
Afisa wa Israel pia aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba mazungumzo yalikuwa katika hatua za juu, na makubaliano yanawezekana kwa saa, siku au zaidi.
Rais wa Marekani Joe Biden alizungumza na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu siku ya Jumapili, na Sheikh Tamim bin Hamad Al-Thani wa Qatar ambaye ni mpatanishi wa mazungumzo hayo siku ya Jumatatu.