Uchaguzi 2020 Issa Mtemvu, Kibamba inakuhitaji sana

Uchaguzi 2020 Issa Mtemvu, Kibamba inakuhitaji sana

Mgombea Ubunge katika Jimbo la Kibamba kupitia tiketi ya chama cha CCM Ndg. Issa Mtemvu kwa uchunguzi nilio ufanya ni kwamba wananchi wa jimbo la Kibamba wanakuhitaji sana ili uweze kutatua changamoto zao na endapo utachaguliwa hakikisha unatekeleza au unatatua mambo yafuatayo;

1. Barabara za mitaani ni mbovu sana haswa katika maeneo ya Kiluvya Gogoni, Hondogo n.k. Tafadhali hakikisha mradi wa DMDP unahamia ktk maeneo haya. Wananchi wanapata shida sana wakati wa mvua.

2. Tatizo la umeme kuwa na nguvu ndogo kutokana na uchache wa transfoma, hivyo kupelekea transfoma moja kuelemewa, katika maeneo ya Kiluvya Hondogo,

3. Zahanati/hospitali ya kata/wilaya.

4. Fufua ulinzi shirikishi katika maeneo hayo ili kuimarisha usalama.

5. Hakikisha mradi wa stendi ya mabasi unawanufaisha wakazi wa maeneo hayo na Dar es Salaam kwa ujumla.

6. Kibamba ni eneo la kimkakati kulingana na jografia yake ilivyo kwani ndio lango la jiji hivyo itangaze tupate wawekezaji katika meneo haya ili wananchi wapate maendeleo.

Wananchi wa jimbo la Kibamba walicheleweshwa sana katika maendeleo yao, safari hii hawatofanya makosa.
Kwahiyo wamelipwa FIDIA ya kubomolewa nyumba zao na huku pakiwepo zuio la Mahakama Kuu mpk Kibamba ichukuliwe na CCM. Wana maumivu makubwa sana na uhalamia waliofanyiwa. Mtu kasitafu baada ya kujenga nyumba kwa miaka 30 ya utumishi wake. Leo unabomoa bila kujali amri ya mahakama. Haki iko wap tena eti mita 120 kila upande. Alaf unaishia kutumia mita 50 tu. Mita 110 umeonea watu masikin alaf uje kuomba kura daah.watu aibu hawana
 
Magufuli kasema hataki kuchanganyiwa betirii na "gunzi" wewe mchague mtevu ili ujihakikishie maendeleo ya jimbo lako vinginevyo huyo unaye mtaji hatambuliki kwa Magufuli.
na kasema ukimchanganyia sahau kuhusu maendeleo.hivyo usipoteze kura yako kwa mbuge wa upinzani bora kumpa wa ccm
Mnakusanya hela zetu kwa jina la kodi, kwenye maendeleo mnatusimanga, kwanini?
 
jambo dogo tu la kujiuliza ni, kama serikali inaundwa na CCM inamaaana Mbunge wa CCM ndio atakuwa na uwezo wa kusikilizwa na Rais zaidi kuliko Mbunge wa chama kingine. Hivyo huna sababu ya kupoteza kura yako kumchagua mbunge wa chama kingine ni bora ukamchagua huyo mbunge wa CCM ndiye atakuwa karibu na Rais kuzungumza changamoto zinazo wakabili ktk maeneo yenu
 
nimefanya utafiti na nimebaini kuwa ktk majimbo ambayo hawataki kusikia chama cha upinzani ni jimbo la Kibamba, inaonekana Mnyika ndiye aliharibu ktk kipindi chake cha miaka 10, hakuna alicho fanya. sasa safari hii ccm watateleza tu
Hilo Jimbo Wana Jambo lao tarehe 28 CCM hawatoboi
 
Magufuli kasema hataki kuchanganyiwa betirii na "gunzi" wewe mchague mtevu ili ujihakikishie maendeleo ya jimbo lako vinginevyo huyo unaye mtaji hatambuliki kwa Magufuli.
na kasema ukimchanganyia sahau kuhusu maendeleo.hivyo usipoteze kura yako kwa mbuge wa upinzani bora kumpa wa ccm
Magufuli mwenyewe Urais anapumulia mashine.Waulize vyombo vya usalama watakwambia joto lilivyo huko ndani
 
kwa muda wa miaka 10 John Mnyika wa Chadema alikuwa mbunge wa Jimbo la Kibamba....hakuna alicho fanya zaidi ya kujilimbikizia utajiri na kisha akakimbia.....leo tena mnataka kurubuniwa na huyooo.....mtakuwa watu wa ajaabu kweli...
hapana jamani....Kura ni siri ..nenda kampigie Mtenvu
Mradi wa Stendi ya Kibamba,Hospital Mlonganzila,Mradi wa Maji,kudai wananchi walipwe fidia japo Magufuli alikataaa,ulitaka afanye Nini zaidi?
 
kwa muda wa miaka 10 John Mnyika wa Chadema alikuwa mbunge wa Jimbo la Kibamba....hakuna alicho fanya zaidi ya kujilimbikizia utajiri na kisha akakimbia.....leo tena mnataka kurubuniwa na huyooo.....mtakuwa watu wa ajaabu kweli...
hapana jamani....Kura ni siri ..nenda kampigie Mtenvu

Itakuwa hivo hata kwa Mtemvu. Matatizo ya nchi hii ni zaidi ya mbunge kutatua. Ungenipa mfano wa jimbo lolote la CCM ambalo wao kwa kuwa na mbunge wa CCM mambo yaliyotajwa na mleta mada kwao hayako.

Ungefahamu ni nani hasa anaamua nini kifanyike ungejua mbunge si mhusika. Umeshawahi kusikia waziri akipigiwa simu hadharani na kuambiwa “leta watu wako hapa wafanye hiki na nitatoa hizo bilioni tano” - hao ndio waamuzi wa nini kifanyike. Si mbunge wala waziri!!
 
kwa maneno yako yanamaanisha ni angalau kumchagua mbuge wa ccm kuliko wa upinzani
 
Mpelekeni Mtemvu ili iwe rahisi kufikisha kero zenu kwa Rais Magufuli
 
Back
Top Bottom