It is officially: Ujenzi wa reli ya Tanzania mpaka Rwanda kuanza Oktoba mwaka 2018

Hata hivyo lilitakiwa liwe listed long before ila sababu tayari ni independent company litafanya kazi sasa kibiashara zaidi easy profit no competitors
Share zake zingedorora TRL walikosea kuwauzia RITES kampuni.
 
Na hiyo rites ndio iliopelekea TRL kuwa worst ever awali kabla hawajawapa wahindi walikua somehow at least ila walivyopewa rites mpaka zile route za tanga moshi Arusha wakaziua kabisa, kadogosa ndio amelifufua shirika.

Hizi proposed SGR routes zote zikikamilika TRL litakua shirika lenye ukwasi wa kutisha baada ya miaka 10 tu.
 
TRL Itakuwa listed later on so wenye mabasi wanaweza kufahidika. Na pia kama usafiri wa mabasi haujafa Ulaya kwann ufe Bongo? Sanasana naona utapunguza gharama za mabasi
kumbe hitachi wanatengeneza Train??
 
Tupeni mrejesho wa awamu ya kwanza. Tumefikia wapi . Tuwekeeni picha tujidai na sisi
 
Ila hii SGR yetu itaondoa mamia ya mabasi kwenye route zao kwa kiasi kikubwa sana najaribu kuangazia basi za Dar Moro zilivyo nyingi, Dar Dom zilivyo nyingi, Dar Kahama, Dar Tabora, Dar Shinyanga, Dar Mwanza, Dar Kigali itakua kilio kwa regional busses.

Mbarawa juzi kasema SGR itafika mpaka Mtwara (tenda itatangazwa hivi karibuni), kisha Tanga na Arusha so hali ni tete.
ndio changomoto ya teknolojia hiyo mkuu lazima upande fulani uumie ila kwa faida ya wengi na usalama pia
 
Tupeni mrejesho wa awamu ya kwanza. Tumefikia wapi . Tuwekeeni picha tujidai na sisi
Kuna fununu serikali inazuia picha, ije kuzitoa kupitia media ikulu. Wanapendaga sifa.
 
Pacha wa thread hii huyu hapa:

It is officially: Ujenzi wa reli ya Tanzania mpaka Rwanda kuanza Oktoba mwaka 2018
 
Ila hii SGR yetu itaondoa mamia ya mabasi kwenye route zao kwa kiasi kikubwa sana najaribu kuangazia basi za Dar Moro zilivyo nyingi, Dar Dom zilivyo nyingi, Dar Kahama, Dar Tabora, Dar Shinyanga, Dar Mwanza, Dar Kigali itakua kilio kwa regional busses.

Mbarawa juzi kasema SGR itafika mpaka Mtwara (tenda itatangazwa hivi karibuni), kisha Tanga na Arusha so hali ni tete.
Wataya-divert sehemu zingine.
 
Me sio mwepesi kushangilia maandishi hadi nione imeanza tekelezwa,tumelishwa maneno matamu mengi sana na ccm toka Uhuru,tunaelekea kuzeeka hakuna cha maana tangible kimefangika
 
Wenye uzi mbona kimya? Hii white elephant kama ile bagamoyo mbona haina funding?
 
Serikali ya Tanzania na Rwanda kupitia mawaziri wanaohusika na ujenzi wamesaini makubaliano ya kuanza ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Isaka hadi Kigali ifikapo Oktoba mwaka huu.
3244834

Tukio hilo limewakutanisha mawaziri watatu wa Tanzania ambao ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Augustine Mahiga pamoja na Waziri wa Ujenzi wa Rwanda, James Musoni huku wakiwa wameongozana na wataalamu mbalimbali wa miundombinu kutoka nchi hizo.

Kabla ya kusaini makubaliano hayo yaliyofanyika jana Januari 20,2018 ,jijini Dar es salaam, mawaziri wamepokea rasimu ya ujenzi wa reli hiyo na kuijadili kabla ya kupitisha rasmi.

"Reli hii ni biashara, lazima tufanye haraka, itasaidia kukuza uchumi nchini, kuongezeka fedha za kigeni, barabara zetu zitadumu, watu wetu watakuza biashara zao, "amesema Waziri Mpango.

Kwa mujibu wa mapendekezo ya rasimu hiyo iliyoandaliwa na makatibu wakuu kutoka Rwanda na Tanzania, mradi huo ulioanza mchakato wake miaka mitatu iliyopita, sasa utaanza ujenzi wake rasmi baada ya kuwekwa jiwe la msingi Oktoba mwaka huu na marais wa nchi hizo.

Makubaliano yaliyofanyika jana Jumamosi ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya wakuu wa nchi hizo mbili kupitia ziara ya rais Paul Kagame Januari 12, mwaka huu.

Akiwasilisha rasimu hiyo kabla ya kupitishwa, Mkurugenzi wa Miundombinu kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Rogatus Mativila amesema rasimu imependekeza njia mbili za ufanikishaji wa mradi huo wenye urefu wa kilometa 521.

Mativila amesema njia ya kwanza ni kushirikisha sekta binafsi na njia ya pili ni kutumia bajeti za serikali mbili kwa kila nchi kugharamia kipande kilicho katika nchi yake.

Kabla ya kusaini, Waziri Mpango amesema Januari 29, viongozi hao wanakutana tena katika vikao vya ndani kwa ajili ya kujadili upatikanaji wa gharama za mradi.
Its official.... Sio its officially... English ngumu
 
Kwa umeme gani labda tuswaze masaa machache ya kufika mwanza bila resource
 
Wewe ndio mwenye akili sana kuliko wataalam waliokaa na kuleta hii project?

Kaa subiri train iletwe ikose umeme ndio uongee otherwise you should shut up.
 
Back
Top Bottom