IT wabongo, Elon Musk katoa shavu kwenu! Tumeni kazi zenu!

Kuna ka kijana kangu katundu sana ngoja niendelee kukaacha kavumbue vumbue vitu..kuna siku katuambia kitu kwny gari hata hatukuwa tunajua kama kunauwezekano wa kufanya hivyo...ni vingi tuu amekua msaada japo yupo drs la 5....kuna siku katakua huko kwa Elon musk
 
Shida ya Bongo IT anajifunza codes yupo Chuo anamiaka labda 19 kuendelea unategemea uwezo wake ufanane na wa Mzungu anayejifunza codes akiwa na miaka 10.
 
Badili kichwa cha habari jomba. Jinsi ulivyoiweka ni kama Elon katoa shavu kwa ma IT wa bongo specifically!
 
Shida ya Bongo IT anajifunza codes yupo Chuo anamiaka labda 19 kuendelea unategemea uwezo wake ufanane na wa Mzungu anayejifunza codes akiwa na miaka 10.
Hilo sio tatizo, akiwa na consistency ya miaka miwili Hadi mitatu seriously anakuwa mkali tu sanaaa huenda hata zaidi ya walio mtangulia
 
UKO SERIOUS KWELI???

Unaijua codes? Au unahisi ni notes za history unakalili?
 
Kuna ka kijana kangu katundu sana ngoja niendelee kukaacha kavumbue vumbue vitu..kuna siku katuambia kitu kwny gari hata hatukuwa tunajua kama kunauwezekano wa kufanya hivyo...ni vingi tuu amekua msaada japo yupo drs la 5....kuna siku katakua huko kwa Elon musk
Msaidieni kukiendeleza kipaji chake, uelekeo umeshaonekana.
 
Hilo sio tatizo, akiwa na consistency ya miaka miwili Hadi mitatu seriously anakuwa mkali tu sanaaa huenda hata zaidi ya walio mtangulia
Sawa jitihada zinamfanya mtu awe bora lakini mzungu mwenye consistency ya codes toka akiwa na miaka kumi experience yake sio sawa na mbongo mwenye consistency ya codes toka akiwa na miaka 19. Hata Elon Musk alianza kujishughulisha na computer tangu akiwa mdogo.
 
Bongo hamna IT ni wazugaji tu.

Nilipeleka simu yangu kwa jamaa aliyesifika kuwa ni nguli wa ku unlock network.

Nilipofika pale akanitajia bei nikasema poa nitalipia akaniambia kaa hapo. Kacheza nayo pale mezani na laptop yake kama lisaa hivi kila akigusa ngoma ngumu.

Baada ya muda jamaa akashusha laptop chini so nikawa sioni kinachoendelea.

Then kama sekunde kadhaa akiwa huko chini nikasikia "welcome guys this is my YouTube channel and today we'll learn how to unlock network" kabla hata haijamaliza nikamwambia hiyo tutorial ya huyo muhindi hata mimi nimeiangalia.

Akasimama akasema "eeeeh basi hii haiwezekani mzee"
Huyo siyo IT. Ni tap kid, yaani wale wanaotatua matatizo ya tech device kwa kugoogle au kuangalia tutorials za YouTube.
 
Sawa jitihada zinamfanya mtu awe bora lakini mzungu mwenye consistency ya codes toka akiwa na miaka kumi experience yake sio sawa na mbongo mwenye consistency ya codes toka akiwa na miaka 19. Hata Elon Musk alianza kujishughulisha na computer tangu akiwa mdogo.
Code ni sanaa, code ni kichwa cha mtu namna alivyopesi kufikiri na kupata majibu. Kuna hao wabongo walio julia code ukubwani, wanafanya vizuri sana huko ulaya kuliko hao waliojifunza utotoni..
 
Shida ya Bongo IT anajifunza codes yupo Chuo anamiaka labda 19 kuendelea unategemea uwezo wake ufanane na wa Mzungu anayejifunza codes akiwa na miaka 10.
Sio miaka 10, ni miaka 4.

Miaka flani kuna dogo nilisoma nae shule ya msingi ila nilimtangulia darasa moja.

Baadae tukakutana chuo kikuu, akisoma computer Science, siku moja nakutana nae computer lab nadhani ndio alikua ameripoti chuo ana kama wiki 1 ama 2, tukakutana lab, ananiuliza mouse ni ipi? Nikasema hapa kazi ipo.

Leo hii ni peogrammer ama ICT specialist kwenye taasisi moja hivi.

Point yangu ni kwamba Tanzania watu wanachelewa sana kuijua computer, watu tunakutana na computer chuo kikuu kweli? Atleast miaka hii kuna ahueni kidogo sio kama miaka ile niliyosoma mimi.

Mimi mwenyewe computer niliiona siku bro wangu amekuja likizo kutoka chuo kikuu nikiwa form 3, niliishangaa na nilikesha siku hiyo naichezea😂
 
Lazima uwe best of the best, Kuna watu huwa nawaambia dunia inapoelekea lazima ufanye vitu viwe, watu wanataka matokeo.
 
Bongo hamna IT ni wazugaji tu.

Nilipeleka simu yangu kwa jamaa aliyesifika kuwa ni nguli wa ku unlock network.

Nilipofika pale akanitajia bei nikasema poa nitalipia akaniambia kaa hapo. Kacheza nayo pale mezani na laptop yake kama lisaa hivi kila akigusa ngoma ngumu.

Baada ya muda jamaa akashusha laptop chini so nikawa sioni kinachoendelea.

Then kama sekunde kadhaa akiwa huko chini nikasikia "welcome guys this is my YouTube channel and today we'll learn how to unlock network" kabla hata haijamaliza nikamwambia hiyo tutorial ya huyo muhindi hata mimi nimeiangalia.

Akasimama akasema "eeeeh basi hii haiwezekani mzee"
😂😂😂😂 Hii ilinitokea pia kariakoo, fundi nguli kafail, akasema nakuja., akatokomea huko😏
 
Back
Top Bottom