Makengeza, si bure unaitwa Makengeza. Wanajulikana sana kama wasiojulikana. Richard Mabala, mwandishi mahiri, anajulikana sana kama Makengeza na lile pua lake. Wanajulikana sana wasiojulikana!
Mchezo umeishaanza wa safari ya wasiojulikana wanaojulikana. Wimbo wa Jualikali, Kibajaji na Musukuma na kiitikio cha Spika umefana sana. Yale makofi ya watunga sheria wetu ni ushahidi tosha. Muruto, licha ya maneno ya kuisumbua serkali kusikika na washambuliaji, anasema shambulio lisihusishwe na siasa! Kwa upelelezi upi kusema hayo?