Israel Preparing Options To Strike Iran...

Kama unakubali hili, huoni kuwa Israeli nao wana hakk ya kuifuta Iran kutoka kwenye ramani ya dunia?

Mkuu,

kumbuka kua either way the die has been cast,
and somebody will eventually blink and cast the first stone.
Who it will be ...I dont know... but I know for sure kama
Israeli will cast the first kama walivyofanya na Iraq, then
Iran will hit back and then the marigedi will tokota kinoma!

Meanwhile I don't condone war in any form and in this case
siasa za Middle East hazitotatuliwa leo na sio kwa mapanga
 
Wao tangu vita ya 1967 wamekalia ardhi ambayo siyo ya kwao kwa miaka 41 sasa wakati dunia imefumbia macho swala hilo. Hakuna nchi yeyote duniani ambayo itakubali ardhi yao ikaliwe na Taifa jingine duniani. Katika vita vyetu na nduli hatukuikalia hata mita moja ya nchi yao mara baada ya vita vile kumalizika rasmi.

Ni makosa kusema Israeli inaikalia ardhi ambayo si yake. Ownership ya ardhi ni kitu dynamic.

Historia inatukumbusha mengi kuhusu struggle na maingiliano baina ya watu mbalimbali duniani pote. Hapa Tz tunaweza kuona mfano wa jamii ya Wangoni..kutoka vuguvugu lililosababisha kuhama kwao kutoka pembezoni mwa Afrika mpaka kuingia ktkt kabisa ya continent.

Lazima tukubaliane kuwa hapa duniani ili tuishi kwa amani inabidi turidhike na principle ya survival of the fittest, ambapo resources humilikiwa zimilikiwe na mtu/watu powerful..Unapozidiwa ukubali kuchukua defeat.
 
Mkuu,

kumbuka kua either way the die has been cast,
and somebody will eventually blink and cast the first stone.
Who it will be ...I dont know... but I know for sure kama
Israeli will cast the first kama walivyofanya na Iraq, then
Iran will hit back and then the marigedi will tokota kinoma!

Meanwhile I don't condone war in any form and in this case
siasa za Middle East hazitotatuliwa leo na sio kwa mapanga

Mkuu,

Mi nadhani Iran ndo ya kulaumiwa, maana ndo inaanza kuvuta kamba ya kutegua ugomvi..

Au wewe unaonaje?
 
Hakuna nchi duniani yenye haki ya kujiamulia mambo mazito kivyakevyake..Na ndo maana kuna bodies mbalimbali za kuregulate mambo haya ya nuclear n.k. Si rahisi mtu eti kwa sababu ni nchi huru ukaruka mipaka ya convection za kimataifa..Never..

Bonge la pointi mkuu....waambiwe wamarekani na Wa-Israeli ambao
wamekataa kusign mikataba against landmines, cluster bombs, torture,
nuclear proliferation...the list goes on!
 
Bw. Mwanjelwa ktk post # 11 ametoa point moja ambayo naiona imetulia. Anasema kuwa hawa mabwanavita wa Mashariki ya Kati wana tatizo la uongozi wa kidikteta na serikali vinazoongozwa nyuma ya pazia na mamullah au viongozi fundamentalists.

Hali hii inawapa woga magharibi kuwaruhusu kuwa na zana nzitonzito maana..the rest inajulikana..
 
Mkuu,

Mi nadhani Iran ndo ya kulaumiwa, maana ndo inaanza kuvuta kamba ya kutegua ugomvi..

Au wewe unaonaje?

Wenyewe watakuuliza unatumia kigezo gani kutoa lawama?
Watakuambia based on history, the Jews have been the
aggressors in the Middle East confrontation.
 
Bw. Mwanjelwa ktk post # 11 ametoa point moja ambayo naiona imetulia. Anasema kuwa hawa mabwanavita wa Mashariki ya Kati wana tatizo la uongozi wa kidikteta na serikali vinazoongozwa nyuma ya pazia na mamullah au viongozi fundamentalists.

Hali hii inawapa woga magharibi kuwaruhusu kuwa na zana nzitonzito maana..the rest inajulikana..

..Na hapo ndipo ngoma ilipo...nyuma ya hizo pazia!
 
Wanajuana hawa watu wa Middle East....Ila hii vita ikilipuka itakiwa ni Western Europe against Iran...
By the way Iraq ni buffer zone!!!
 
