mimi kama mtanzania mpenda haki na amani, ninao wajibu wa kutoa yangu ya moyoni
ushauri uliokuwa umetolewa na rais wetu kwa rais wa rwanda juu ya kiongozi huyo kuangalia uwezekanpo wa kukaa na waasi nchini rwanda ulikuwa muafaka, sisi sote tunajua kuwa palipo na kutokuelewana lazima watu waweze kukaa na kuzungumuza
lakini rais kikwete akupaswa kutoa ushauri nyeti wa namna hii kupitia mkutano akiwa nchini ethopia bali alipaswa yeye kumueleza kiongozi mwenzie kama ushauri binafsi wa kumsaidia katika uongozi wake, kwa kufanya vile ni kama rais kikwete alikuwa anamshutumu kiongozi mwenzie. Viongozi hao ni mara kwa mara wanakutana kwenye vikao vyao vya jumuiya ya afrika mashariki, kwa nini asingetumia muda huo kakaa naye akamshauri ? Ndio maana nasema ushauri ulikuwa mzuri lakini njia haikuwa sahihi
pia leo nimesoma gazeti la raia mwema, rais wetu akiwa nchini malawi anawashutumu viongozi wa upinzani kuwa ndio wanaokuuza malumbano baina ya rwanda na tanzania, kwa kweli napo katika hilo naona ameendelea kufanya kosa kiongozi wetu. Kwa nini yeye akiwa kiongozi wa nchi asikae na hao wapinzani na kujadili kama anaona ndio wanaoukuza mgogoro huo. Mimi nijuavyo mahusiano ya rwanda na tanzania ni mazuri kabisa isipokuwa tatizo lipo kwa mambo yao binafsi kati ya rais wetu na yule wa rwanda
kwa kitendo alichokifanya mh. Rais cha kuwalaumu wapinzani akiwa nchini malawi sidhani kama kinajenga umoja miongoni mwa chama tawala na vyama pinzani. Mara zote ni vizuri kutafakari kabla ya kutamka