Ab-Titchaz
JF-Expert Member
- Jan 30, 2008
- 14,630
- 4,253
- Thread starter
-
- #21
Kama unakubali hili, huoni kuwa Israeli nao wana hakk ya kuifuta Iran kutoka kwenye ramani ya dunia?
Wao tangu vita ya 1967 wamekalia ardhi ambayo siyo ya kwao kwa miaka 41 sasa wakati dunia imefumbia macho swala hilo. Hakuna nchi yeyote duniani ambayo itakubali ardhi yao ikaliwe na Taifa jingine duniani. Katika vita vyetu na nduli hatukuikalia hata mita moja ya nchi yao mara baada ya vita vile kumalizika rasmi.
Mkuu,
kumbuka kua either way the die has been cast,
and somebody will eventually blink and cast the first stone.
Who it will be ...I dont know... but I know for sure kama
Israeli will cast the first kama walivyofanya na Iraq, then
Iran will hit back and then the marigedi will tokota kinoma!
Meanwhile I don't condone war in any form and in this case
siasa za Middle East hazitotatuliwa leo na sio kwa mapanga
Hakuna nchi duniani yenye haki ya kujiamulia mambo mazito kivyakevyake..Na ndo maana kuna bodies mbalimbali za kuregulate mambo haya ya nuclear n.k. Si rahisi mtu eti kwa sababu ni nchi huru ukaruka mipaka ya convection za kimataifa..Never..
Bonge la pointi mkuu....waambiwe wamarekani na Wa-Israeli ambao
wamekataa kusign mikataba against landmines, cluster bombs, torture,
nuclear proliferation...the list goes on!
Mkuu,
Mi nadhani Iran ndo ya kulaumiwa, maana ndo inaanza kuvuta kamba ya kutegua ugomvi..
Au wewe unaonaje?
Bw. Mwanjelwa ktk post # 11 ametoa point moja ambayo naiona imetulia. Anasema kuwa hawa mabwanavita wa Mashariki ya Kati wana tatizo la uongozi wa kidikteta na serikali vinazoongozwa nyuma ya pazia na mamullah au viongozi fundamentalists.
Hali hii inawapa woga magharibi kuwaruhusu kuwa na zana nzitonzito maana..the rest inajulikana..
Kumbuka kuwa ISrael isipopata Signals from USA ni Risk Taking. Je kama Israel isipofanikiwa kulipua hivyo vinu vya Nuklea, imagine nini kitatokea. Hii itakuwa vita kubwa sana. Na Tanzania tutaathirika kwa namna moja au nyingine. Example utalii utayumba. Mwaka huu sekta ya utalii imeongoza kwa kuliingizia taifa pato
Mnaukandamiza Uislamu.
Hehe ab-tichaz umelenga pale nilipogusia mwanzo kuwa Iraq ni buffer zone..
...afu mkuu, nani atakua anamiliki Iraq at that time?
Bush doctrine ingewawezesha wamarekani kukaa Iraq and make it
a buffer zone(refuelling station for the jets after bombing the reactors)
lakini kama watakua washaondoka na the Iranian influence ikitandaa
Iraq (as we are being told) basi wayahudi itabidi waepue mbinu nyengine.
At best, this will be an interesting piece of historical footnote...but
I don't know if I wanna experience this kind of history...😕
Ni makosa kusema Israeli inaikalia ardhi ambayo si yake. Ownership ya ardhi ni kitu dynamic.
Historia inatukumbusha mengi kuhusu struggle na maingiliano baina ya watu mbalimbali duniani pote. Hapa Tz tunaweza kuona mfano wa jamii ya Wangoni..kutoka vuguvugu lililosababisha kuhama kwao kutoka pembezoni mwa Afrika mpaka kuingia ktkt kabisa ya continent.
Lazima tukubaliane kuwa hapa duniani ili tuishi kwa amani inabidi turidhike na principle ya survival of the fittest, ambapo resources humilikiwa zimilikiwe na mtu/watu powerful..Unapozidiwa ukubali kuchukua defeat.
Hakuna makosa yoyote yale. Mipaka ya Kimataifa inaeleweka. Hata katika majaribio ya Clinton alipokuwa Rais katika kutafuta suluhisho la Wapalestina na Wayahudi hili la kurudisha ardhi iliyotekwa na Wayahudi 1967 lilikuwemo. Hivyo si siri kwamba wamekalia ardhi ambayo kimataifa inajulikana siyo ya kwao. Vinginevyo sheria za kimataifa hazina umuhimu wowote wa kuwepo, maana mwenye nguvu mwache afanya anavyotaka na wale wanyonge wanyamaze tu. Kweli mkuki kwa nguruwe....
Sasa kibao kinageuka wababe wa dunia watakuwa siyo tena Marekani bali China huku wakishirikiana na Russia na nchi za kiarabu hapo ndipo principle ya survival of the fittest itaonekana uzuri wake kwa Taifa kubwa. Wana deni la nje $10.5 Trillioni na linaongezeka kwa haraka sana, wana budget deficit ya $500 billioni nayo inaongezeka kwa haraka sana. Kwa kipindi kirefu kijacho watakuwa katika hali ngumu kunyanyua uchumi wao tena, kupambana na budget deficit na deni la nje. Na kwa kuwa uchumi wao umeathirika vibaya sana hawatakuwa na uwezo wa kuwapa Israel $3 billioni kila mwaka.
Naimani hata kama uchumiwa wa Ulaya utadidimia kiasi gani hawatosita kuleta hela ya bajeti hapa TANZANIA