It is officially: Ujenzi wa reli ya Tanzania mpaka Rwanda kuanza Oktoba mwaka 2018

It is officially: Ujenzi wa reli ya Tanzania mpaka Rwanda kuanza Oktoba mwaka 2018

REDEEMER.

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2015
Posts
8,925
Reaction score
14,890

Serikali ya Tanzania na Rwanda kupitia mawaziri wanaohusika na ujenzi wamesaini makubaliano ya kuanza ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Isaka hadi Kigali ifikapo Oktoba mwaka huu.
3244834

Tukio hilo limewakutanisha mawaziri watatu wa Tanzania ambao ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Augustine Mahiga pamoja na Waziri wa Ujenzi wa Rwanda, James Musoni huku wakiwa wameongozana na wataalamu mbalimbali wa miundombinu kutoka nchi hizo.

Kabla ya kusaini makubaliano hayo yaliyofanyika jana Januari 20,2018 ,jijini Dar es salaam, mawaziri wamepokea rasimu ya ujenzi wa reli hiyo na kuijadili kabla ya kupitisha rasmi.

"Reli hii ni biashara, lazima tufanye haraka, itasaidia kukuza uchumi nchini, kuongezeka fedha za kigeni, barabara zetu zitadumu, watu wetu watakuza biashara zao, "amesema Waziri Mpango.

Kwa mujibu wa mapendekezo ya rasimu hiyo iliyoandaliwa na makatibu wakuu kutoka Rwanda na Tanzania, mradi huo ulioanza mchakato wake miaka mitatu iliyopita, sasa utaanza ujenzi wake rasmi baada ya kuwekwa jiwe la msingi Oktoba mwaka huu na marais wa nchi hizo.

Makubaliano yaliyofanyika jana Jumamosi ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya wakuu wa nchi hizo mbili kupitia ziara ya rais Paul Kagame Januari 12, mwaka huu.

Akiwasilisha rasimu hiyo kabla ya kupitishwa, Mkurugenzi wa Miundombinu kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Rogatus Mativila amesema rasimu imependekeza njia mbili za ufanikishaji wa mradi huo wenye urefu wa kilometa 521.

Mativila amesema njia ya kwanza ni kushirikisha sekta binafsi na njia ya pili ni kutumia bajeti za serikali mbili kwa kila nchi kugharamia kipande kilicho katika nchi yake.

Kabla ya kusaini, Waziri Mpango amesema Januari 29, viongozi hao wanakutana tena katika vikao vya ndani kwa ajili ya kujadili upatikanaji wa gharama za mradi.
 
Swali,kipande cha kutoka makutopora hadi hapo isaka mbona sijaskia mchakato wake??
Kaka ujenzi wa reli toka Dar hadi Mwanza linahusu Tanzania pekee, hilo lipo katika ratiba na bajeti ya Tanzania, linafanywa kwa awamu tano, zimeshaanza mbili, wakati wowote utasikia tenda ya Makutopora Tabora inatangazwa.

Kipande cha Isaka hadi mpakani wa Rusumo na kutoka Rusumo hadi Kigali, hivi vinategemeana, kama kimoja hakifanyiki, basi kingine hakina maana tena, kama Tanzania hawafikishi reli hadi ampaka wa Rusumo, badi kipande cha Rusumo Kigali hakina maana, na Kama Rwanda haitojenga reli toka Kigali hadi Rusumo, kipande cha Isaka hadi Rusumo hakina sababu ya kujengwa, kwahiyo ujenzi wa vipande hivi viwili lazim viwe coordinated na kujengwa kwa pamoja ili nchi moja iseje kupata hasara kwa nchi nyingine kushindwa kujenga upande wake.
 
Ila hii SGR yetu itaondoa mamia ya mabasi kwenye route zao kwa kiasi kikubwa sana najaribu kuangazia basi za Dar Moro zilivyo nyingi, Dar Dom zilivyo nyingi, Dar Kahama, Dar Tabora, Dar Shinyanga, Dar Mwanza, Dar Kigali itakua kilio kwa regional busses.

Mbarawa juzi kasema SGR itafika mpaka Mtwara (tenda itatangazwa hivi karibuni), kisha Tanga na Arusha so hali ni tete.
 
Rwanda, Tanzania to jointly mobilise funds for SGR
By: JAMES KARUHANGA
PUBLISHED: January 21, 2018

Ministers for Infrastructure of Rwanda and Tanzania yesterday met in Dar es Salaam, Tanzania, to consider implementation of the countries’ joint 521kilometre Isaka-Kigali Standard Gauge Railway (SGR) project which is estimated to cost $2.5 billion.

Besides adoption of feasibility studies already conducted in the two countries, key outcomes also include an agreement to lay the foundation stone by October, and the two countries jointly mobilizing funds for construction of the joint project with each country meeting the cost of infrastructure in its own territory.

A related joint communiqué indicates that James Musoni, Rwanda’s minister of infrastructure, was invited to visit Tanzania from Friday to Saturday, by his counterpart, Prof. MakameMbarwa, Tanzania’s minister of works, transport and communications.

