Issa Michuzi na vekesheni

Status
Not open for further replies.
Naamini katika motto ya JF, where we dare to talk openly, hivyo naheshimu mawazo ya wote, wanaokubaliana na wasiokubaliana na mada. Ila nalaumu wanaotumia matusi.

Baada ya kusoma michango mbalimbali, nimegundua kuwa watanzania bado tuna safari ndefu sana kuelekea maendeleo na chachu ya kupata uongozi bora.


Nimekuja kuhitimisha kuwa, kukosa elimu ya uraia na kutokujua maadili ya uongozi na pia wajibu na maadili ya mtumishi wa umma, ndiko kunakopelekea hata CCM kuendelea kuchukua ushindi masiku nenda masiku rudi. Kama hapa JF kisiwe kisima cha kukutanisha great thinkers tu, bali kiwe kisima cha kuzalisha hao magreat thinkers. Together WE CAN
help to change Tanzania to become a better place.

Nashauri kama kuna member/s w/anaweza kuweka elimu ya uraia na maadli ya uongozi hapa jamvini, kwa kiasi kidogo tu, na tukawa tunaiupdate hiyo thread appropriately, basi nadhani tutafanikiwa kuwaelimisha na kuwafumbua macho Watanzania walio wengi. Elimu hii iwekwe kwenye jukwaa maalum ambalo members wengi wanaojiunga na ambao hawajui what JF is here for walifunze.

JF haiko kwa ajili ya kutukana, iko kwa ajili ya kuelimisha, kukosoa, kujenga etc.. Hivyo basi hapa Michuzi hatukanwi, haonewi wivu, bali ni scrunity ya kawaida kwa vile yeye ni mfanyakazi wa serikali (analipwa kwa kutumia pesa za wavuja jasho).

Over.

 
Last edited by a moderator:

Ila ujue humu hoja hujobiwa kwa hoja na si matusi mkuu. Michuzi ni rafiki yangu sana ila siwezi kumchekea endapo atafanya ukiukaji wowote kwani najua hakuna kitu kinachoitwa bahati mbaya. Kila jambo limekusudiwa na limepagwa.



Michuzi kahamasisha wadau waje kuchangia hoja hii. Nilidhani angetumia blog yake kuelezea vekesheni zake analipiwa na nani ili 'asishambuliwe'. Kwa nini Michuzi anajihami? Mbona haijawahi kutokea akiwahamasisha wananchi waje kuchangia mashambulizi ya L Masha, Rostam Aziz, Mbowe au Kikwete?

Hii ni dharau kwa wananchi na walipa kodi kwa ujumla kama anawanyali hivi, ilihali analipwa na fedha za wavuja jasho.


Hivyo huyo Tarishi, ni tarishi wa bwana Michuzi, nategemea wanatkuja wengi wa aina yake, Michuzi kawahamasisha kwenye blog yake kama ninavyoiweka hapo chini.
=======================================================================
Kutoka michuzi blog.
WADAU KUNRADHI,
KULE MTAA WA PILI (JAMII FORUM) KUNA MADA AMBAYO IMERUSHWA KWA MDAU ANAYEDAI KUUMIZWA SANA NA VEKESHENI ZA NANIHII, NA KUMSHAMBULIA SANA SANA. WADAU NAOMBA MCHANGIE HOJA HIYO BAADA YA KUISOMA KWENYE LINKI HIYO HAPO CHINI.

KWA UPANDE WANGU MSIKONDE WALA NINI. LIBENEKE LA VEKESHENI LITAENDELEA KAMA KAWA. MIE NARUDI MWEZI UJAO. HIVI SASA NAELEKEA UJERUMANI KISHA NTAENDA AUSTRALIA NA KUMALIZIA JAPAN.
-MICHUZI


https://www.jamiiforums.com/celebrities-forum
/29662-issa-michuzi-na-vekesheni.html



 

WELL SAID TUKO PAMOJA,NIDHAMU YA WOGA NDO INATUKWAMISHA KILA SIKU.....Kwani Michuzi ni nani asikosolewe kama anafanya makosa?????NI KWELI KABISA ANAKULA PESA YA WAVUJA JASHO kiubwete....NA YEYE NI FISADI TU KAMA WENGINE.UBAYA UBAYA TUU......MPAKA KIELEWEKE.😕
 
Watu bana mbona mnapotosha mjadala wengine wanatumia lugha ambazo hazisistahili tutawareport kwa wahusika oooh!
 
Hivi huyu issa michuzi anafanya kazi ofisi gani ya serikali?
 
ahaaa
kumbe ndo maana nilikuwa nashangaa watu walivyokuja kichwa kichwa kwa kutoa shutuma kwa mtoa hoja badala ya kuijadili hoja yenwewe.

Basi narudia kusema kwamba hata shetani ana watetezi wake. (msiniquote vibaya sijamuita michuzi shetani ebo!)
 
 
Watu bana mbona mnapotosha mjadala wengine wanatumia lugha ambazo hazisistahili tutawareport kwa wahusika oooh!

kuna lugha gani chafu hapo juu????zaidi ya ukweli tuu...Hii nchi haitaendelea kama tutaendelea kuchekeana kihivyo,watu wanatumia vibaya nyadhifa zao ...watu mnasema wivu.HOW????😕
 
Hivi huyu issa michuzi anafanya kazi ofisi gani ya serikali?