Kumbuka kuwa ISrael isipopata Signals from USA ni Risk Taking. Je kama Israel isipofanikiwa kulipua hivyo vinu vya Nuklea, imagine nini kitatokea. Hii itakuwa vita kubwa sana. Na Tanzania tutaathirika kwa namna moja au nyingine. Example utalii utayumba. Mwaka huu sekta ya utalii imeongoza kwa kuliingizia taifa pato
 
Last edited by a moderator:

...It will be a blunder of astronomic proportions.

Safari ya kutokea Israel kuelekea Iran lazima wapitie Iraq (kama watatumia
ndege).Hio safari ndefu ambapo hata wakitimiza kuenda one way kuna
swala la kurudi kwao.Lazima waland katika safe zone na hapo ndo maswala
ya logistics yanapojitokeza.

Kweli lazima wapate green light kutoka US maana ndio wadhamini wao
wakuu.Pia hao nd'o watakaosaidia na clean up of the aftermath.Kweli itakua
shy sana kama wataenda safari yote hio kisha washindwe kutengue hivyo
vinu.....
 
Last edited:
Hehe ab-tichaz umelenga pale nilipogusia mwanzo kuwa Iraq ni buffer zone..
 
Mnaukandamiza Uislamu.

Yoyo,

Vipi tena mkuu mwenzangu?

Uislamu like any other religion is here to stay na hao
wanaopiga vita wafahamishwe hio kitu.If this thing is
turned into a religious campaign then I'm moving to Mars
maana sijui how mankind will co-exist after that.

But the irony of it all is that, if a fight ever breaks out,
itageuzwa kua swala la udini wa tabaka moja kujaribu
kukandamiza tabaka lengine.
 
Hehe ab-tichaz umelenga pale nilipogusia mwanzo kuwa Iraq ni buffer zone..

...afu mkuu, nani atakua anamiliki Iraq at that time?

Bush doctrine ingewawezesha wamarekani kukaa Iraq and make it
a buffer zone(refuelling station for the jets after bombing the reactors)
lakini kama watakua washaondoka na the Iranian influence ikitandaa
Iraq (as we are being told) basi wayahudi itabidi waepue mbinu nyengine.

At best, this will be an interesting piece of historical footnote...but
I don't know if I wanna experience this kind of history...😕
 
Ukweli ni kwamba iran haiwezi kuondoa Israel,nakama ikitokea the sun will be no more shining believe me.kwasababu Quran imesema hakuna Mungu kama wa waisrael.g9t
 
...afu mkuu, nani atakua anamiliki Iraq at that time?

Bush doctrine ingewawezesha wamarekani kukaa Iraq and make it
a buffer zone(refuelling station for the jets after bombing the reactors)
lakini kama watakua washaondoka na the Iranian influence ikitandaa
Iraq (as we are being told) basi wayahudi itabidi waepue mbinu nyengine.

At best, this will be an interesting piece of historical footnote...but
I don't know if I wanna experience this kind of history...😕

Hii kitu inanikumbusha Executive Orders by Tom Clancy(Iran wanavamia Iraq wanaform nchi moja alafu wanamove on kutaka kutawala Saudi Arabia na Kuwait). Msimamo wa Saudi Arabia kwenye hili swala ni upi?

McCain angeshinda hii vita ingelipuka baada ya kuapishwa tu, ila yule mama akichukua uwaziri mkuu wa Israel hapo Middle East patachafuka zaidi ya sasa hivi.
 
Ni makosa kusema Israeli inaikalia ardhi ambayo si yake. Ownership ya ardhi ni kitu dynamic.

Historia inatukumbusha mengi kuhusu struggle na maingiliano baina ya watu mbalimbali duniani pote. Hapa Tz tunaweza kuona mfano wa jamii ya Wangoni..kutoka vuguvugu lililosababisha kuhama kwao kutoka pembezoni mwa Afrika mpaka kuingia ktkt kabisa ya continent.

Lazima tukubaliane kuwa hapa duniani ili tuishi kwa amani inabidi turidhike na principle ya survival of the fittest, ambapo resources humilikiwa zimilikiwe na mtu/watu powerful..Unapozidiwa ukubali kuchukua defeat.

Hakuna makosa yoyote yale. Mipaka ya Kimataifa inaeleweka. Hata katika majaribio ya Clinton alipokuwa Rais katika kutafuta suluhisho la Wapalestina na Wayahudi hili la kurudisha ardhi iliyotekwa na Wayahudi 1967 lilikuwemo. Hivyo si siri kwamba wamekalia ardhi ambayo kimataifa inajulikana siyo ya kwao. Vinginevyo sheria za kimataifa hazina umuhimu wowote wa kuwepo, maana mwenye nguvu mwache afanya anavyotaka na wale wanyonge wanyamaze tu. Kweli mkuki kwa nguruwe....