On Saturday, the two ministers held a meeting to arrange the implementation of the two countries’ Presidents given on January 14 that ministers responsible for transport in the two countries meet within two weeks to deliberate on how to implement construction of the joint railway line.

“The Ministers meeting was preceded by the meeting of the Permanent Secretaries responsible for transport of the two countries and the Permanent Secretary of Finance and Planning of Tanzania,” reads part of the communiqué.

“The Ministers reiterated their strong commitment to further strengthen the relationship for the mutual benefits of the two countries and their people and the prevailing commitment to realize the implementation of the Isaka-Kigali railway project and its significance to reduce transport cost, foster physical integration of transport modes, economic growth and improved social services in the sub region.”

The meeting was also attended by Tanzania’s minister of Foreign Affairs and East Africa Cooperation, Dr. Augustine Mahiga, and other senior government officials from both countries.

Deliberations were on key implementation issues of the project, including: progress already made by Tanzania on construction of the SGR – from Dar to Morogoro and from Morogoro to Makutupora; and they also agreed to adopt the railway feasibility studies already conducted in the two countries.

The ministers adopted the proposed project delivery method of design and build similar to the Dar to Morogoro and Morogoro to Makutupora SGR project for purpose of uniformity of standards.

“Issues regarding train operations and track access shall be agreed in future separately,” reads the joint communiqué.

Furthermore, the ministers agreed on the proposal to adopt the setup of the existing joint technical monitoring committee for the Dar-Isaka to Kigali or Keza-Musongati (DIKKM) project reduced to Tanzania and Rwanda.

They adopted the proposed timeline towards implementation of the Presidents’ directives so as to lay the foundation stone by October, 2018.

Rwanda and Tanzania agreed on joint construction of the SGR from Isaka (northwestern Tanzania) to Kigali, to facilitate movement of goods and services, following a meeting between Presidents Paul Kagame and John PombeMagufuli, during the former’s one-day working visit to Dar-es-Salaam, mid this month.

After the leaders’ meeting, President Magufuli, among others, said they want the construction “to start immediately” because the feasibility studies and designs are complete.

Nearly 80 per cent of Rwanda’s imports and exports go through Tanzania.

Sources say both countries ministers of finance are scheduled to meet in Dar on January 29 on the same project and to discuss on the finance mechanism of the joint project.

editorial@newtimes.co.rw

Rwanda, Tanzania to jointly mobilise funds for SGR
 
Ila hii SGR yetu itaondoa mamia ya mabasi kwenye route zao kwa kiasi kikubwa sana najaribu kuangazia basi za Dar Moro zilivyo nyingi, Dar Dom zilivyo nyingi, Dar Kahama, Dar Tabora, Dar Shinyanga, Dar Mwanza, Dar Kigali itakua kilio kwa regional busses.

Mbarawa juzi kasema SGR itafika mpaka Mtwara (tenda itatangazwa hivi karibuni), kisha Tanga na Arusha so hali ni tete.
Ikifika Arusha na uko mtwara basi watapiga hela hawajakaa waamini...trust me movement za Arusha dar ni nyingi sana...hela zipo waache kupuuza iyo route
 
Ila hii SGR yetu itaondoa mamia ya mabasi kwenye route zao kwa kiasi kikubwa sana najaribu kuangazia basi za Dar Moro zilivyo nyingi, Dar Dom zilivyo nyingi, Dar Kahama, Dar Tabora, Dar Shinyanga, Dar Mwanza, Dar Kigali itakua kilio kwa regional busses.

Mbarawa juzi kasema SGR itafika mpaka Mtwara (tenda itatangazwa hivi karibuni), kisha Tanga na Arusha so hali ni tete.
Hata Ulaya na Marekani treni za umeme zipo lakini haijazuia watu kupanda mabasi.Hata mwendokasi upo haijazuia watu kupanda mabasi ya kawaida.Hata treni ya gongo la mboto ipo haijazuia watu kupanda mabasi
 
TRL Itakuwa listed later on so wenye mabasi wanaweza kufahidika. Na pia kama usafiri wa mabasi haujafa Ulaya kwann ufe Bongo? Sanasana naona utapunguza gharama za mabasi
 
Kutoka Dar kwenda Mwanza ni saa 18 ikiescape torch ni saa 17 wakati train ni saa 8 sasa ni nani mwenye muda wa kukaa kwenye kitu masaa 17 wakati kuna alternative ya saa 8?

Wanaweza wakawepo ila ni 10 out of 100 so bado ni hasara kwa busses.
 
Hapo lazima pawe na diversification of economy mbona sumry kaona competition kubwa kahamia kwenye kilimo.Hapo hamna namna lazima iwe hivyo
 
TRL Itakuwa listed later on so wenye mabasi wanaweza kufahidika. Na pia kama usafiri wa mabasi haujafa Ulaya kwann ufe Bongo? Sanasana naona utapunguza gharama za mabasi
Hata hivyo lilitakiwa liwe listed long before ila sababu tayari ni independent company litafanya kazi sasa kibiashara zaidi easy profit no competitors
 
Back
Top Bottom