Geza Ulole
JF-Expert Member
- Oct 31, 2009
- 65,136
- 91,917
Share zake zingedorora TRL walikosea kuwauzia RITES kampuni.Hata hivyo lilitakiwa liwe listed long before ila sababu tayari ni independent company litafanya kazi sasa kibiashara zaidi easy profit no competitors
Na hiyo rites ndio iliopelekea TRL kuwa worst ever awali kabla hawajawapa wahindi walikua somehow at least ila walivyopewa rites mpaka zile route za tanga moshi Arusha wakaziua kabisa, kadogosa ndio amelifufua shirika.Share zake zingedorora TRL walikosea kuwauzia RITES kampuni.
kumbe hitachi wanatengeneza Train??TRL Itakuwa listed later on so wenye mabasi wanaweza kufahidika. Na pia kama usafiri wa mabasi haujafa Ulaya kwann ufe Bongo? Sanasana naona utapunguza gharama za mabasi
ndio changomoto ya teknolojia hiyo mkuu lazima upande fulani uumie ila kwa faida ya wengi na usalama piaIla hii SGR yetu itaondoa mamia ya mabasi kwenye route zao kwa kiasi kikubwa sana najaribu kuangazia basi za Dar Moro zilivyo nyingi, Dar Dom zilivyo nyingi, Dar Kahama, Dar Tabora, Dar Shinyanga, Dar Mwanza, Dar Kigali itakua kilio kwa regional busses.
Mbarawa juzi kasema SGR itafika mpaka Mtwara (tenda itatangazwa hivi karibuni), kisha Tanga na Arusha so hali ni tete.
Kuna fununu serikali inazuia picha, ije kuzitoa kupitia media ikulu. Wanapendaga sifa.Tupeni mrejesho wa awamu ya kwanza. Tumefikia wapi . Tuwekeeni picha tujidai na sisi
hehehe,ni unjenzi ni siriKuna fununu serikali inazuia picha, ije kuzitoa kupitia media ikulu. Wanapendaga sifa.
Wataya-divert sehemu zingine.Ila hii SGR yetu itaondoa mamia ya mabasi kwenye route zao kwa kiasi kikubwa sana najaribu kuangazia basi za Dar Moro zilivyo nyingi, Dar Dom zilivyo nyingi, Dar Kahama, Dar Tabora, Dar Shinyanga, Dar Mwanza, Dar Kigali itakua kilio kwa regional busses.
Mbarawa juzi kasema SGR itafika mpaka Mtwara (tenda itatangazwa hivi karibuni), kisha Tanga na Arusha so hali ni tete.
samsung anatengeneza hadi vifaru na magari ya vita!..nakazia tu!kumbe hitachi wanatengeneza Train??
Jiandaeni kwa maumivu zaidi, ila maumivu yakizidi, ruksa kumuona daktari.[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]Wazee wa kulaunch bado wanalaunch. Waiter niongeze tusker mbili
Its official.... Sio its officially... English ngumu
Serikali ya Tanzania na Rwanda kupitia mawaziri wanaohusika na ujenzi wamesaini makubaliano ya kuanza ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Isaka hadi Kigali ifikapo Oktoba mwaka huu.
Tukio hilo limewakutanisha mawaziri watatu wa Tanzania ambao ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Augustine Mahiga pamoja na Waziri wa Ujenzi wa Rwanda, James Musoni huku wakiwa wameongozana na wataalamu mbalimbali wa miundombinu kutoka nchi hizo.
Kabla ya kusaini makubaliano hayo yaliyofanyika jana Januari 20,2018 ,jijini Dar es salaam, mawaziri wamepokea rasimu ya ujenzi wa reli hiyo na kuijadili kabla ya kupitisha rasmi.
"Reli hii ni biashara, lazima tufanye haraka, itasaidia kukuza uchumi nchini, kuongezeka fedha za kigeni, barabara zetu zitadumu, watu wetu watakuza biashara zao, "amesema Waziri Mpango.
Kwa mujibu wa mapendekezo ya rasimu hiyo iliyoandaliwa na makatibu wakuu kutoka Rwanda na Tanzania, mradi huo ulioanza mchakato wake miaka mitatu iliyopita, sasa utaanza ujenzi wake rasmi baada ya kuwekwa jiwe la msingi Oktoba mwaka huu na marais wa nchi hizo.
Makubaliano yaliyofanyika jana Jumamosi ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya wakuu wa nchi hizo mbili kupitia ziara ya rais Paul Kagame Januari 12, mwaka huu.
Akiwasilisha rasimu hiyo kabla ya kupitishwa, Mkurugenzi wa Miundombinu kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Rogatus Mativila amesema rasimu imependekeza njia mbili za ufanikishaji wa mradi huo wenye urefu wa kilometa 521.
Mativila amesema njia ya kwanza ni kushirikisha sekta binafsi na njia ya pili ni kutumia bajeti za serikali mbili kwa kila nchi kugharamia kipande kilicho katika nchi yake.
Kabla ya kusaini, Waziri Mpango amesema Januari 29, viongozi hao wanakutana tena katika vikao vya ndani kwa ajili ya kujadili upatikanaji wa gharama za mradi.
Kwa umeme gani labda tuswaze masaa machache ya kufika mwanza bila resource

Wewe ndio mwenye akili sana kuliko wataalam waliokaa na kuleta hii project?Kwa umeme gani labda tuswaze masaa machache ya kufika mwanza bila resource