Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Baada ya Iran kutuma makombora ya Ballisctic jana kaskazini mwa Israeli na kuharibu baadhi ya miundombinu ikiwemo majengo ya idara ya ujasusi ya Mossad, Israeli imekuwa kimya ikifanya vikao vya kupanga namna ya kujibu mapigo.
Kwa mujibu wa wachambuzi kadhaa wa masuala ya vita, Iran ilifanikiwa kufanya uharibifu mkubwa katika katika maeneo kadhaa kaskazini huku ikichukua tahadhari kubwa ya kutoua raia wengi. Kwa kuwa raia wengi wa Israeli walikwishapewa tahadhari ya kwenda kujificha, makombora hayo yaliweza kuharibu majengo kama shule, na kambi za jeshi la anga pamoja na makao makuu ya idara ya Mossad.
Na kama si msaada wa mitambo ya kudaka makombora hayo ilotolewa na UK, Marekani na Jordan, Israeli ingekuwa imeharibiwa vibaya eneo hilo la kaskazini ukizingatia kuwa ni makombora zaidi ya 180 yalitumwa na Iran.
Uchambuzi wa gazeti la Guardian la UK umeangalia namna Iran ilivyoamua kufanya mashambulizi haya lakini kwa kutoa taarifa kwanza kwa Marekani na Russia bila kutoa muda maalum wa kujiandaa, Explainer, The Guardian October 2nd, (2024).
Jeshi la ukombozi la Iran IRGC limetoa onyo kwa Israeli kutojaribu kijibu mapigo hayo na endapo itafanya hivyo Iran itashambulia zaidi kwa makombora na silaha zingine nyingi.
Ahron Bregman mhadhiri mwandamizi wa stadi za vita katika chuo kikuu cha Kings College London, asema Israeli haiwezi kujibu mashambulizi hayo kwa kupiga vinu vya nyuklia wazo ambalo laungwa mkono na raisi Joe Biden ambae leo hii mchana akihojiwa na waandishi wa habari amesema haungi mkono mashambulizi katika vinu vya nyuklia isipokuwa kuzidisha vikwazo zaidi vya kiuchumi kwa Iran.
Akiongea mapema leo waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ameapa kulipiza kisasi kwa Iran jambo ambalo halijaungwa mkono na waziri mkuu wa UK bwana Keir Starmer ambae akiongea na waandishi wa habari jioni hii amesema pamoja na kwamba Israeli yastahiki kujilinda na usalama wake UK yaunga mkono juhudi zozote za kusitisha mapigano kati ya Iran na Israeli.
Lakini je , ni aina gani ya mashambulizi ambayo Israeli itaweza au kushindwa kufanya juu ya Iran?
Kushambulia vyanzo vya gesi na mafuta.
Shambulizi hili litaweza kuharibu miundombinu ya mafuta na gesi nchini humo na kusababisha mathara kiuchumi na hilo litaweza kusababisha sintofahamu nchini humo kwa bei ya mafuta kupanda kutokana na uhaba kwa visima vya mafuta vyote kuwa vyaungua moto.
Mashambulizi ya pamoja yaani "simultaneous attacks or targeted assassinations" ndani ya Iran.
Israeli yaweza kufanya mashambulizi kama hilo la hapo juu na pia wakati huohuo likafanya mauaji ya mmoja wa viongozi wa juu wa nchi hiyo kama Ayatollah Khamenei. Benjamin Netanyahu akiongea leo amesema kuwa viongozi wa Iran waonekana hawaelewi somo na wameshindwa kuelewa somo, jambo linoashiria kuwa atoa tishio la maisha kwa Khamenei au viongosi wengine wa juu wa taifa hilo. Itakumbukwa kuwa Ismail Haniyeh na kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallha wote wameuliwa ndani ya Iran na kile kinachosemwa kuwa ni majasusi wa Mossad ingawa Israeli haijakataa wala kukubali kuhusika na mauaji hayo.
Shambulizi dhidi ya vinu vya nyuklia.
Shambulizi hili litalenga kuzorotesha umaliziaji wa mradi wa nyuklia ambao Iran imekuwa ikiuboresha na kwa kuwa israeli wanazo picha za maeneo hayo yote kazi ya kushambulia itakuwa ni ndogo. Lakini wazo hili nchi za UK, Ufaransa, na Marekani zimeionya Israeli dhidi ya mashambulizi hayo ambayo hata balozi wa Iran katika umoja wa mataifa Amir Saeid Iravan amesema leo kuwa yatasababisha madhara makubwa katika eneo la mashariki ya kati .
Mashambulizi dhidi ya maeneo maalum pamoja na mifumo ya ulinzi wa anga.
Israeli ikiwa yajianda ndani ya siku chache zijazo pia yaangalia uwezekano wa kushambulia maeneo maalum au mifumo ya ulinzi wa anga jambo ambalo pia linazuiwa kwa kuzingatia kuwa anga la Iran bado lachukuliwa kuwa ni muhimu kwa matumizi ya ndege mbalimbali zinotua humo. Jambo hili lasisitizwa na pia kuwepo na ugeni wa Sergei Lavrov waziri wa mambo ya nje wa Russia ambae leo hii ametua Iran kwa ziara ya siku chache.
Pia raisi wa Iran Masoud Pezeshkian, leo pia akiwa mjini Doha nchini Qatar amesema Iran yataka kuwepo amani ya kudumu katika eneo hilo na pia yupo tayari kuwezesha kuwepo kwa mazungumzo ya amani kati ya Israeli na Hamas kuhusu Gaza. Pia akizungumza na Lavrov kabla ya kwenda Doha, Pezeshkian amesema lengo kuu la mashambulizi ya Iran kwa Israeli lilikuwa ni kuikumbusha Israeli kuwa na tahadhari ya vita yake wanoiendeleza katika eneo hilo la mashariki ya kati.
Pamoja na hayo yote bado yaonekana Israeli imepania kupanua wigo wake wa vita kutoka Gaza, Lebanon, Syria, Yeman Iraq na maeneo.
Nyuma ya pazia Marekani imekuwa ikiishawishi Israeli kutochukua maamuzi ambayo yatakuja kuigharimu ingawa yote yaonyesha kuwa yamepuuzwa na Israeli chini ya uongozi wa Benjamin Netanyahu kwamba Iran ni tatizo katika eneo la mashariki ya kati na ni mhimili wa kishetani unopaswa kubomolewa.
Akitoa hotuba ilojaa jazba katika mkutano wa umoja wa mataifa wiki ilopita, Netanyahu alidai kuwa sasa hivi eneo la mshariki ya kati limegawanyika katika pande mbili yaani upande ambao umelaaniwa ambao wajumuisha nchi za Iran, Iraq na Syria na upande wa pili ukiwa ni ule ulobarikiwa ukijumuisha nchi za Saudi Arabia, Sudan na Misri.
Lakini ni dhahiri kuwa Israeli bado itahitaji msaada mkubwa kutoka kwa wahisani wake wakubwa Marekani pamoja na UK, Ufaransa na nchi zingine zilozo nyuma ya pazia kama Jordan na Cyprus ambazio zasaidia kukinga na kudaka makombora kutoka Iran pamoja na kurusha ndege za kivita kwenda kukabiliana na makombora hayo.
Ni miezi 12 sasa tangia Hamas wafanye mashambulizi yao terehe 7 mwezi October na bado Israeli ipo vitani huku ikisogea zaidi katika emel la tukio likiwa ni Lebanon ambalo ndilo laelezwa kuwa litakuwa ni kitovu cha maamuzi.