Issa Michuzi na vekesheni

Status
Not open for further replies.
anawafisadi kivipi?
 
mkuu nikuulize swali...

....ulifehemu ratiba ya Mr michuzi akiwa majuu?
 
... blog yake yenye wafadhali wenye pesa kama VODACOM, je wewe unayehoji unajua vodacom wanamlipa shilingi ngapi kuwatangaza kwa wadau millioni sita dunia nzima walipo wabongo,je jamii forum mnao wafadhili
Mmmh, ndugu!!! Umejiunga ili kuishambulia JF?

Mbona members wengi tu wa JF pia ni wadau wa kule Michuzi? Au unadhani hii thread ni JF Vs Michuzi?

Kama ingekuwa hivyo wala usingeona debate humu, ingekuwa ni conclusion tu. Kwanza hata wewe kuweza kupost humu tayari ni member, kwa hiyo suala la iwapo JF tuna wafadhili au la ni la member wote, ukiwamo na wewe!!

Sisi tuna mfuko wetu, anayepata anaweka, mambo mengine hayo ni ya JF Management, we are proud of it, na ni marafiki wa watu wote including Michuzi
 
Last edited:
mkuu nikuulize swali...

....ulifehemu ratiba ya Mr michuzi akiwa majuu?

Ratiba ya nini? Kwani hukuona picha ya white house? Ama unataka kusema ameenda white house yeye kama Mithupu?
Sina haja ya kulumbana,michuzi ni kazi yake kufafanua,kama huna habari za uhakika kuhusu vekesheni yake wakati wa ziara ya kikazi ya Rais ni bora ukae kimya tu. Ama ufuatilie ujue kama amekiuka taratibu za kazi na za kimkataba maana ameajiriwa na serikali,ama?
 
jamani michuzi kutumia neno vekesheni wewe limekuuma nini? hata kama hayuko vacation au yuko vacation si hoja ya kutuletea hapa nadhani kuna hoja za msingi zaidi kujadiliwa...................
 
jamani michuzi kutumia neno vekesheni wewe limekuuma nini? hata kama hayuko vacation au yuko vacation si hoja ya kutuletea hapa nadhani kuna hoja za msingi zaidi kujadiliwa...................

Wengine tulidhani tatizo ni hilo neno "Vekesheni" Lakini inasemekana kuwa ni kweli yuko vacation.
Hakuna mtu mwenye chuki na michuzi,michuzi ni mtu wetu,ila kwenye issue za wananchi especially kodi zao tuwe makini,nidhamu ni muhimu kwenye issue flani zinazogusa maslahi ya wananchi,huwezi kuwa kwenye ziara ya kikazki inayotumia kodi ya wananchi halafu useme uko vekesheni,yeye ndo ana kazi ya kutujulisha kuwa ni neno tu na wala si ufujaji wa pesa za walalahoi kwa vacation badala ya kazi....Fuatilia mjadala na haswa bandiko la Mama.
 

Mama,Jmushi na mauza uza.

Michuzi kaanza kusafiri toka akiwa shirika la Reli,maswali mnayouliza kama kumdhalilisha muajiri wa Michuzi kuwa hajui taratibu za kazi.

Michuzi anatusadia sana waTanzania kwa kutumia muda wake kutuhabarisha hata kabla VODACOM hawaingia nae mkataba.tunapata taarifa za misiba nk vitu vingi muhimu,nadhani tumuunge mkono kwani mwajiri wake hajalalamika kuwa hafanyi kazi.
 

Swali jee amefanya kazi iliyompeleka au hakufanya?ilitakiwa umtathimini kwa vitendo vyake sio kauli yake,michuzi hutumia neno MY WIFE WAKE jee nini tafsiri yake? VAKESHENI imekuuma Mushi?tutajidili ya muhimu hapa michuzi anaonewa.
 
Kwani hii topic ina nini mpaka inaangaliwa hivi? What's so special?

I have to read from the 1st post?
Kwa kuwa kule nako kuna mashtaka ya kuwepo kwa thread hii huku JF, so nadhani member wa kule wengi wao wamefungua JF. You may read from 1st post, but hakuna umuhimu sana Mkuu.
 


Siamini kwamba huyu ni Michuzi, mpiga picha wa gazeti la serikali.
 
Siamini kwamba huyu ni Michuzi, mpiga picha wa gazeti la serikali.
Mama kitu gani kinakufanya usiamini? Au jinsi alivyopozi kipicha picha huku mwenye duka akishangaa? Si yupo kazini na vekesheni?
 

