macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 25,191
- 48,765
Hee hee hee ''Your excellency i am just trying to preach but .... but I can't reach you'' alisikika Magufuli akimwambia rais wa Malawi. Hii ni tafsiri ya moja kwa moja ya neno kwa neno, hata Google nafuu. ''Mheshimiwa najaribu tu kuhubiri lakini siwezi kukufikia (level yako ya kuhubiri)''Mimi naanza kushawishika kuwa Magufuli anaogopa kwenda nje ya Afrika kwa sababu anajua haimudu vizuri lugha ya Kiingereza.
Maana nje ya Afrika itakuwa ngumu kwa yeye kuzungumza Kiswahili.
Lakini ndani ya Afrika anaweza kuzuga kuwa kwa kuongea Kiswahili, anakuwa anaienzi lugha hiyo.
Deep down naamini hata yeye anajua kuwa Kiingereza hakimudu vizuri....
Mimi huwa namwonea huruma sana anavyokuwa anajikakamua anapozungumza kiingereza. Inaonekana tangu zamani amekuwa anachekwa au anaona aibu kuzungumza hivyo anakuwa anajishtukia mwenyewe. Ameshaingia kwenye vicious circle mbaya sana ya kutojiamini. Naona tatizo lake liko zaidi kwenye kutojiamini na kuona aibu kuliko kujua kiingereza. Ni lazima atakuwa anaweza kuongea vizuri zaidi lakini kutojiamini na aibu kunachangia afanye vibaya zaidi.