Sasa kibao kinageuka wababe wa dunia watakuwa siyo tena Marekani bali China huku wakishirikiana na Russia na nchi za kiarabu hapo ndipo principle ya survival of the fittest itaonekana uzuri wake kwa Taifa kubwa. Wana deni la nje $10.5 Trillioni na linaongezeka kwa haraka sana, wana budget deficit ya $500 billioni nayo inaongezeka kwa haraka sana. Kwa kipindi kirefu kijacho watakuwa katika hali ngumu kunyanyua uchumi wao tena, kupambana na budget deficit na deni la nje. Na kwa kuwa uchumi wao umeathirika vibaya sana hawatakuwa na uwezo wa kuwapa Israel $3 billioni kila mwaka.
 
Wanatakiwa kukumbuka kuwa Iran sio Iraq, muziki utakaochezwa baada ya jaribio hilo kufanikiwa au kushindwa unaweza kuja kumbukwa kama wanavyomkumbuka Hitler. Mwiba wa Israel uko Lebanon na Syria, proxies za Iran, ambazo zinasubiri orders tu kufanya mambo. Cha muhimu hapa ni kuangalia what will be the cost of denying Iran the nukes, and what will be the cost of letting it have them and concetrate and building up a deterence. Mabomu ya nyuklia huwa hayatumiwi, yanawekwa kwa vitisho tu na kutaka heshima. Let us wait and see, kama wakitaka kujaribu moto basi wajaribu.
 
Hakuna makosa yoyote yale. Mipaka ya Kimataifa inaeleweka. Hata katika majaribio ya Clinton alipokuwa Rais katika kutafuta suluhisho la Wapalestina na Wayahudi hili la kurudisha ardhi iliyotekwa na Wayahudi 1967 lilikuwemo. Hivyo si siri kwamba wamekalia ardhi ambayo kimataifa inajulikana siyo ya kwao. Vinginevyo sheria za kimataifa hazina umuhimu wowote wa kuwepo, maana mwenye nguvu mwache afanya anavyotaka na wale wanyonge wanyamaze tu. Kweli mkuki kwa nguruwe....

Sasa kibao kinageuka wababe wa dunia watakuwa siyo tena Marekani bali China huku wakishirikiana na Russia na nchi za kiarabu hapo ndipo principle ya survival of the fittest itaonekana uzuri wake kwa Taifa kubwa. Wana deni la nje $10.5 Trillioni na linaongezeka kwa haraka sana, wana budget deficit ya $500 billioni nayo inaongezeka kwa haraka sana. Kwa kipindi kirefu kijacho watakuwa katika hali ngumu kunyanyua uchumi wao tena, kupambana na budget deficit na deni la nje. Na kwa kuwa uchumi wao umeathirika vibaya sana hawatakuwa na uwezo wa kuwapa Israel $3 billioni kila mwaka.

Naimani hata kama uchumiwa wa Ulaya utadidimia kiasi gani hawatosita kuleta hela ya bajeti hapa TANZANIA
 
Last edited:
Naimani hata kama uchumiwa wa Ulaya utadidimia kiasi gani hawatosita kuleta hela ya bajeti hapa TANZANIA

Labda, lakini sidhani. Nchi ina unemployment ya 10% au zaidi halafu wananchi wao wanasikia nchi yao wameipa nchi ya Afrika msaada wa pound 200 millioni ili kujenga barabara kiongozi huyo anajiharibia PR yake na wananchi wake. Watamuuliza kwa nini hizo pound 200 millioni hukuzitumia kucreate jobs badala ya kwenda kutoa msaada nchi ya Afrika? Uchaguzi mwingine ukija atapigwa mueleka.

Mimi naamini kwa Tanzania tunaweza kabisa kujitosheleza wenyewe bila msaada wa mtu kama viongozi wetu wangekuwa makini katika kusaini mikataba inayohusu rasilimali zetu yenye maslahi, kupunguza gharama kubwa za uendeshaji serikali ambazo haziongezi tija yoyote na kuhakikisha utajiri wetu tuliojaliwa unatumika kuinua maisha ya Watanzania wote.
 
Back
Top Bottom