Eeeeh bana eeh,Michuzi kafanya kazi shirika la Reli lini...???Michuzi katoka kupiga picha za mtaani pale margot,Mbowe et al..kajiunga na Daily News au unamuongelea Michuzi mwingine.
Mbona wengi wanasafiri na hatupigi kelele???Hapa kuna issue ya kutumia the so called vekesheni vibaya= UFISADI.
 
kwanini huamini? wewe hii picha unaitafsiri vipi?
YO YO ,

Kazi unayo mzee..utajibu sana ..kwanini usinyamaze tu? Una uhakika gani kama naniii ndiyo kanuunua hiyo makitu...isije ikawa imelipiwa na wadau
 
Mama kitu gani kinakufanya usiamini? Au jinsi alivyopozi kipicha picha huku mwenye duka akishangaa?

Hata mwenye duka anamshangaa,baba mzima na suti, ananunua mguu wa mtoto wa nini???Mpiga picha wa magazeti ya serikali anayeandamana na Rais kila kukicha???au shopping zao ziko hivyo???na huko kwenye plastic bag inaonesha kuna makubwa zaidi!!Ukishangaa ya mussa bado hujaona ya firauni.
Pesa yako ya mfukoni huwezi nunua haya madudu...hizi ni za walipa kodi hazina uchungu hata akijaza maporn dvds yote pouwa.
 

Wewe tatizo lako ni nini hasa? Acha uvivu wa kufikiria kama tulivyo Watz wengi. Wether yuko kikazi au kalipiwa na fedha za kodi, zote ni vokesheni kama anavyosema yeye. La msingi ni kutimiza wajibu wake kama alvyoenda kule. Hii tabia ya uvivu wa kufikiria lazima ikomeshwe kwa watanzania kama tunataka kuendelea.
 
Swali jee amefanya kazi iliyompeleka au hakufanya?ilitakiwa umtathimini kwa vitendo vyake sio kauli yake,michuzi hutumia neno MY WIFE WAKE jee nini tafsiri yake? VAKESHENI imekuuma Mushi?tutajidili ya muhimu hapa michuzi anaonewa.

Kanda2 tusitoke nje ya mjadala,vekesheni imeniuma? Are you sure mkuu? Mbona hiyo anayoita vekesheni yeye ni maisha ya kawaida tu ya kila siku sometimes?
Kinachozungumziwa hapa ni kuhusu matumizi ya pesa za walipa kodi,Kwamba ametumia neno "Vekesheni" Mbona si dili? Hata hivyo habari ni kwamba uko vacation. So ni yeye mwenyewe mwenye majukumu ya kutueleza kuwa ya kazi ni kazi na kwa pembeni kuna vacation.

Na pia jamii ya aina gani tunajenga?Ok maybe kwasababu ni blogu ya Michuzi so tumezoea lugha hizo za kina maiwaifu wangu,Lakini yeye kama mtumishi wa serikali ni halali kusema unakwenda mapumziko badala ya kazini? Tena kwa kutumia pesa za umma?

Mimi nachofahamu ni kuwa kulikuwa na ziara ya Rais USA,na michuzi na yeye alikuwemo,wakati ziara ya Rais ilikuwa ya kikazi,Michuzi alikuwa vacation,sasa kama ni neno tu,yeye ndo aseme na si wewe umsemee.

Ndio maana nikasema toka mwanzo inawezekana ni hilo neno,lakini FMES akaja hapa akasema ni kweli yuko likizo kwani hata Mh Rais keshaondoka,na Michuzi pia na yeye si amesema bado anaedelea na likizo hadi sijui Japan? Nani angemuuliza kuhusu hilo kama hakuanzia na safari ya Mh Rais? Kwani ni mara ngapi Michuzi kasafiri sehemu mbali mbali na hakuna anyeuliza maswali hayo?

Ndio maana nikasema wenye insight zaidi ndo waseme maana ramifications ni nyingi,kuanzia kama hiyo globu yake ni personal ama ina mikataba,kazi zake alizoajiriwa na serikali nk. Hakuna mtu mwenye haja ya kuchimba zaidi ila cha muhimu ni kuhakikisha kodi za wananchi hazifujwi kwani tunataka kuendeleza kizazi cha mizaha inayotu cost kwa kutokuwa serious in almost everything?

Kusema uko vacation wakati uko kazini na halafu ukawa unapost picha zinazoonyesha kuwa uko vacation bila ya kutaja kazi,then watu watajiuliza,labda sasa tutajua kuwa Globu ni globu na Daily News ni Daily News,lets wait n c.
 
Tizama tzuk.com kuna picha ya Sumaye yeye amekwenda kutibiwa uingereza kwa pesa za walipa kodi, lakini amepiga picha yuko kwenye mahubiri ya dini, chanzo cha habari soma Tanzania Daima kwenye maoni ya Richmond kwenda bungeni freemedia.co.tz

Je, Sumaye na Michuzi nani wa kusemwa?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…