Jamaa is supposed to be mwandishi na photo editor wa DAILY NEWS. Lakini cheki hiki kitu alichowahi kutamka Radio Butiama, Ohio. Niliposikia sikuamini masikio yangu:

"...hii blogu ni kama mdudu, akishakuingia hakutoki, na kweli, mimi sasa nimeprove kwamba ni kweli, kwa kweli, yani najikuta kwamba sasa hivi nakuwa dedicated zaidi huko kuliko hata huko Daily News. Saa zote naangalia vitu vya kuwapa wasomaji wangu..." (Hapa)
 
hehehehe
anatumia ofisi ya serikali kufanikisha kazi zake binafsi.... (hivi yale matangazo ktk blog yake analipia pasenti kwa bosi wake zaidi ya kodi)
And huyo ndiye mtanzania wa kupigiwa mfano teh teh wizi mtupu.

Kwa nini asije mtaani tujumuike ktk sekta binafsi kujiingizia faida??? Na kwa nini asiige mfano bora wa akina Invisible wa kuwa wajasiriamali wasioiegemea serikali ktk kuendesha forum???? wizi mtupu na ufinyu wa upeo kwa sana tu (na hasa wale wanaomtetea maana jamaa anajua afanyalo ila wao...).
 
hao ndio wanakula nchi na kumdanganya mkulu kuwa bado unakubalika.....wanatumbua tu maisha....siku zao zinahesabika...
 
 

Jamani jaman jamani, this is not fair at all. Hebu semeni wenyewe wangapi hivi leo ni waajiriwa aidha wa serikali au sekta binafsi na mna biashara/shughuli zenu binafsi za kijiongezea kipato na wakati mwingine hata mnachomoka kwenye ofisi zenu kwenda kufanikisha hizo shughuli zenu? Mbona wako walimu wengi wanaendekeza tuition zaidi na kutofundisha vizuri madarasani hampigi kelele? Mbona wako madaktari wengi wana kliniki au Hospitali zao na wakati mwingi wako huko hampigi kelele? Kwani Michuzi amelipiwa pesa na mwajiri wake kwenda kufanya shughuli zake binafsi? Si yuko kwenye kazi aliyotumwa na ofisi yake? Na wakati wa mapumziko anafanyakazi zake binafsi? Kwani hafanyi kazi aliyotumwa huko na anafanya kazi zake binafsi tuu? Hee! Ndugu zangu hebu tusipoteze mwelekeo wa mapambano dhidi ya mafisadi kwa kuletewa huu mjadala usio na tija hata kidogo. Nafikiri UW na dada yake Idda wametumwa kuja kutuvuruga hapa. Nasema acheni hizo tuendelee kuwaandama hawa mafisadi akina RA & co. ambao kwa hakika wamesababisha umaskini na taabu kwa ndugu zetu mpaka kieleweke. Aluta continua.
 

...Kwa vile wewe uko ughaibuni, unafurahia picha na updates huna cha kupoteza, lazima umpe credit Michuzi.

That's the nub of the whole thing really. Watu wanapenda kuona picha na ma update ya TZ. Hawana principle ya kusema, duu, huyu jamaa anatupa picha lakini anafanya haya kwa fursa, muda, camera ya serikali.

Hakutumwa Marekani kwenda kutengeneza video ya ma DJ wa Voice of America hukusu wanamuziki wa Marekani. Au kupiga picha akiwa na Chriss Tucker hotelini na "wadau" wengine wengine wasio na tija katika ku file reportza za DAILY NEWS.

Bosi wa DAILY NEWS anateuliwa na Rais, ni mtu mzito, anaweza na anatakiwa kum fire mwajiriwa anayetamka kwamba hana dedication na DAILY NEWS toka aanzishe blog.
 

Nashangaa unashabikia watu kutumia nafasi zao kuwezesha shughuli zao. Nasita kusema kuwa inawezekana na wewe uko kwenye kundi hilo kiasi kwamba unaona ni sawa kutumia muda au pesa za mwajiri kufanya mambo binafsi. Una element za ufisadi.

Huwezi kupanga cha kufanya hapa JF, fisadi ni fisadi. Yalekea kwa upande wako wewe FISADI ni RA & company. Nakukumbusha kuwa kwa JF fisadi ni fisadi, hata wewe kama ni fisadi tutakumulika, hata uwe fisadi sisimizi.

Bwana mashauri, wewe nani kakutuma?
 
 
 

Michuzi ni fisadi, na pia hayuko accountable na responsible kwa muajiri, wananchi anaowatumikia na taifa kwa ujumla.

Mtu responsible na accountable hawezi kupewa kazi na mwajiri wake, halafu badala ya kuwaambia wananchi ametumwa na mwajiri kuliwakilisha taifa, yeye anajigamba kwamba amekwenda vekesheni. Michuzi ni muongo. Kadanganya umma. Michuzi kakosa uzalendo.

Michuzi jiuzulu, waachie wenye moyo waifanye kazi hiyo.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…