#COVID19 Israel yaweka zuio la kusafiri karibu nchi zote za Afrika

SNAP J

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2013
Posts
7,106
Reaction score
8,043
Karibu Nchi zote za Africa, kasoro zile zinazopatikana kaskazini mwa Africa (Northern African countries) zimepigwa ban na taifa la Israel ijumaa ya tarehe 26 Novemba 2021 kutokana na hatari ya kirusi kipya cha korona kilichopewa jina na la "Omicron" na shirika la afya duniani WHO ambacho kiligunduliwa Africa ya kusini wiki moja iliyopita.

Watu kutoka mataifa hayo ya Africa hawataruhusiwa kuingia Israeli.

Mpaka sasa mataifa mbali mbali duniani yameshaweka zuio la kusafiri katika nchi ya South Africa pamoja na nchi zinazopatikana kusini mwa bara la Africa kutokana na hofu ya kirusi hicho cha"Omicron".

42364222_101.jpeg
 
Ina maana Israel hawajui kwamba Tanzania mama anaupiga mwingi? Wanatuzuiaje kwenda kwao tena?
 
Kwa nini wanazuia usafiri wakati watu wamepata Chanjo ya Corona?
Kwa nini wanataka kuwaweka wasafiri karantini wakati wamepata Chanjo?
Inatosha kuamini kuwa hiki kirusi kitahitaji Chanjo nyingine jina linabadilishwa Na kuitwa Bust
 
Ni bahati mbaya tu wametaja south africa ili kirusi kionekane kimetokea africa ila icho kirusi kipo europe muda sana tu ndio kimesababisha ma hospital ya uholanzi yamezidiwa wagonjwa hadi wanapeleka ujerumani… wametafuta tu jumba bovu limwangukie nani
 
wazungu ni wajinga sana ,eti chanjeni muwe salaama,wanatia hasira kumbe wanatufanyia majaribio,poleni mliochanja
 
Ni bahati mbaya tu wametaja south africa ili kirusi kionekane kimetokea africa ila icho kirusi kipo europe muda sana tu ndio kimesababisha ma hospital ya uholanzi yamezidiwa wagonjwa hadi wanapeleka ujerumani… wametafuta tu jumba bovu limwangukie nani
Wazungu Wana fitna mingi sana😠
 
Tanzania tujiandae.

South Africa watu wanalia huko .
Makampuni ya ndege, mahotel, AirBnB, nasekta ya kitalii kwa ujumla yameshaadhirika VIBAYA baada ya watalii ku-cancel safari zao kueleka msimu wa sikuu za Christmas.
Janga kubwa hili.
 
Karibu Nchi zote za Africa, kasoro zile zinazopatikana kaskazini mwa Africa (Northern African countries) zimepigwa ban na taifa la Israel ijumaa ya tarehe 26 Novemba 2021 kutokana na hatari ya kirusi kipya cha korona kilichopewa jina na la "Omicron" na shirika la afya duniani WHO ambacho kiligunduliwa Africa ya kusini wiki moja iliyopita.

Watu kutoka mataifa hayo ya Africa hawataruhusiwa kuingia Israeli.

Mpaka sasa mataifa mbali mbali duniani yameshaweka zuio la kusafiri katika nchi ya South Africa pamoja na nchi zinazopatikana kusini mwa bara la Africa kutokana na hofu ya kirusi hicho cha"Omicron".

View attachment 2025278

Tumekuckia baba,,,nawasubiri wayahudi weuc watakuwa na maoni gani kuhusu hili.
 
Back
Top Bottom