Israel yaishambulia Syria kujibu mashambulizi ya anga

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Jeshi la Israel limesema lilishambulia betri za makombora nchini Syria baada ya kombora la kutungulia ndege kurushwa kuelekea Israel wakati ambapo televisheni ya taifa ya Syria iliripoti kuwa ni shambulio la awali karibu na Damascus Shirika la Reuters linaripoti .

Msemaji wa jeshi alikataa kuzungumzia ripoti ya Syria ya shambulio la awali la Israel karibu na mji mkuu wa Syria ambalo liliripotiwa kumuua mwanajeshi mmoja na kujeruhi watano.

Lakini jeshi lilisema lilifanya shambulio la kujibu Syria baada ya kurusha kombora la kutungua ndege.

Ilisema kuwa kombora hilo lilifyatua ving'ora katika maeneo ya Israel na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, na kulipuka angani.

"Kufuatia kurushwa kombora la kutungulia ndege mapema usiku wa kuamkia leo, Vikosi vya Ulinzi vya Israel vilishambulia betri za makombora ya kutoka ardhini hadi angani na rada ambazo zilirusha ndege za jeshi la anga la Israeli," jeshi lilisema kwenye Twitter.

Televisheni ya serikali ya Syria ilisema hapo awali kwamba Kikosi cha ulinzi wa anga cha Syria kilidungua idadi ya makombora ya Israeli juu ya Damascus.

Israel ilirusha makombora kutoka kwa Miinuko ya Golan inayokaliwa na Israel na ulinzi wa anga wa Syria ukaangusha baadhi yao, televisheni ya taifa ya Syria ilisema.
 
Wameharibu Mifumo ya Ulinzi ya Syria ambayo ilirusha Makombora nchini Israel.

Waziri mkuu wa zamani wa Israel alishaiambia Urusi kwamba,Operation zake nchini Syria hazilengi Majeshi ya Urusi Wala wa Syria Bali Miundombinu ya Wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran. Lakini akaonya,endapo Mifumo ya Ulinzi ya Syria au Urusi itazishambulia ndege za kivita za Israel zinazofanya operations zake ndani ya Syria dhidi ya Iran Basi hatasita kuiharibu Mifumo hiyo ya Ulinzi. Hiki ndicho kilichotokea leo hii.
 
Back
Top Bottom