Israeli yaelekea kushindwa kuwamaliza na kuwateketeza kundi la Hamas kama walivyoahidi

Israeli yaelekea kushindwa kuwamaliza na kuwateketeza kundi la Hamas kama walivyoahidi

Eti wapiganaji wa Hamas kujitangazia ushindi!! Wakiwa wapi? Humo kwenye mahandaki?

Hivi nyie ndugu zetu katika Imani mna matatizo Gani? Ndo maana Kuna Mtume mwingine wa Hezbollah anasema eti vita ya Gaza iliyoteketeza watu zaidi ya 25,000 lengo lilikuwa ni kupima uwezo wa Israel. Pathetic

Imani zingine ni majanga duniani
Mbona mleta mada alivyokuja hajahusisha dini na hajataja dini yake husika??
Mie naona watu mnaogeuza mijadala ya kidiplomasia kuwa ya kidini ni wajinga msiojielewa.
Jielewe kijana acha udini.
Hapo imezungumziwa vita sio dini.
Na ni kweli IDF anahelemewa tena sana tu.
Nitajie vita IDF aliopata wanajeshi wengi walemavu kupita hii??
Mpaka sasa kuna walemavu wakudumu 8000 ambao ni askari wa IDF..
 
Naam, tarehe rasmi ya kuitambua Palestina kama taifa huru imepangwa kuwa ni 28 mwezi huu wa Mei.

Nchi za Ireland, Norway na Hispania zimetangaza rasi kuwa zaenda kuitambua rasmi Palestina kama taifa huru na linojitegemea.

Hivyo kuanzia tarehe 28 Mwezi huu wa Mei nchi hizo zitaweza kuwa na wawakilishi wa kibalozi katika taifa la Palestina ambao wataeza kuwa na ofisi katika nchi za kiarabu kama Jordan na Misri kwa kuanzia.

Hii ni hatua ingine kubwa ambayo imechukuliwa na nchi hizi tatu na pia ni mwendelezo wa tathmini yangu kuwa Israeli imeshindwa kuwamaliza Hamas na kuteketeza kabisa kundi hilo.

Pia hatua hii yafuatia uamuzi wa mahakama ya kimataifa ya ICC kuwa imetoa ombi la kukamatawa kwa waziri mkuu wa Israeli, waziri wake wa ulinzi na baadhi ya mawaziri pamoja na viongozi watatu wa kundi la Hamas kwa kukiuka sheria za kimataifa juu ya haki za binadamu zinofanyika huko Ukanda wa Gaza.
 
Norway ndo nchi ilowakutanisha kiongozi wa Palestina Yaser Arafat na Ehud Yitzhak Rabin mwaka 1990 mjini Oslo na kitendo kilofuatiwa na jina la Oslo Accord.

Mwaka 1993 ndipo mkataba rasmi wa kwanza wa kulitambua taifa la Palestina uloitwa "Oslo Agreement" ukasainiwa kati ya Arafat na Rabin mbele ya Raisi Bill Clinton pale Camp David mjini Washington.

Mkataba wa pili wa Oslo Accord II ulisainiwa mjini Cairo nchini Misri mwaka 1995.
 
Back
Top Bottom