Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Watu zaidi ya laki moja waliohamishwa kaskazini ya Israel kwa hofu ya Hizbullah sasa wamekuwa ni ajenda kubwa inayojadiliwa na viongozi wa nchi hiyo.
Kwanza watu hao wamekuwa mzigo kwa uchumi kwani wamewekwa kwenye maeneo kama hoteli kwa malipo ya serikali.Vile vile maeneo yaliyohamwa ni maeneo muhimu ya uchumi na uzalishaji kwa ujumla.
Malalamiko kutoka kwa watu hao yamekuwa ni makubwa sana.Kwa upande mwengine hali hiyo imekuwa ni aibu kubwa kwa viongozi kutengeneza wakimbizi wa ndani
Jambo hilo limeifanya serikali ya Netanyahu kuongeza lengo jengine la vita vyake vya Gaza kuwa ni kuwarudisha wananchi hao maeneo yao.
Ikumbukwe sababu ya kuhamishwa kwao ilikuwa ni kitisho cha kufikiwa na mashambulizi ya Hizbullah.Kitisho hicho badala kupungua kila siku kimekuwa kikiongezeka kwani Israel bado haijafikia muafaka wa kusitisha vita kule Gaza na wala hawajafanikiwa kufikia malengo waliyojiwekea eneo hilo.
Kinachoonekana hapa kwa mfuatiliaji mzuri wa vita hivi ni kwamba baada ya mwaka mmoja wa vita Israel sasa imeanza kuchanganyikiwa na kuona vitisho vilivyo mbele yao vikiongezeka kwa namna tofauti kupelekea kuchukua maamuzi yenye utata.